Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kwa hakika ima wakome watu kuziacha swala za Ijumaa, au Mwenyezi Mungu atawapiga mihuri juu ya mioyo yao, kisha kwa hakika watakuwa ni miongoni mwa walioghafilika

عن عبد الله بن عُمر وأبي هريرة رضي الله عنهما أنهما سمعا رسول الله صلى الله عليه وسلم، يقول على أعواد منبره: «لَيَنْتَهِيَنَّ أَقْوَامٌ عَنْ وَدْعِهِمُ الْجُمُعَاتِ أَوْ لَيَخْتِمَنَّ اللهُ عَلَى قُلُوبِهِمْ، ثُمَّ لَيَكُونُنَّ مِنَ الْغَافِلِينَ».
Kutoka kwa Abdallah bin Omari na Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yao, ya kwamba wao walimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akisema akiwa juu ya Mimbari yake: "Kwa hakika ima wakome watu kuziacha swala za Ijumaa, au Mwenyezi Mungu atawapiga mihuri juu ya mioyo yao, kisha kwa hakika watakuwa ni miongoni mwa walioghafilika".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Amemtahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa juu ya Mimbari yake, mwenye kuacha swala ya Ijumaa na kutohudhuria bila udhuru, kwa uvivu na uzembe, au vinginevyo Mwenyezi Mungu atapiga muhuri juu ya nyoyo zao na kuzifunika na kuziwekea kizuizi kitakachozizuia kufuata haki, kisha wawe miongoni mwa walioghafilika kuzikumbuka sababu za kheri, na kinachokataa kheri ni nafsi zao wao wenyewe.

Mafunzo
  1. Mkazo katika kuacha swala za Ijumaa, na kwamba hilo ni katika madhambi makubwa.
  2. Amesema Nawawi: Hapa ni kwamba Ijumaa ni faradhi kwa kila mmoja.
  3. Sheria ya kuweka Mimbari kwa ajili ya hotuba.
  4. Amesema Assanadi: Maana yake ni kwamba moja kati ya mambo ni lazima litokee hakuna namna, ima kukoma kuacha swala za Ijumaa, au Mwenyezi Mungu kupiga muhuri juu ya mioyo yao, kwani kuzoea kuacha Ijumaa hujaza mfuniko juu ya moyo, na kuiweka mbali nafsi na mambo ya ibada.
  5. Ni wajibu kwa mtoa mawaidha na mkumbushaji kuficha majina ya watu anaotaka kuwazungumzia katika mawaidha; kwa sababu hilo huleta msukumo zaidi wa kukubali nasaha, na kuzitekeleza amri.
Marejeo

صحيح مسلم (2/ 591) (865). النهاية في غريب الحديث والأثر (964). البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (17/ 250).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Virtue of Friday

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com