عن عبد الله بن عُمر وأبي هريرة رضي الله عنهما أنهما سمعا رسول الله صلى الله عليه وسلم، يقول على أعواد منبره: «لَيَنْتَهِيَنَّ أَقْوَامٌ عَنْ وَدْعِهِمُ الْجُمُعَاتِ أَوْ لَيَخْتِمَنَّ اللهُ عَلَى قُلُوبِهِمْ، ثُمَّ لَيَكُونُنَّ مِنَ الْغَافِلِينَ».
Kutoka kwa Abdallah bin Omari na Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yao, ya kwamba wao walimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akisema akiwa juu ya Mimbari yake: "Kwa hakika ima wakome watu kuziacha swala za Ijumaa, au Mwenyezi Mungu atawapiga mihuri juu ya mioyo yao, kisha kwa hakika watakuwa ni miongoni mwa walioghafilika".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Amemtahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa juu ya Mimbari yake, mwenye kuacha swala ya Ijumaa na kutohudhuria bila udhuru, kwa uvivu na uzembe, au vinginevyo Mwenyezi Mungu atapiga muhuri juu ya nyoyo zao na kuzifunika na kuziwekea kizuizi kitakachozizuia kufuata haki, kisha wawe miongoni mwa walioghafilika kuzikumbuka sababu za kheri, na kinachokataa kheri ni nafsi zao wao wenyewe.
Mafunzo
Mkazo katika kuacha swala za Ijumaa, na kwamba hilo ni katika madhambi makubwa.
Amesema Nawawi: Hapa ni kwamba Ijumaa ni faradhi kwa kila mmoja.
Sheria ya kuweka Mimbari kwa ajili ya hotuba.
Amesema Assanadi: Maana yake ni kwamba moja kati ya mambo ni lazima litokee hakuna namna, ima kukoma kuacha swala za Ijumaa, au Mwenyezi Mungu kupiga muhuri juu ya mioyo yao, kwani kuzoea kuacha Ijumaa hujaza mfuniko juu ya moyo, na kuiweka mbali nafsi na mambo ya ibada.
Ni wajibu kwa mtoa mawaidha na mkumbushaji kuficha majina ya watu anaotaka kuwazungumzia katika mawaidha; kwa sababu hilo huleta msukumo zaidi wa kukubali nasaha, na kuzitekeleza amri.
Marejeo
صحيح مسلم (2/ 591) (865).
النهاية في غريب الحديث والأثر (964).
البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (17/ 250).
Kutoka kwa Abul Ja'di Adh-dhwamri radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa na uswahaba, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema: "Atakayeacha Ijumaa tatu kwa kuzipuuzia; Mwenyezi Mungu hupiga muhuri katika moyo wake"
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoacha swala ya Ijumaa, na kwamba mwenye kuacha swala ya Ijumaa mara tatu kwa kupuuza na uzembe pasina udhuru basi Mwenyezi Mungu atapiga na kufunika juu ya moyo wake na kizibo kinachozuia kuingia kheri yoyote ndani ya nafsi yake.
Mafunzo
Ameeleza bin Mundhiri kuwa kuna makubaliano ya wanachuoni wote kuwa swala ya Ijumaa ni faradhi ya lazima kwa kila mtu.
Ahadi mbaya kwa atakayeacha swala ya Ijumaa kwa kupuuza, kwamba Mwenyezi Mungu atapiga muhuri juu ya moyo wake.
Atakayeacha swala ya Ijumaa kwa dharura huyu haingii katika ahadi hii mbaya.
Amesema Shaukani: Kauli yake: (Ijumaa tatu), inategemea maana mbili, kuacha kwa ujumla sawa sawa zimefuatana Ijumaa hizo au zimetofautiana, hata akiacha katika kila mwaka Ijumaa moja basi Mwenyezi Mungu angepiga muhuri juu ya moyo wake baada ya Ijumaa ya tatu, na ndivyo hadithi inavyoonyesha, na maana ya pili nikuwa inakusudiwa Ijumaa tatu mfululizo.
Marejeo
سنن أبي داود (2/ 284) (1052).
سنن الترمذي (1/ 630) (500).
سنن النسائي (3/ 88) (1369).
سنن ابن ماجه (2/ 213) (1125).
مسند أحمد (24/ 255) (15498).
النهاية في غريب الحديث والأثر (557).
شرح سنن أبي داود للعباد (134/ 3).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com