Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Swala ya Ijumaa

Hadithi 8

Utakapomwambia mwenzako: Nyamaza, siku ya Ijumaa, na imamu akihutubu, basi utakuwa umefanya mchezo

عن أبِي هُرَيرةَ رضي الله عنه أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلمَ قال: «إذا قُلْتَ لِصَاحِبِكَ: أَنْصِتْ، يومَ الجمعةِ، والْإِمامُ يَخْطُبُ، فَقَدْ لَغَوْتَ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Utakapomwambia mwenzako: Nyamaza, siku ya Ijumaa, na imamu akihutubu, basi utakuwa umefanya mchezo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa katika adabu za wajibu kwa atakayehudhuria hotuba ya Ijumaa: Ni kunyamaza na kumsikiliza hatibu; ili mtu azingatie mawaidha, nakuwa atakayezungumza walau kwa jambo dogo, na imamu akihutubu, akasema kumwambia mwenzie: "Nyamaza" na "Sikiliza", basi zitakuwa zimempita fadhila za swala ya Ijumaa.

Mafunzo
  1. Uharamu wa mazungumzo wakati wa hotuba, hata kama ni kuzia uovu au kujibu salamu au kumuombea dua aliyepiga chafya.
  2. Anaondolewa katika katazo hili atayemsemesha imamu au imamu akamsemesha yeye.
  3. Inafaa kuzungumza kati ya hotuba mbili.
  4. Akitajwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na imamu akiwa katika hotuba basi unatakiwa kumswalia kwa siri, na hivyo hivyo kuitikia dua.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 13) (934). صحيح مسلم (2/ 583) (851). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص244). تنبيه الأفهام، للعثيمين (2/ 307). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 195). فتح الباري، لابن حجر (2/ 409). تاج العروس من جواهر القاموس، لمحمّد الحسيني الزَّبيدي (39/ 463).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakaye koga siku ya Ijumaa josho la janaba, kisha akatoka katika saa ya kwanza ni kana kwamba katoa sadaka ya ngamia

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنِ اغْتَسَلَ يَوْمَ الجُمُعَةِ غُسْلَ الجَنَابَةِ ثُمَّ رَاحَ، فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ بَدَنَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الثَّانِيَةِ، فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ بَقَرَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الثَّالِثَةِ، فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ كَبْشًا أَقْرَنَ، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الرَّابِعَةِ، فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ دَجَاجَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الخَامِسَةِ، فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ بَيْضَةً، فَإِذَا خَرَجَ الإِمَامُ حَضَرَتِ المَلاَئِكَةُ يَسْتَمِعُونَ الذِّكْرَ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakaye koga siku ya Ijumaa josho la janaba, kisha akatoka katika saa ya kwanza ni kana kwamba katoa sadaka ya ngamia, na atakayetoka katika saa ya pili ni kana kwamba katoa sadaka ya ng'ombe, na atakayetoka katika saa ya tatu ni kana kwamba katoa sadaka ya kondoo, na atakayetoka katika saa ya nne ni kana kwamba katoa sadaka ya kuku, na atakaye kwenda katika saa ya tano ni kama katoa yai, akitoka imamu Malaika wanahudhuria kusikiliza ukumbusho".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu fadhila za kuwahi kwenda kuswali swala ya Ijumaa mapema. Na kuwasili mapema kunaanza tangu kuchomoza jua hadi kuwasili kwa Imam; Nazo ni saa tano, na zinagawanywa katika sehemu tano kulingana na muda kati ya kuchomoza kwa jua mpaka kuingia kwa imamu na kupanda kwake juu ya mimbari kutoa hotuba. Ya kwanza: Atakayeoga josho kamili, kama kuoga janaba, kisha akaenda katika msikiti wa Ijumaa katika saa ya kwanza, ni kama katoa sadaka ya ngamia. Ya pili: Mwenye kwenda saa ya pili ni kama katoa sadaka ya ng'ombe. Ya tatu: Yeyote atakayekwenda saa ya tatu ni kama ametoa sadaka kondoo dume mwenye pembe. Ya nne: Mwenye kwenda katika saa ya nne ni kama ametoa sadaka kuku. Ya tano: Mwenye kwenda saa tano, ni kama ametoa yai katika sadaka. Anapotoka imamu kwenda kutoa hotuba; Malaika waliokaa milangoni huacha kuwaandikia thawabu wale wanaoingia msikitini mmoja mmoja, na huja kusikiliza ukumbusho na hotuba.

Mafunzo
  1. Himizo la kuoga siku ya Ijumaa kabla ya kwenda kuswali.
  2. Fadhila za kuwahi swala ya Ijumaa kuanzia saa za mwanzo wa mchana.
  3. Himizo la kwenda mbio katika matendo mema.
  4. Malaika huhudhuria swala ya Ijumaa na kusikiliza hotuba.
  5. Malaika wako katika milango ya misikiti, wakiwaandikia wale wanaokuja, mmoja baada ya mwingine, wanapokuja kwa ajili ya Swala ya Ijumaa.
  6. Amesema bin Rajab: Kauli yake: “Mwenye kuoga siku ya Ijumaa kisha akaondoka” Inaashiria kuwa josho lililopendekezwa kwa siku ya Ijumaa linaanza kwa kuchomoza alfajiri, na mwisho wake ni muda wa kwenda katika swala ya Ijumaa.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 3) (881). صحيح مسلم (2/ 582) (850). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، عبد الله البسام (ص244). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (2/ 308). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، إسماعيل الأنصاري (1/ 196). معالم السنن (شرح سنن أبي داود)، أبو سليمان الخطابي (1/ 109). تهذيب اللغة، محمد الأزهري (14/ 102).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayekuja miongoni mwenu kwa ajili ya Ijumaa basi na aoge

عن عَبْدِ اللهِ بْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: «‌مَنْ ‌جَاءَ ‌مِنْكُمُ ‌الْجُمُعَةَ فَلْيَغْتَسِلْ».
kutoka kwa Abdullahi bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Atakayekuja miongoni mwenu kwa ajili ya Ijumaa basi na aoge".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anasisitiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa atakayetaka kuja kwa ajili ya swala ya Ijumaa basi inapendeza kwake kuoga, mfano wa kuoga kwake josho la janaba.

Mafunzo
  1. Mkazo wa kuoga kwa ajili ya Ijumaa, nakuwa hilo ni sunna kwa muumini siku ya Ijumaa na ikiwa wakati anataka kwenda kuswali ndio bora zaidi.
  2. Kutilia manani swala la usafi na harufu nzuri ni katika tabia njema za muislamu na adabu zake, na amri inakuwa na mkazo zaidi wakati wa kukutana na watu na kukaa nao, hasa hasa katika mikusanyiko na swala za jamaa.
  3. Tamko katika hadithi linamuhusu mwenye uwajibu wa kuswali Ijumaa; kwa sababu yeye ndiye anayekwenda kuswali.
  4. Ni lazima kwa mwenye kwenda katika swala ya Ijumaa awe msafi, aoge ili harufu iondoke katika mwili wake na ajitie manukato, na ikiwa atatawadha pekee pia itatosha.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 81) (1294). صحيح مسلم (1/ 99) (103). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص239). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (2/ 302). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 192).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com