Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alimsimulia akasema: Alinijia mwanamke mmoja akiwa na watoto wake wawili akiniomba, nikawa sikupata ndani kwangu zaidi ya tende moja, nikampatia, akaigawanya baina ya watoto wake, kisha akanyanyuka akatoka, muda si mrefu, akaingia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akamsimulia kisa hicho, akasema: "Atakayesimamia chochote kwa watoto wa kike hawa, akawatendea wema, basi watakuwa ni kinga kwake kutokana na moto".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake, ya kwamba mwanamke mmoja alimjia akiwa na mabinti zake wawili akimuomba chochote kinacholiwa, Aisha akawa hakupata kwake zaidi ya tende moja, akampatia basi mwanamke yule akaigawanya tende hiyo baina ya watoto wake, na yeye hakula chochote, kisha akanyanyuka na akaondoka, punde akaingia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, Aisha akamsimulia kisa hicho, akasema: Atakayesimamia chochote katika malezi ya mabinti hawa, akawatendea wema na akawalisha na akawanywesha na akawavisha, na akawa na subira juu ya hilo, basi watakuwa ni sitara na kinga kwake dhidi ya moto.
Mafunzo
Kuwalea watoto wa kike na kushughulika nao ni katika amali bora miogoni mwa amali njema zinazomuepusha mtu na moto.
Sunna ya kutoa chochote kilicho ndani ya uwezo wa mtu hata kama ni kidogo.
Huruma kubwa ya wazazi kwa watoto wao.
Kumebainishwa hali ya nyumba za Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kwamba riziki yake ilikuwa ya kumtosheleza pekee.
Kumebainishwa fadhila za kujinyima kwa ajili ya watu wengine, na kwamba hilo ni katika alama za waumini; kwani Aisha alimpendelea yule mwanamke na watoto wake kuliko nafsi yake, na hii inaonyesha juu ya ukarimu wake na moyo wake wa kujitolea pamoja na kuwa ana uvihitaji.
Zawadi ya watoto wa kike imeitwa kuwa ni mtihani; kwa sababu kuwalea kwake kuna shida na tabu nyingi, au kwa sababu ya baadhi ya watu kuwachukia, au ni kwa sababu mara nyingi wao huwa hawana vyanzo vya mapato ya maisha.
Uislamu ulikuja kung'oa mizizi ya desturi mbovu za zama za ujinga, na miongoni mwake nikuwa uliusia watu kuwalea vizuri watoto wa kike.
Mtu anapata malipo haya hata akiwa na binti mmoja kama ilivyokuja katika baadhi ya riwaya.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 7) (5995).
صحيح مسلم (4/ 2027) (2629).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 353).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص199).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (5/ 151).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 106).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 277).
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna siku ambayo wanaamka ndani yake waja isipokuwa kuna Malaika wawili wanateremka, anasema mmoja wao: Ewe Mwenyezi Mungu mpe mtoaji badala, na anasema mwingine: Ewe Mwenyezi Mungu mpe mzuiaji (Bahili) hasara".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa katika kila siku inayochomozewa na Jua ndani yake kuna Malaika wawili wanateremka na kunadi, anasema mmoja wao:
Ewe Mwenyezi Mungu mpe mwenye kutoa katika njia za utiifu na kwa familia na kwa wageni na sadaka za hiyari mrejeshee na mpe badala bora kuliko kile alichotoa, na umbariki.
Na anasema mwingine: Ewe Mwenyezi Mungu mpe bahili mzuiaji uharibifu katika mali yake na uiteketeze mali yake anayoizuia na kutompa mwenye kustahiki.
Mafunzo
Inafaa kumuombea dua nzuri mkarimu kuzidishiwa badala, na kurejeshewa kheri zaidi ya ile aliyotoa, na inafaa kumuombea dua mbaya bahili kwa kuharibika mali yake ambayo anaifanyia ubahili na anaizuia kuitoa katika yale aliyowajibishiwa na Mwenyezi Mungu juu yake.
Dua ya Malaika kuwaombea waumini wema wenye kutoa, kuwaombea kheri na baraka, nakuwa dua zao hujibiwa.
Himizo la kutoa katika yale ya wajibu na ya hiyari; kama kutoa matumizi kwa familia, na kuunga udugu, na milango mbali mbali ya kheri.
Kumebainishwa fadhila za mtoaji katika njia za kheri, nakuwa mwisho wake nikuwa Mwenyezi Mungu humrejeshea badala, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na wala hamtatoa chochote ila yeye atakirejesha, naye ni mbora wa wanaoruzuku" [Sabai:39].
Dua hii mbaya ni kwa mtu bahili katika matumizi ya wajibu, ama matumizi ya hiyari dua haingii hapo; kwa sababu mwenye mali hapa hastahiki dua hii.
Uharamu wa ubahili na tamaa.
Marejeo
صحيح البخاري (2/ 115) (1442).
صحيح مسلم (2/ 700) (1010).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 157).
نزهة المتقين بشرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 293).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 376).
Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake-: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema huku akiwa juu ya Mimbari, na akataja sadaka, na kujizuia kuomba, na kuombaomba: "Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini, mkono wa juu: Ni ule unaotoa, na mkono wa chini: Ni ule unaoomba".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitaja sadaka, na kujizuia kuombaomba, aliyasema hayo wakati akihutubia katika Mimbari; kisha akasema: Mkono wa juu wenye kutoa sadaka ni bora na unapendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko mkono wa chini wenye kuomba.
Mafunzo
Hapa kuna fadhila za ukarimu na utoaji katika njia za kheri, na ubaya wa kuombaomba.
Hapa kuna himizo la kujizuia kuomba, na kuwaepuka watu, na himizo la kufanya mambo matukufu, na kuacha yenye udhalili, na Mwenyezi Mungu anapenda mambo ya juu zaidi.
Mikono ina aina nne katika ubora, kama ifuatavyo: Wa juu zaidi ni ule unaotoa, kisha unaojizuia kuchukua, kisha unaopokea pasina kuomba, kisha unafuata wa chini kuliko hiyo, ule unaoomba.
Marejeo
صحيح البخاري (2/ 112) (1429).
صحيح مسلم (2/ 717) (1033).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 590).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 465).
التوضيح لشرح الجامع الصحيح، لابن الملقن (10/ 315).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 388).
تحفة الأحوذي بشرح جامع الترمذي، المباركفوري (3/ 288).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص212).
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Dharri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba watu miongoni mwa Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake walisema kumwambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wamechukua malipo mengi wenye utajiri: Wanaswali kama tunavyoswali na wanafunga kama tunavyofunga, na wanatoa sadaka katika mali yao ya akiba. Akasema: Hivi kwani hajakuwekeeni Mwenyezi Mungu mambo mnayoweza kutoa sadaka: Hakika katika kila tasbihi (kauli ya sub-haanallaah) ni sadaka, na kila takbira (Allahu Akbaru) ni sadaka, na kila tahmidi (Alhamdulillah) ni sadaka, na kila tahalili (Laa ilaaha illallaahu) ni sadaka, na kuamrisha mema ni sadaka, na kukataza maovu ni sadaka, na katika kiungo cha siri cha mmoja wenu kuna sadaka" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi yawezekanaje akidhi mmoja wetu matamanio yake kisha awe na malipo? Akasema: Mnasemaje ikiwa atakiweka katika haramu, je atakuwa na mzigo wa dhambi? basi ndivyo hivyo akikiweka katika halali atakuwa na malipo".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Walilalamikia baadhi ya mafukara wa kiswahaba hali ya umasikini wao kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kutotoa kwao sadaka kwa mali ili wapate malipo mengi kama walivyoyapata ndugu zao wenye mali nyingi na ili na wao wafanye kheri kama wao; kiasi ambacho wao wanaswali kama tunavyoswali, na wanafunga kama tunavyofunga, na wanatoa sadaka kwa mali yao ya ziada na sisi hatutoi! Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawaelekeza katika yale wanayoyaweza katika sadaka, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kwani hakukujaalieni Mwenyezi Mungu vile mnavyoweza kuvitoa sadaka kwa ajili nafsi zenu?! Kwani kauli yenu: "Sub-haanallaah" Inakuwa kwenu na malipo ya sadaka, na vile vile kauli: "Allaahu Akbar" ni sadaka, na kauli: "Alhamdulillaah" ni sadaka, na kauli: Laa ilaaha illa llaah" ni sadaka, na kuamrisha mema" ni sadaka, na "kukataza maovu" ni sadaka, bali hata katika tendo la ndoa la mmoja wenu kwa mke wake ni sadaka. Wakashangaa, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi akidhi mmoja wenu matamanio yake na awe na malipo katika hilo?! Akasema: Hivi mwaonaje kama akiweka katika haramu kama zinaa au kinginecho, je, atakuwa na madhambi? Hivyo hivyo akiweka katika halali anakuwa na malipo.
Mafunzo
Kushindana kwa Maswahaba katika kufanya kheri, na pupa yao ya kupata malipo na fadhila kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Kukithiri kwa njia za amali za kheri, nakuwa zinakusanya kila amali anayoifanya muislamu kwa nia njema na lengo zuri.
Urahisi wa Uislamu na wepesi wake, kila muislamu anapata anayoweza kuyafanya ili amtii Mwenyezi Mungu kwayo.
Amesema Nawawi: Na katika hili kuna dalili yakuwa mambo ya halali yanaweza kuwa ibada kwa nia ya kweli, tendo la ndoa linakuwa ibada atakaponuia kukidhi haki ya mke na kushiriki naye kwa wema ambao ameamrishwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, au kutafuta mtoto mwema, na kuilinda nafsi yake na nafsi ya mke wake na kujizuia wote wawili na kutazama haramu, au kuifikiria, au kutamani kufanya, au mengineyo katika malengo mazuri.
Amepiga mfano na kupima kwa akili; ili jambo liwe wazi na liingie vizuri ndani ya nafsi ya msikilizaji.
Marejeo
صحيح مسلم (2/ 697) (1006).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 201).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 161).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (3/ 31).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 150).
عن أبي هريرة رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «مَا نَقَصَتْ صَدَقَةٌ مِنْ مَالٍ، وَمَا زَادَ اللهُ عَبْدًا بِعَفْوٍ إِلَّا عِزًّا، وَمَا تَوَاضَعَ أَحَدٌ لِلهِ إِلَّا رَفَعَهُ اللهُ».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Sadaka haikuwahi kupunguza chochote katika mali, na hakuna jambo zuri zaidi analomzidishia Mwenyezi Mungu mja kwa kusamehe zaidi kama kupewa utukufu, na hakuwahi kunyenyekea yeyote kwa ajili Mwenyezi Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu humnyanyua".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa sadaka haipunguzi mali, bali inaikinga na maafa, na Mwenyezi Mungu humpa badala mwenye nayo ya kheri kubwa, inakuwa ni ziada na sio kupungua.
Na kusamehe kunapokuwa na uwezo wa kulipiza kisasi hakukuwahi kuzidisha kwa mwenye kusamehe isipokuwa nguvu na utukufu.
Na hakuwahi kunyenyekea na kujidhalilisha yeyote kwa kutaka radhi za Allah, si kwa kumuogopa yeyote, na si kwa kujipendekeza kwa yeyote, na wala si kwa kutaka manufaa kwake, isipokuwa mtu huyu malipo yake yatakuwa ni kunyanyuliwa na kupewa utukufu.
Mafunzo
Kheri na kufaulu vinapatikana kwa kutekeleza sheria na kufanya mambo ya kheri hata kama baadhi ya watu watadhania kinyume na hivyo.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2001) (2588).
توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 501).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 354).
فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 438).
سبل السلام بشرح بلوغ المرام، للصنعاني (2/ 692).
عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «قَالَ اللهُ: أَنْفِقْ يَا ابْنَ آدَمَ أُنْفِقْ عَلَيْكَ».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Toa ewe mwanadamu na mimi nikupe".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Toa ewe mwanadamu -katika matumizi ya wajibu na ya hiyari- nikukunjulie na nikupe badala ya hicho na nikubariki ndani yake.
Mafunzo
Himizo la kutoa sadaka na kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu.
Kutoa katika njia za heri ni miongoni mwa sababu kubwa za kupata baraka katika riziki na kuzidishwa kwake, na Mwenyezi Mungu kumpa badala mja katika kile alichokitoa.
Hadithi hii ni katika zile anazozipokea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutoka kwa Mola wake Mlezi, na huitwa Hadithil Qudsi au Hadithil Ilahi, nayo ni ile ambayo tamko lake na maana yake inatoka kwa Allah, isipokuwa haina upekee kama wa Qur'ani inaojipambanua nayo kwa vingine, ikiwa kisomo chake kutumika katika ibada, na kuwa twahara kabla ya kusoma, na kuwashinda watu kwa changamoto zake, na mengineyo.
Marejeo
صحيح البخاري (7/ 62) (5352).
صحيح مسلم (2/ 690) (993).
شرح النووي على مسلم (7/ 79).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 603).
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Dinari moja unayoitoa kwenye njia ya Allah, na dinari moja unayoitoa kwa mtumwa, na dinari moja unayoitoa sadaka kwa masikini, na dinari moja unayoitoa kwa familia yako, yenye malipo makubwa kuliko yote ni ile unayoitoa kwa familia yako".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ametaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya aina za utoaji, akasema: Dinari uliyoitoa katika Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na dinari uliyoitoa katika shingo ya mtumwa, na dinari uliyoitoa sadaka kwa masikini mwenye uhitaji, na dinari uliyoitoa kwa watu wako na familia yako, kisha akaeleza kuwa yenye malipo makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu ni ile uliyoitoa kwa watu wako na familia na wale wanaokulazimu kuwahudumia.
Mafunzo
Wingi wa milango ya kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu.
Kutanguliza kilicho bora katika mlango wa kutoa panapokuwa na msongamano wa mambo, na miongoni mwake ni kutoa kwa familia uwezo unapokosekana wa kuyatekeleza yote.
Amesema Nawawi katika kitabu cha Sharhe Muslim: Himizo la kutoa matumizi kwa familia, na kumebainishwa ukubwa wa thawabu ndani yake; kwa sababu wako miongoni mwao wanaomlazimu kuwahudumia kwa sababu ya ukaribu wa udugu, na yuko miongoni mwao inakuwa ni sunna na inakuwa ni sadaka na kuunga udugu, na yuko ambaye inakuwa wajibu kwa kummiliki kwa sababu ya ndoa au umiliki wa kuume (kama mateka na vijakazi), na hii yote ni fadhila iliyohimizwa, nayo ni bora kuliko sadaka ya hiyari.
Amesema As-Sanadi: Kauli yake "Dinari anayoitoa kwa familia yake", Yaani: Atakaponuia kupata radhi za Allah na akakusudia kutoa katika familia kwa mfano haki.
Amesema Abuu Qilaba: Na ni mtu gani mwenye malipo makubwa kuliko mtu anayetoa matumizi kwa familia ndogo anayowasitiri au Mwenyezi Mungu anawanufaisha kwayo na kuwatosheleza?!
Marejeo
صحيح مسلم (2/ 692) (995).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 156).
نزهة المتقين بشرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 291).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 374).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص209).
Kutoka kwa Ka'bu bin Hatim -radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakuna yeyote miongoni mwenu, isipokuwa ataongeleshwa na Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama bila ya kuwapo na mkalimani yeyote kati yake na Yeye (Allah). Atatazama kuliani kwake, na wala hataona kitu chochote isipokuwa matendo yake aliyotanguliza. Kisha ataangalia kushotoni kwake, na wala hataona kitu chochote isipokuwa matendo yake aliyotanguliza. Na ataangalia mbele yake, na hataona isipokuwa Moto mbele ya uso wake. Basi uepukeni Moto hata kama ni kwa nusu ya tende."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Alieleza Mtume rehema amani ziwe juu yake kuwa kila Muumini atasimama mbele ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama peke yake, na kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atazungumza naye bila ya muwakilishi, na hakuna mkalimani baina yao wa kutafsiri maneno, hivyo atatazama kulia na kushoto kutokana na hofu kali, labda atapata njia ya kwenda ili aweze kuokolewa na moto uliombele yake. Akitazama upande ulioko kuliani kwake hatoona isipokuwa yale aliyoyatanguliza katika matendo mema, na akitazama kushotoni kwake hatoona isipokuwa yale aliyoyatanguliza katika matendo mabaya, na akitazama mbele yake hatoona isipokuwa moto, na hatoweza kuukwepa, kwani hakuna budi ni lazima apite juu daraja (Swirat). Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Wekeni kinga kati yenu na moto, kama kutoa sadaka na matendo mema, walau kwa kitu kidogo kama nusu ya tende.
Mafunzo
Himizo la kutoa sadaka hata kama itakuwa ndogo, na kujipamba na mambo mazuri, na kuamiliana kwa upole na maneno laini.
Ukaribu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake siku ya Kiyama, kiasi kwamba hapatokuwa na kizuizi kati yao, wala muwakilishi wala mkalimani, basi muumini achukue tahadhari asijekwenda kinyume na amri za Mola wake Mlezi.
Ni lazima kwa mtu asidharau anachokitoa sadaka, hata kama ni kidogo, kwani ni kinga ya kutoingia motoni.
Marejeo
صحيح البخاري (9/ 148) (7512).
صحيح مسلم (2/ 703) (1016).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين.
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (1/ 476).
نزهة المتقين، مجموعة من الباحثين (1/ 370).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 201).
بهجة قلوب الأبرار، عبد الرحمن آل سعدي (ص181).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com