Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Mambo yanayohusu Hukumu na Mipango.

Hadithi 3

Mwenye kutakiwa kheri na Allah, (Allah) humuonja kutokana na kheri hiyo

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «مَنْ يُرِدِ اللهُ بِهِ خَيْرًا يُصِبْ مِنْهُ».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwenye kutakiwa kheri na Allah, (Allah) humuonja kutokana na kheri hiyo.
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehama na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu akitaka kheri kwa yeyote katika waja wake waumini huwapa mtihani katika nafsi zao na mali zao, na familia zao, kwa kile kinachotokea kwa muumini ikiwemo kurejea kwa Allah Mtukufu kwa maombi na dua, na kufutiwa makosa, na kunyanyuliwa daraja.

Mafunzo
  1. Nikuwa muumini anakabiliwa na mabalaa mbali mbali.
  2. Mtihani unaweza kuwa alama ya mapenzi ya Allah kwa mja wake, ili amnyanyue daraja yake, na ampandishe cheo chake, na amfutie madhambi yake.
  3. Himizo la kuwa na subira wakati wa matatizo na kutolalama.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 115) (5645). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 509). بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (1/ 98). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص45). نزهة المتقين، مجموعة من المشايخ (1/ 71). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 244). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (3/ 1127).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alijitenga mbali na mpiga mayowe, na mnyoa nywele, na mchana nguo

عَن أَبِي بُرْدَةَ بْنِ أَبِي مُوسَى رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: وَجِعَ أَبُو مُوسَى وَجَعًا شَدِيدًا، فَغُشِيَ عَلَيْهِ وَرَأْسُهُ فِي حَجْرِ امْرَأَةٍ مِنْ أَهْلِهِ، فَلَمْ يَسْتَطِعْ أَنْ يَرُدَّ عَلَيْهَا شَيْئًا، فَلَمَّا أَفَاقَ، قَالَ: أَنَا بَرِيءٌ مِمَّنْ بَرِئَ مِنْهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَرِئَ مِنَ الصَّالِقَةِ وَالحَالِقَةِ وَالشَّاقَّةِ.
Kutoka kwa Abuu Burda bin Abii Mussa radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Aliumia Abuu Mussa maumivu makali, akazimia na kichwa chake kikiwa katika paja la mwanamke katika wake zake, akawa hakuweza kumjibu chochote, alipozinduka, akasema: Mimi najitenga mbali na yule aliyejitenga mbali naye Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alijitenga mbali na mpiga mayowe, na mnyoa nywele, na mchana nguo.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amesimulia Abuu Burda radhi za Allah ziwe juu yake kuwa baba yake Abuu Mussa Al-Ash'ary radhi za Allah ziwe juu yake aliugua maradhi makali, akazimia, na kichwa chake kilikuwa katika paja la mwanamke mmoja katika wake zake, akapiga mayowe yule mwanamke kwa kumuita, akawa hakuweza kumjibu chochote kwa sababu ya kuzimia kwake. Alipozinduka akasema kuwa: Hakika yeye anajitenga mbali na yule aliyejitenga mbali naye Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na hakika yeye rehema na amani ziwe juu yake alijitenga naye. Mpiga mayowe: Naye ni mwanamke anayenyanyua sauti yake wakati wa msiba. Na mnyoaji: Ni mwanamke anayenyoa nywele zake wakati wa msiba. Na mchana nguo: Ni mwanamke anayechana nguo zake wakati wa msiba. Kwa sababu haya ni katika mambo ya zama za ujinga, bali aliamrisha kuwa na subira wakati wa msiba, na kutaraji malipo yake kwa Mwenyezi Mungu.

Mafunzo
  1. Katazo la kuchana nguo, na kunyoa nywele, na kunyanyua sauti wakati wa kutokea misiba, nakuwa hilo ni katika madhambi makubwa.
  2. Huzuni na kulia pasina maombolezo na kunyanyua sauti si haramu, hili halipingani na subira juu ya maamuzi ya Mwenyezi Mungu, bali ni rehema.
  3. Uharamu wa kulalamika katika makadirio ya Mwenyezi Mungu yenye kuumiza kwa kauli au vitendo.
  4. Uwajibu wa kuwa na subira wakati wa misiba.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 81) (1296). صحيح مسلم (1/ 100) (104). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص287). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (2/ 371).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu kuliko muumini dhaifu, na katika kila kheri,

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الْمُؤْمِنُ الْقَوِيُّ، خَيْرٌ وَأَحَبُّ إِلَى اللهِ مِنَ الْمُؤْمِنِ الضَّعِيفِ، وَفِي كُلٍّ خَيْرٌ، احْرِصْ عَلَى مَا يَنْفَعُكَ، وَاسْتَعِنْ بِاللهِ وَلَا تَعْجَزْ، وَإِنْ أَصَابَكَ شَيْءٌ، فَلَا تَقُلْ لَوْ أَنِّي فَعَلْتُ كَانَ كَذَا وَكَذَا، وَلَكِنْ قُلْ قَدَرُ اللهِ وَمَا شَاءَ فَعَلَ، فَإِنَّ (لَوْ) تَفْتَحُ عَمَلَ الشَّيْطَانِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu kuliko muumini dhaifu, na katika kila kheri, Pupia yenye manufaa na wewe, na utake msaada kwa Allah na wala usishindwe, na likikusibu jambo usiseme: Lau ningelifanya kadha basi ingelikuwa kadhaa wa kadhaa, lakini sema: Hili ni kwa makadirio ya Allah naye hufanya alitakalo, maana neno "Lau" hufungua matendo ya shetani".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muumini ni mtu wa kheri maisha yake yote, lakini muumini mwenye nguvu katika imani yake na maamuzi yake na mali yake na mengineyo yenye kuendana na nguvu huyu ni bora zaidi na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko muumini dhaifu. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuusia muumini kuchukuwa sababu katika yale yenye kumnufaisha katika mambo ya Dunia na Akhera, ikiwa ni pamoja kuegemea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kutaka msaada kwake, na kutegemea kwake. Kisha akakataza rehema na amani ziwe juu yake kuhusu kushindwa, na uvivu, na uzembe wa mtu kufanya yale yenye manufaa Duniani na Akhera. Muumini akijitahidi katika matendo, na akachukua sababu, huku akitaka msaada kwa Mwenyezi Mungu, na kwa kutaka kheri kutoka kwa Mwenyezi Mungu, basi hapo hana la kufanya zaidi ya kukabidhi jambo lake lote kwa Mwenyezi Mungu, na ajue kuwa uchaguzi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndio wenye kheri, ukimpata msiba baada ya hapo, basi asiseme: "Laiti ningelifanya kadha wa kadha"; "Kwani neno "Lau" Hufungua kazi ya Shetani" kuanzia kupingana na mipango ya Allah, na kuhuzunika kwa yale aliyoyakosa, bali anatakiwa aseme tena kwa kujisalimisha na kuridhika: "Ni mipango ya Mwenyezi Mungu na alitakalo hufanya", kilichotokea ni kwa mujibu wa yale aliyoyataka Mwenyezi Mungu, kwani yeye ni mfanyaji asiye na mipaka wa yale ayatakayo, na hakuna awezaye kuzuia maamuzi yake, na hakuna awezaye kuhukumu baada ya hukumu yake.

Mafunzo
  1. Kutofauti watu katika swala la imani.
  2. Inapendeza kuwa na nguvu katika matendo; kwani hupatikana faida kwa matendo hayo ambayo haipatikani kukiwa na udhaifu.
  3. Mwanadamu anatakiwa apupie katika yale yenye kumnufaisha, na aache yasiyomnufaisha.
  4. Ni wajibu kwa muumini atake msaada wa Mwenyezi Mungu kwake katika mambo yake yote, na wala asiitegemee nafsi yake.
  5. Kuthibiti uwepo wa mipango na maamuzi ya Mwenyezi Mungu (kadhaa na kadari), nakuwa hilo halipingani na swala la mtu kufanya sababu na kwenda kutafuta mambo mazuri na ya kheri.
  6. Katazo la kusema: "Lau" kwa njia ya kulalamika wakati wa kupatwa na mitihani, na uharamu wa kupingana na maamuzi na mipango ya Allah Mtukufu.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2052) (2664). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، لعبد الله البسام (7/ 492). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 338). فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 430).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com