Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Atakayeacha Ijumaa tatu kwa kuzipuuzia; Mwenyezi Mungu hupiga muhuri katika moyo wake

عَنْ أَبِي الْجَعْدِ الضَّمْرِيِّ رَضيَ اللهُ عنهُ، وَكَانَتْ لَهُ صُحْبَةٌ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ تَرَكَ ثَلَاثَ جُمَعٍ تَهَاوُنًا بِهَا طَبَعَ اللَّهُ عَلَى قَلْبِهِ».
Kutoka kwa Abul Ja'di Adh-dhwamri radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa na uswahaba, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema: "Atakayeacha Ijumaa tatu kwa kuzipuuzia; Mwenyezi Mungu hupiga muhuri katika moyo wake"
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoacha swala ya Ijumaa, na kwamba mwenye kuacha swala ya Ijumaa mara tatu kwa kupuuza na uzembe pasina udhuru basi Mwenyezi Mungu atapiga na kufunika juu ya moyo wake na kizibo kinachozuia kuingia kheri yoyote ndani ya nafsi yake.

Mafunzo
  1. Ameeleza bin Mundhiri kuwa kuna makubaliano ya wanachuoni wote kuwa swala ya Ijumaa ni faradhi ya lazima kwa kila mtu.
  2. Ahadi mbaya kwa atakayeacha swala ya Ijumaa kwa kupuuza, kwamba Mwenyezi Mungu atapiga muhuri juu ya moyo wake.
  3. Atakayeacha swala ya Ijumaa kwa dharura huyu haingii katika ahadi hii mbaya.
  4. Amesema Shaukani: Kauli yake: (Ijumaa tatu), inategemea maana mbili, kuacha kwa ujumla sawa sawa zimefuatana Ijumaa hizo au zimetofautiana, hata akiacha katika kila mwaka Ijumaa moja basi Mwenyezi Mungu angepiga muhuri juu ya moyo wake baada ya Ijumaa ya tatu, na ndivyo hadithi inavyoonyesha, na maana ya pili nikuwa inakusudiwa Ijumaa tatu mfululizo.
Marejeo

سنن أبي داود (2/ 284) (1052). سنن الترمذي (1/ 630) (500). سنن النسائي (3/ 88) (1369). سنن ابن ماجه (2/ 213) (1125). مسند أحمد (24/ 255) (15498). النهاية في غريب الحديث والأثر (557). شرح سنن أبي داود للعباد (134/ 3).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Virtue of Friday

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com