Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitaja sadaka, na kujizuia kuombaomba, aliyasema hayo wakati akihutubia katika Mimbari; kisha akasema: Mkono wa juu wenye kutoa sadaka ni bora na unapendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko mkono wa chini wenye kuomba.
- Hapa kuna fadhila za ukarimu na utoaji katika njia za kheri, na ubaya wa kuombaomba.
- Hapa kuna himizo la kujizuia kuomba, na kuwaepuka watu, na himizo la kufanya mambo matukufu, na kuacha yenye udhalili, na Mwenyezi Mungu anapenda mambo ya juu zaidi.
- Mikono ina aina nne katika ubora, kama ifuatavyo: Wa juu zaidi ni ule unaotoa, kisha unaojizuia kuchukua, kisha unaopokea pasina kuomba, kisha unafuata wa chini kuliko hiyo, ule unaoomba.
صحيح البخاري (2/ 112) (1429). صحيح مسلم (2/ 717) (1033). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 590). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 465). التوضيح لشرح الجامع الصحيح، لابن الملقن (10/ 315). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 388). تحفة الأحوذي بشرح جامع الترمذي، المباركفوري (3/ 288). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص212).