Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Aliandika Mwenyezi Mungu makadirio ya viumbe kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ رضي الله عنهما قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «كَتَبَ اللهُ مَقَادِيرَ الْخَلَائِقِ قَبْلَ أَنْ يَخْلُقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِخَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ، قَالَ: وَعَرْشُهُ عَلَى الْمَاءِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Amrou Bin Aaswi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Aliandika Mwenyezi Mungu makadirio ya viumbe kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini, akasema: Na Arshi yake ilikuwa juu ya maji."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anatoa habari Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu aliandika mambo yote ambayo yatatokea miongoni mwa mambo ya kuwakadiria viumbe kwa uchanganuzi kuanzia kuishi na kufa na riziki na mambo mengineyo aliyaandika katika Lauhil Mah-fuudh kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini, na hayo aliyoyaandika hutokea kwa mujibu wa alivyopanga Hivyo basi kila kitu chenye kutokea, basi kinatokea kwa mipango ya Mwenyezi Mungu na kukadiria kwake. Basi jambo lolote linalompata mja lisingeweza kumkosa, na lenye kumkosa lisingeweza kumpata.

Mafunzo
  1. Ni wajibu kuamini hukumu na Kadari.
  2. Na Kadari: Ni ujuzi wa Mwenyezi Mungu wa kujua vitu vyote na kuviandika na kutaka kwake viwe na kuviumba.
  3. Kuamini kuwa mipango ya Mwenyezi Mungu (Kadari) ilikwisha andikwa kabla ya kuumbwa Mbingu na Ardhi kunaleta tija ya kuridhika na kujisalimisha na kukubali.
  4. Kwa hakika Arshi ya Mwenyezi Mungu ilikuwa juu ya maji kabla ya kuumbwa Mbingu na Ardhi.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2044) (2653)، إكمال المعلم (8/141)، البحر المحيط الثجاج (41/450).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Ngazi za hukumu na Mipango

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com