Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Ngazi za hukumu na Mipango

Hadithi 4

Ewe kijana, hakika mimi ninakufundisha maneno, muhifadhi Mwenyezi Mungu naye atakuhifadhi, muhifadhi Mwenyezi Mungu utamkuta uendako, utakapoomba basi muombe Mwenyezi Mungu, na utakapotaka msaada basi taka msaada kwa Mwenyezi Mungu

عن ابن عباس رضي الله عنهما قال: كُنْتُ خَلْفَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمًا، فَقَالَ: «يَا غُلَامُ، إِنِّي أُعَلِّمُكَ كَلِمَاتٍ، احْفَظِ اللهَ يَحْفَظْكَ، احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ تُجَاهَكَ، إِذَا سَأَلْتَ فَاسْأَلِ اللهَ، وَإِذَا اسْتَعَنْتَ فَاسْتَعِنْ بِاللهِ، وَاعْلَمْ أَنَّ الْأُمَّةَ لَوِ اجْتَمَعَتْ عَلَى أَنْ يَنْفَعُوكَ بِشَيْءٍ، لَمْ يَنْفَعُوكَ إِلَّا بِشَيْءٍ قَدْ كَتَبَهُ اللهُ لَكَ، وَلَوِ اجْتَمَعُوا عَلَى أَنْ يَضُرُّوكَ بِشَيْءٍ، لَمْ يَضُرُّوكَ إِلَّا بِشَيْءٍ قَدْ كَتَبَهُ اللهُ عَلَيْكَ، رُفِعَتِ الْأَقْلَامُ وَجَفَّتِ الصُّحُفُ».
Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- amesema: Siku moja nilikuwa nyuma ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: "Ewe kijana, hakika mimi ninakufundisha maneno, muhifadhi Mwenyezi Mungu naye atakuhifadhi, muhifadhi Mwenyezi Mungu utamkuta uendako, utakapoomba basi muombe Mwenyezi Mungu, na utakapotaka msaada basi taka msaada kwa Mwenyezi Mungu, na tambua kuwa umma mzima lau wangekusanyika ili wakunufaishe kwa chochote, basi wasingelikunufaisha isipokuwa kwa kitu alicho kuandikia Mwenyezi Mungu kuwa chako, na lau kama wangelikusanyika ili wakudhuru kwa chochote, basi wasingeweza kukudhuru isipokuwa kwa kitu alichokiandika Mwenyezi Mungu dhidi yako, kalamu zimenyanyuliwa na kurasa zimekauka".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yake- kuwa yeye alipokuwa kijana mdogo alikuwa kapanda pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akasema kumwambia -Amani iwe juu yake-: Hakika mimi ninakufundisha vitu na mambo ambayo Mwenyezi Mungu atakunufaisha kwayo: Muhifadhi Mwenyezi Mungu kwa kuhifadhi maamrisho yake na kuepuka makatazo yake, kiasi kwamba akukute katika utiifu na yale yenye kukuweka karibu naye, na asikukute katika maasi na madhambi, ikiwa utafanya hivyo basi malipo yako yatakuwa ni Mwenyezi Mungu kukuhifadhi kutokana na kero za Dunia na Akhera, na atakunusuru katika mambo yako magumu mahala popote utakapoelekea. Na ukitaka kuomba jambo, basi usimuombe ila Mwenyezi Mungu kwani Yeye pekee ndiye mwenye kuwajibu waombaji. Na ukitaka msaada basi usiutake ila kwa Mwenyezi Mungu. Na uwe na yakini kuwa hutopata manufaa yoyote hata kama viumbe wote wa Ardhini watakusanyika ili kutaka kukunufaisha, isipokuwa kwa kile alichokiandika Mwenyezi Mungu kwako, na wala hutopata madhara hata kama viumbe wote wa Ardhini watakusanyika ili kutaka kukudhuru, isipokuwa kwa lile alilolikadiria Mwenyezi Mungu juu yako. Na kuwa jambo hili kashaliandika Mwenyezi Mungu Mtukufu na akalikadiria kulingana na namna hekima na elimu yake zilivyopelekea, na hakuna kubadilishwa yale aliyoyaandika Mwenyezi Mungu.

Mafunzo
  1. Umuhimu wa kuwafundisha vijana na watoto wadogo mambo ya dini kuanzia Tauhidi na adabu na mengineyo.
  2. Malipo huenda sawa na matendo.
  3. Amri ya kumtegemea Mwenyezi Mungu, na kutawakali kwake bila kumtegemea asiyekuwa yeye, na yeye ndiye msaidizi bora.
  4. Kuamini maamuzi na mipango ya Mwenyezi Mungu na kuridhika nayo, nakuwa Mwenyezi Mungu amekwisha kadiria kila kitu.
  5. Atakayetelekeza amri ya Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu naye humtelekeza na humnyima ulinzi.
Marejeo

سنن الترمذي (4/ 284) (2516). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية (ص42). شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص200). فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للعباد (ص69).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ametuhadithia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- naye ni mkweli mwenye kukubaliwa: "Kwa hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake kwenye tumbo la mama yake mchana arobaini na nyusiku arobaini

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ الصَّادِقُ المَصْدُوقُ: «أَنَّ خَلْقَ أَحَدِكُمْ يُجْمَعُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا وَأَرْبَعِينَ لَيْلَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَهُ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَهُ، ثُمَّ يُبْعَثُ إِلَيْهِ المَلَكُ، فَيُؤْذَنُ بِأَرْبَعِ كَلِمَاتٍ، فَيَكْتُبُ: رِزْقَهُ وَأَجَلَهُ وَعَمَلَهُ وَشَقِيٌّ أَمْ سَعِيدٌ، ثُمَّ يَنْفُخُ فِيهِ الرُّوحَ، فَإِنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الجَنَّةِ حَتَّى لاَ يَكُونُ بَيْنَهَا وَبَيْنَهُ إِلَّا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكِتَابُ، فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُ النَّارَ، وَإِنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهَا وَبَيْنَهُ إِلَّا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكِتَابُ، فَيَعْمَلُ عَمَلَ أَهْلِ الجَنَّةِ فَيَدْخُلُهَا».
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Ametuhadithia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- naye ni mkweli mwenye kukubaliwa: "Kwa hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake kwenye tumbo la mama yake mchana arobaini na nyusiku arobaini kisha anakuwa tone la manii kwa muda kama huo kisha anakuwa pande la damu kwa mfano wa siku hizo, kisha hutumwa Malaika na huamrishwa kufanya mambo manne; Hivyo basi ataandika riziki yake, na muda wa kufa kwake na matendo yake na ataandika kuwa ni muovu au ni mwema, kisha atampulizia roho, na kwa hakika mmoja wenu anaweza kufanya matendo ya watu wa Peponi kiasi ya kuwa haitobakia kati yake na kuingia Peponi isipokuwa usawa wa urefu wa mkono, basi kikamtangulia kitabu -Kadari- na akafanya matendo ya watu wa motoni na akaingia motoni, na kwa hakika mmoja wenu anaweza akafanya matendo miongoni mwa matendo ya watu wa motoni mpaka ikabakia kati yake na kuingia motoni kiasi cha usawa wa mkono kisha kikamtangulia kitabu -Kadari- akafanya mataendo ya watu wa peponi na akaingia peponi."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amesema Bin Masoud: Ametuhadithia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake naye ni mkweli kwenye maneno yake, na mwenye kukubaliwa, Mwenyezi Mungu Mtukufu amemkubali, Amesema: Kwa hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake, na jambo hilo ni kuwa mtu akimuingilia mke wake basi yale manii yake yaliyosambaa hukusanywa kwenye tumbo la mwanamke kwa muda wa siku arobaini yakiwa ni tone la manii, Kisha hubadilika na kuwa pande la damu nzito iliyoganda, haya hufanyika katika arobaini ya pili, Kisha hubadilika kuwa pande la nyama, nacho ni kipande cha nyama chenye ukubwa wa kuweza kutafunwa, na mabadiliko haya ni katika arobaini ya tatu, Kisha Mwenyezi Mungu hulitumia pande hilo la nyama Malaika, kisha hulipulizia ndani yake roho baada ya kuisha siku arobaini za tatu, Na huamrishwa Malaika aandike maneno manne, nayo ni: Riziki yake, nacho ni kiwango ambacho atakipata miongoni mwake ni neema katika umri wake, Na pia huandikwa wakati wake, nao ni muda wa kubakia kwake Duniani, Na matendo yake, yatakuwa ni yapi? Na je atakuwa muovu au mwema. Kisha akaapa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yawezekana mtu akafanya matendo miongoni mwa matendo ya watu wa peponi, na yakawa matendo yake ni mazuri, yaani kwenye muonekano wa watu, na akabakia hivyo mpaka inakuwa kati yake na Pepo ni kiasi cha mkono, yaani kiasi kilichobaki kati yake mpaka kuifikia pepo ni kidogo sana kama vile ambavyo mtu amebakiza nafasi kati yake na ardhi kiasi cha mkono, mara Kitabu kinamtangulia na kile alichopangiwa, na wakati huo anafanya matendo ya watu wa motoni na akaandikiwa kuwa huo ndio mwisho wake na akaingia motoni; Kwa sababu sharti la kukubaliwa matendo yake ni kudumu katika matendo hayo na wala asibadilishe, na watu wengine wapo wenye kufanya matendo ya watu wa motoni mpaka mtu anakaribia kuingia motoni, mpaka inakuwa kati yake na kuingia motoni ni kiasi cha urefu wa mkono, basi kikamtangulia kitabu na alichopangiwa hivyo akafanya matendo ya watu wa peponi na akaingia peponi.

Mafunzo
  1. Mwisho wa mambo yote huwa kwa namna ambavyo imekwishapangwa na kukadiriwa.
  2. Tahadhari ya kutodanganyika na muonekano wa matendo; Bali matendo huangaliwa mwisho wake.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 135) (7454)، (4/ 111) (3208)، صحيح مسلم (4/ 2036) (2643)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (15/ 130)، شرح الأربعين النووية للعثيمين (ص: 84).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Aliandika Mwenyezi Mungu makadirio ya viumbe kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ رضي الله عنهما قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «كَتَبَ اللهُ مَقَادِيرَ الْخَلَائِقِ قَبْلَ أَنْ يَخْلُقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِخَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ، قَالَ: وَعَرْشُهُ عَلَى الْمَاءِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Amrou Bin Aaswi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Aliandika Mwenyezi Mungu makadirio ya viumbe kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini, akasema: Na Arshi yake ilikuwa juu ya maji."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anatoa habari Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu aliandika mambo yote ambayo yatatokea miongoni mwa mambo ya kuwakadiria viumbe kwa uchanganuzi kuanzia kuishi na kufa na riziki na mambo mengineyo aliyaandika katika Lauhil Mah-fuudh kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini, na hayo aliyoyaandika hutokea kwa mujibu wa alivyopanga Hivyo basi kila kitu chenye kutokea, basi kinatokea kwa mipango ya Mwenyezi Mungu na kukadiria kwake. Basi jambo lolote linalompata mja lisingeweza kumkosa, na lenye kumkosa lisingeweza kumpata.

Mafunzo
  1. Ni wajibu kuamini hukumu na Kadari.
  2. Na Kadari: Ni ujuzi wa Mwenyezi Mungu wa kujua vitu vyote na kuviandika na kutaka kwake viwe na kuviumba.
  3. Kuamini kuwa mipango ya Mwenyezi Mungu (Kadari) ilikwisha andikwa kabla ya kuumbwa Mbingu na Ardhi kunaleta tija ya kuridhika na kujisalimisha na kukubali.
  4. Kwa hakika Arshi ya Mwenyezi Mungu ilikuwa juu ya maji kabla ya kuumbwa Mbingu na Ardhi.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2044) (2653)، إكمال المعلم (8/141)، البحر المحيط الثجاج (41/450).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila jambo linakuwa kwa namna lilivyopangwa, mpaka kushindwa kufanya jambo fulani au kulifanya kwa ufanisi, au kufanya kwa ufanisi au kushindwa kabisa kufanya

عَنْ طَاوُسٍ أَنَّهُ قَالَ: أَدْرَكْتُ نَاسًا مِنْ أَصْحَابِ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُونَ كُلُّ شَيْءٍ بِقَدَرٍ، قَالَ: وَسَمِعْتُ عَبْدَ اللهِ بْنَ عُمَرَ رضي الله عنهما يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «كُلُّ شَيْءٍ بِقَدَرٍ، حَتَّى الْعَجْزِ وَالْكَيْسِ، أَوِ الْكَيْسِ وَالْعَجْزِ».
Imepokelewa kutoka kwa Twaausi kuwa yeye amesema: Niliwakuta watu miongoni mwa maswahaba wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- wakisema kuwa kila kitu huwa kwa namna ilivyopangwa, akasema: Na nimemsikia Abdullah bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake- anasema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kila jambo linakuwa kwa namna lilivyopangwa, mpaka kushindwa kufanya jambo fulani au kulifanya kwa ufanisi, au kufanya kwa ufanisi au kushindwa kabisa kufanya."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila jambo linakuwa kwa mujibu wa lilivyopangwa; Mpaka kushindwa: Nako nikuacha jambo ambalo ni wajibu kulifanya au kulichelewesha katika mambo ya kidunia au ya Akhera. Na hata kufanya jambo kwa ufanisi: Nako ni kufanya kwa uchangamfu na weledi katika mambo ya kidunia au ya Akhera. Na hakika Mwenyezi Mungu amepangilia jambo la kushindwa au kufanya kwa ufanisi na amepangilia kila kitu, hakuna chochote kinachotokea isipokuwa kinatokea kwa ujuzi wake Mwenyezi Mungu na kutaka kwake.

Mafunzo
  1. Imewekwa wazi itikadi ya Maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- katika kuamini mipango ya Mwenyezi Mungu -Kadari-.
  2. Kila kitu kinatokea kwa mipango ya Mwenyezi Mungu mpaka kushindwa na kuweza kufanya jambo.
  3. Uimara wa Maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- katika kupokea na kufikisha maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake.
  4. Kuamini -Kadari- kheri zake na shari zake.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2045) (2655)، إكمال المعلم (8/143)، شرح النووي على مسلم (16/205)، الفتح الرباني لترتيب مسند الإمام أحمد بن حنبل الشيباني (1/ 122).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com