Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Sadaka haikuwahi kupunguza chochote katika mali, na hakuna jambo zuri zaidi analomzidishia Mwenyezi Mungu mja kwa kusamehe zaidi kama kupewa utukufu, na hakuwahi kunyenyekea yeyote kwa ajili Mwenyezi Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu humnyanyua

عن أبي هريرة رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «مَا نَقَصَتْ صَدَقَةٌ مِنْ مَالٍ، وَمَا زَادَ اللهُ عَبْدًا بِعَفْوٍ إِلَّا عِزًّا، وَمَا تَوَاضَعَ أَحَدٌ لِلهِ إِلَّا رَفَعَهُ اللهُ».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Sadaka haikuwahi kupunguza chochote katika mali, na hakuna jambo zuri zaidi analomzidishia Mwenyezi Mungu mja kwa kusamehe zaidi kama kupewa utukufu, na hakuwahi kunyenyekea yeyote kwa ajili Mwenyezi Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu humnyanyua".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa sadaka haipunguzi mali, bali inaikinga na maafa, na Mwenyezi Mungu humpa badala mwenye nayo ya kheri kubwa, inakuwa ni ziada na sio kupungua. Na kusamehe kunapokuwa na uwezo wa kulipiza kisasi hakukuwahi kuzidisha kwa mwenye kusamehe isipokuwa nguvu na utukufu. Na hakuwahi kunyenyekea na kujidhalilisha yeyote kwa kutaka radhi za Allah, si kwa kumuogopa yeyote, na si kwa kujipendekeza kwa yeyote, na wala si kwa kutaka manufaa kwake, isipokuwa mtu huyu malipo yake yatakuwa ni kunyanyuliwa na kupewa utukufu.

Mafunzo
  1. Kheri na kufaulu vinapatikana kwa kutekeleza sheria na kufanya mambo ya kheri hata kama baadhi ya watu watadhania kinyume na hivyo.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2001) (2588). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 501). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 354). فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 438). سبل السلام بشرح بلوغ المرام، للصنعاني (2/ 692).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Sadaka za kujitolea.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com