Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Adhana na Iqama.

Hadithi 10

Mtakaposikia wito (Adhana), basi semeni mfano wa yale ayasemayo muadhini

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا سَمِعْتُمُ النِّدَاءَ، فَقُولُوا مِثْلَ مَا يَقُولُ المُؤَذِّنُ».
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mtakaposikia wito (Adhana), basi semeni mfano wa yale ayasemayo muadhini".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anahimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumjibu muadhini wakati wa kumsikia, na hii ni kwa sisi kusema mfano wa ayasemayo, sentensi kwa sentensi, Anaposema Allaahu Akbaru nasi tunasema Allaahu Akbaru, na anapotamka shahada mbili, nasi tunazitamka baada yake, Linaondolewa tamko la: (Hayya a'las swalaa, Hayya a'lal falaah) hapo tutasema baada yake: Laa haulaa walaa quwwata illaa billaah.

Mafunzo
  1. Atamfuatisha muadhini wa kwanza baada ya kumaliza wa kwanza, hata kama waadhini watakuwa wengi; kwa sababu ya ujumla wa hadithi hii.
  2. Atamjibu muadhini katika hali zake zote, ikiwa atakuwa hayuko chooni au akikidhi haja.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 126) (611). صحيح مسلم (1/ 288) (383). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص120). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 98).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Itakaposimamishwa swala na kikatengwa chakula cha usiku basi anzeni na chakula cha usiku

عن عائشة وعبد الله بن عمر وأنس بن مالك رضي الله عنهم مرفوعاً: «إِذَا أُقِيمَت الصَّلاَة، وحَضَرَ العَشَاء، فَابْدَءُوا بِالعَشَاء».
Kutoka kwa Aisha na Abdillahi bin Omar na Anasi bin Maliki -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u: "Itakaposimamishwa swala na kikatengwa chakula cha usiku basi anzeni na chakula cha usiku".
Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim katika riwaya zake zoteDarajaSahihi
Maelezo

Itakaposimamishwa swala, na chakula au kinywaji kikawa kiko tayari, inatakiwa kuanza na kula au kunywa mpaka yakatike matamanio ya mwenye kuswali, na akili yake asikaye anafikiria hilo, na aingie katika swala, na sharti ya hilo ni muda wa swala kutokuwa mfinyu, na uwepo wa uhitaji na kufikiria chakula, na hii inathibitisha ukamilifu wa sheria na kuzingatia kwake haki za nafsi pamoja na wepesi na upole.

Marejeo

الإلمام بشرح عمدة الأحكام لإسماعيل الأنصاري، ط1، دار الفكر، دمشق، 1381هـ. تيسير العلام شرح عمدة الأحكام للبسام، حققه وعلق عليه وخرج أحاديثه وصنع فهارسه: محمد صبحي بن حسن حلاق، ط10، مكتبة الصحابة، الإمارات - مكتبة التابعين، القاهرة، 1426هـ. تنبيه الأفهام شرح عمدة لأحكام لابن عثيمين، ط1، مكتبة الصحابة، الإمارات، 1426هـ. عمدة الأحكام من كلام خير الأنام صلى الله عليه وسلم لعبد الغني المقدسي، دراسة وتحقيق: محمود الأرناؤوط، مراجعة وتقديم: عبد القادر الأرناؤوط، ط2، دار الثقافة العربية، دمشق ، بيروت، مؤسسة قرطبة، 1408هـ. صحيح البخاري، تحقيق: محمد زهير بن ناصر الناصر، ط1، دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم: محمد فؤاد عبد الباقي)، 1422هـ. صحيح مسلم، تحقيق: محمد فؤاد عبد الباقي، دار إحياء التراث العربي، بيروت، 1423هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayesema wakati anamsikia muadhini: Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake, nimeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ni Mola wangu na Muhammadi kuwa ni Mtume na Uislamu kuwa ni dini, atasamehewa dhambi zake

عَنْ سَعْدِ بْنِ أَبِي وَقَّاصٍ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ: «مَنْ قَالَ حِينَ يَسْمَعُ الْمُؤَذِّنَ أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، رَضِيتُ بِاللهِ رَبًّا وَبِمُحَمَّدٍ رَسُولًا، وَبِالْإِسْلَامِ دِينًا، غُفِرَ لَهُ ذَنْبُهُ».
Kutoka kwa Sa'd Bin Abi Waqaas Allah amridhie kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayesema wakati anamsikia muadhini: Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake, nimeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ni Mola wangu na Muhammadi kuwa ni Mtume na Uislamu kuwa ni dini, atasamehewa dhambi zake".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema wakati akimsikia muadhini "Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika wake", Yaani: Nina kiri na kukubali na ninatoa habari kuwa hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kila mwenye kuabudiwa kinyume na yeye ni batili, "Na kuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake" Yaani: Yeye ni mja wala haabudiwi, na ni Mjumbe wake haongopi, "Nimeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi" Yaani: Kwa ulezi wake na uungu wake na majina yake na sifa zake, "Na Muhammadi kuwa ni Mtume" Yaani: Kwa yote aliyotumwa kwayo, na akatufikishia, "Na Uislamu" Yaani: Kwa hukumu zote za Uislamu ikiwemo maamrisho na makatazo, "Dini" Yaani: Kwa itikadi na kutii, "Atasamehewa dhambi zake" Yaani: Katika dhambi ndogo.

Mafunzo
  1. Kuirudia rudia dua hii wakati wa kusikia adhana ni miongoni mwa mambo yanayofuta madhambi.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 290) (386). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 39). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لملا علي القاري (2/ 562). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 254). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (2/ 771).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Waadhini wote watakuwa na shingo ndefu zaidi kuliko watu wote siku ya Kiyama

عَنْ مُعَاوِيَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «الْمُؤَذِّنُونَ أَطْوَلُ النَّاسِ أَعْنَاقًا يَوْمَ الْقِيَامَةِ».
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Waadhini wote watakuwa na shingo ndefu zaidi kuliko watu wote siku ya Kiyama".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba waadhini wote ambao huwaita watu kuja katika swala ndio watakuwa watu wenye shingo ndefu zaidi siku ya Kiyama kwa sababu ya utukufu wa amali yao, na wingi wa kheri zao, na ukubwa wa malipo yao.

Mafunzo
  1. Ubora wa Adhana na himizo lake.
  2. Kumebainishwa utukufu wa waadhini, na daraja lao la juu siku ya Kiyama.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 290) (387). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 251). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 31). شرح صحيح مسلم، النووي (4/ 89). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 768).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Katika sunna atakaposema muadhini katika adhana ya Alfajiri: Hayya Alal-fala'h, aseme: Aswalatu khairu mmina nnaum. Yaani: Swala ni bora kuliko usingizi

عَنْ أَنَسٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: مِنَ السُّنَّةِ إِذَا قَالَ الْمُؤَذِّنُ فِي أَذَانِ الْفَجْرِ حَيَّ عَلَى الْفَلَاحِ، قَالَ: الصَّلَاةُ خَيْرٌ مِنَ النَّوْمِ.
Imepokelewa kutoka kwa Anas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake amesema: Katika sunna atakaposema muadhini katika adhana ya Alfajiri: Hayya Alal-fala'h, aseme: Aswalatu khairu mmina nnaum. Yaani: Swala ni bora kuliko usingizi.
Imepokelewa na Ibnu Khuzaymah, Addar- Alqutni na AlbayhaqyDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Anasi bin Maliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kuwa miongoni mwa mambo aliyoyakubali Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika sunna zake, ni Muadhini kusema katika Adhana Alfajiri pekee, baada ya kauli yake: "Hayya a'lal falaah" asema: "Asswalaatu khairuni minan nauum" Yaani swala ni bora kuliko usingizi.

Mafunzo
  1. Kauli yake: "Katika sunna": Yaani: Sunna ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, inahukumu ya kufikishwa kwa Mtume, yaani inanasibishwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  2. Sunna asema Muadhini katika swala ya Alfajiri baada ya: Hayya a'lal falaah: Aseme: Asswalaatu khairun minan nauum, yaani: Swala ni bora kuliko usingizi, mara mbili; kwa sababu swala ya Alfajiri watu wengi hulala, na wanaamka kwenda katika swala kutoka usingizini, ikahusika swala ya Alfajiri pekee pasina swala nyinginezo.
Marejeo

صحيح ابن خزيمة (1/ 233) (386). سنن الدارقطني (1/ 454) (944). السنن الكبرى للبيهقي (1/ 623) (1984). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (1/ 510). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (2/ 239). فتاوى اللجنة الدائمة، اللجنة الدائمة للبحوث العلمية والإفتاء (6/ 62).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayesema wakati anasikia adhana: Allaahumma rabba haadhihid da'watit taamma, was swalaatul qaaima, aati Muhammadanil wasiilata wal fadhwiila, wab'ath-huu maqaaman mahmuudanil ladhii wa a'ttah, (Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wa wito huu uliotimia, na swala iliyosimama, mpe Muhammad utetezi na fadhila, na umfufue mahali pakusifiwa ulipomuahidi) basi utakuwa halali kwake utetezi wangu siku ya Kiyama

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رضي الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ قَالَ حِينَ يَسْمَعُ النِّدَاءَ: اللَّهُمَّ رَبَّ هَذِهِ الدَّعْوَةِ التَّامَّةِ، وَالصَّلاَةِ القَائِمَةِ، آتِ مُحَمَّدًا الوَسِيلَةَ وَالفَضِيلَةَ، وَابْعَثْهُ مَقَامًا مَحْمُودًا الَّذِي وَعَدْتَهُ، حَلَّتْ لَهُ شَفَاعَتِي يَوْمَ القِيَامَةِ».
Na kutoka kwa Jaabir bin Abdillah -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayesema wakati anasikia adhana: Allaahumma rabba haadhihid da'watit taamma, was swalaatul qaaima, aati Muhammadanil wasiilata wal fadhwiila, wab'ath-huu maqaaman mahmuudanil ladhii wa a'ttah, (Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wa wito huu uliotimia, na swala iliyosimama, mpe Muhammad utetezi na fadhila, na umfufue mahali pakusifiwa ulipomuahidi) basi utakuwa halali kwake utetezi wangu siku ya Kiyama".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema wakati amemsikia muadhini baada ya kumaliza adhana: "Ewe Mwenyezi Mungu Mola wa wito huu" nayo ni matamshi ambayo hutumika kuita katika ibada ya Mwenyezi Mungu na swala, "Uliotimia" uliokamilika, wito wa tauhidi na ujumbe, "na swala iliyosimama" yenye kudumu ambayo itasimamishwa hivi punde, "mpe" mgawie, "Muhammadi utetezi" na cheo cha juu peponi ambacho hakimstahiki mwingine ila yeye rehema na amani ziwe juu yake, "na fadhila" cheo cha juu zaidi ya vyeo vya viumbe, "na umfufue" na umpe "nafasi yenye kusifiwa" anayosifiwa mwenye kuwanayo; nao ni utetezi mkuu wa siku ya Kiyama, "uliyomuahidi" kwa kauli yako "Huenda akakufufua Mola wako katika nafasi yenye kusifiwa" ili iwe yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Atakayeomba dua hii atastahiki kuupata utetezi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ya Kiyama.

Mafunzo
  1. Sheria ya kuomba dua hii baada ya kumaliza kurudia nyuma ya muadhini, na ambaye hatosikia adhana; basi hatakiwi kuisema.
  2. Ubora wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kiasi kwamba amepewa uwakala na fadhila na nafasi na utetezi mkuu wa kutetea kuhukumiwa baina ya viumbe.
  3. Kuthibitisha utetezi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake; kwa kauli yake: "Ataupata utetezi wangu siku ya Kiyama".
  4. Utetezi wake rehema na amani ziwe juu yake utakuwa kwa wale waliotenda madhambi makubwa katika umma wake ili wasiingie motoni, au aliyeingia atoke, au katika kuingia peponi pasina hesabu, au kunyanyuliwa daraja aliyeingia.
  5. Amesema Attwayyibi: kuanzia mwanzo wa "Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu" huu ndio wito uliotimia, na maneno "Hayya a'la" (njooni katika) ndio swala iliyosimama katika kauli yake wanasimamisha swala, na inawezekana kuwa makusudio ya swala hapa ni dua, na kwa mujibu wa hili kauli yake "na swala iliyosimama" ni kubainishwa wito uliyotimia, na inawezekana kuwa makusudio yake ni swala iliyozoeleka wanayoitwa kwayo kwa wakati huo, na ndilo lililokaribu na maana halisi.
  6. Amesema Al-Mulhab: Katika hadithi hii kuna himizo la kuomba dua katika nyakati za swala; kwa sababu ni hali zinazotarajiwa zaidi kujibiwa dua.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 126) (614). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (1/ 550). فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (1/ 488). شرح سنن أبي داود، لعبد المحسن العباد (73/ 18).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakapo sema Muadhini: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema mmoja wenu: Allahu Akbaru Allahu Akbaru

عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «إِذَا قَالَ الْمُؤَذِّنُ: اللهُ أَكْبَرُ اللهُ أَكْبَرُ، فَقَالَ أَحَدُكُمُ: اللهُ أَكْبَرُ اللهُ أَكْبَرُ، ثُمَّ قَالَ: أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، قَالَ: أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، ثُمَّ قَالَ: أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ، قَالَ: أَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ، ثُمَّ قَالَ: حَيَّ عَلَى الصَّلَاةِ، قَالَ: لَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللهِ، ثُمَّ قَالَ: حَيَّ عَلَى الْفَلَاحِ، قَالَ: لَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللهِ، ثُمَّ قَالَ: اللهُ أَكْبَرُ اللهُ أَكْبَرُ، قَالَ: اللهُ أَكْبَرُ اللهُ أَكْبَرُ، ثُمَّ قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ مِنْ قَلْبِهِ دَخَلَ الْجَنَّةَ».
Imepokewa kutoka kwa Omar Bin Khattwab- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Atakapo sema Muadhini: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema mmoja wenu: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema: Ash-hadu An laa ilaha ila llahu, akasema: Ash-hadu An laa ilaha ila llahu. kisha akasema: Ash-hadu Anna Muhammadan Rasuulullahi, Akasema: Ash-hadu Anna Muhammadan Rasuulullahi, kisha akasema: Hayya ala Swalaah, akasema: Laa Haula wala Quwwata ila Billahi, kisha akasema: Hayya ala lfalaah, akasema: Laa Haula walaa Quwwata ila Billahi, kisha akasema: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, akasema: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema: Laa ilaha ila llahu, akasema: Laa ilaha ila llahu, kutoka ndani ya moyo wake, basi ataingia peponi".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Adhana ni kuwatangazia watu kuwa muda wa swala umeingia, na maneno ya adhana ni maneno yaliyokusanya itikadi ya imani. Na katika hadithi hii anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kinachotakiwa kisheria wakati wa kusikia adhana, nako msikiaji asema kama anavyosema muadhini, muadhini akisema: "Allahu Akbaru" Mwenye kusikia naye anasema: "Allahu Akbaru" ataendelea hivyo, isipokuwa katika kauli ya muadhini "Hayya alas swalaa", "Hayya alal falaah, atasema mwenye kusikia: "Laa haulaa wala quwwata illaa billaah". Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakaye rudia rudia nyuma ya muadhini kwa utakasifu kutoka moyoni mwake ataingia peponi. Na maana ya maneno ya adhana ni: "Allahu Akbaru": Yaani: Yeye mtakasifu ni mtakasifu na ni mtukufu na ni mkubwa kuliko kila kitu. "Ash-hadu an laa ilaaha illa llaah": Yaani: Hapana muabudiwa wa haki zaidi ya Allah. "Ash-hadu anna Muhammadan Rasuulu llaah" Yaani: Nina kiri na nina shuhudia kwa ulimi wangu na moyo wangu, yakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, alimtuma Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ni wajibu kumtii. "Hayya alas swalaa", Yaani: Njooni katika swala, na kauli ya mwenye kusikia: "Laa haulaa walaa quwwata illa billaah", Yaani hakuna ujanja wa kuvimaliza vikwazo vya ibada, wala nguvu ya kuzifanya na wala uwezo wa chochote ila ni kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Hayya alal falaah", Njooni katika sababu ya kufanikiwa, nako ni kufuzu kwa Pepo na kusalimika na moto.

Mafunzo
  1. Fadhila za kumjibu muadhini kwa mfano wa yale anayosema, isipokuwa katika hayyalaa mbili, atasema: "Laa haulaa walaa quwwata illa billaah".
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 289) (385)، إكمال المعلم (2/253)، شرح النووي على مسلم (4/88)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (9/ 116).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Mtakapo msikia muadhini basi semeni mfano wa yale anayo yasema, kisha mnitakie rehema

عَنْ ‌عَبْدِ اللهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ رضي الله عنها أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «إِذَا سَمِعْتُمُ الْمُؤَذِّنَ فَقُولُوا مِثْلَ مَا يَقُولُ، ثُمَّ صَلُّوا عَلَيَّ، فَإِنَّهُ مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلَاةً صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ بِهَا عَشْرًا، ثُمَّ سَلُوا اللهَ لِيَ الْوَسِيلَةَ، فَإِنَّهَا مَنْزِلَةٌ فِي الْجَنَّةِ، لَا تَنْبَغِي إِلَّا لِعَبْدٍ مِنْ عِبَادِ اللهِ، وَأَرْجُو أَنْ أَكُونَ أَنَا هُوَ، فَمَنْ سَأَلَ لِيَ الْوَسِيلَةَ حَلَّتْ لَهُ الشَّفَاعَةُ».
kutoka kwa Abdillah bin Amri bin Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yao- Yakwamba amemsikia Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake anasema: "Mtakapo msikia muadhini basi semeni mfano wa yale anayo yasema, kisha mnitakie rehema, ni kwamba yule atakaye nitakia rehema mara moja Allah atamtakia rehema mara kumi, kisha niombeeni kwa Allah ukaribu, hakika ukaribu huo ni daraja ndani ya Pepo, halipati daraja hilo isipokuwa mja miongoni mwa waja wa Allah, na ninatarajia niwe mimi ndiye huyo mja huyo, na atakayeniombea mimi ukaribu ataupata uombezi".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameelekeza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mwenye kumsikia muadhini kwa ajili ya swala basi naye amfuatilize nyuma yake, aseme mfano wa kauli zake, isipokuwa haiala mbili (Hayya alas-swalaa, na hayya alal falaah), atasema baada yake: Laa haulaa walaa quwwata illa billaah, kisha atamtakia rehema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baada ya kumalizika kwa adhana, kwani atakayemtakiwa rehema mara moja, basi Mwenyezi Mungu atamtakia rehema kumi kwa sababu ya dua hiyo moja, na maana ya Mwenyezi Mungu kumtakia rehema mja wake: Ni kumsifu mja wake mbele ya Malaika. Kisha akaamrisha kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ukaribu -Rehema na amani ziwe juu yake-, nayo ni nafasi iliyoko peponi, na ni daraja ya juu zaidi kuliko zote, haimstahiki na wala haiwezekani nafasi hiyo ila kwa mja mmoja katika waja wote wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na ninataraji mimi kuwa ndiye mja huyo, na alisema hivyo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa sababu ya kujinyenyekeza; kwa sababu nafasi hiyo ikiwa haistahiki ila kwa mtu mmoja, hawezi kuwa mmoja huyo zaidi ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-; kwa sababu yeye ndiye mbora wa viume wote. Kisha akabainsha -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayemuombea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nafasi ya ukaribu basi ataupata utetezi wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.

Mafunzo
  1. Himizo la kumjibu muadhini.
  2. Fadhila za kumtakia rehema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baada ya kumjibu muadhini.
  3. Himizo la kumuombea ukaribu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baada ya kumtakia rehema.
  4. Kumebainishwa maana ya ukaribu, na ukubwa wa nafasi yake, kiasi kwamba haumstahiki ila mja mmoja pekee.
  5. Kumebainishwa ubora wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kiasi ambacho kapendelewa nafasi hiyo ya juu.
  6. Atakayemuomba Mwenyezi Mungu ukaribu kwa ajili ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- basi atastahiki kupata uombezi.
  7. Kumebainishwa unyenyekevu wake -Rehema na amani ziwe juu yake- kiasi kwamba ameuomba umma wake umuombee dua ili apate nafasi hiyo, pamoja nakuwa nafasi hiyo itakuwa yake.
  8. Upana wa fadhila za Mwenyezi Mungu na rehema yake, jema moja linalipwa kwa mema kumi mfano wake.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 288) (384)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (9/ 111 (9/ 109)، المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (2/ 13).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
8 kati ya 10
Hadithi 10
  1. Mtakaposikia wito (Adhana), basi semeni mfano wa yale ayasemayo muadhini
  2. Itakaposimamishwa swala na kikatengwa chakula cha usiku basi anzeni na chakula cha usiku
  3. Atakayesema wakati anamsikia muadhini: Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake, nimeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ni Mola wangu na Muhammadi kuwa ni Mtume na Uislamu kuwa ni dini, atasamehewa dhambi zake
  4. Waadhini wote watakuwa na shingo ndefu zaidi kuliko watu wote siku ya Kiyama
  5. Katika sunna atakaposema muadhini katika adhana ya Alfajiri: Hayya Alal-fala'h, aseme: Aswalatu khairu mmina nnaum. Yaani: Swala ni bora kuliko usingizi
  6. Atakayesema wakati anasikia adhana: Allaahumma rabba haadhihid da'watit taamma, was swalaatul qaaima, aati Muhammadanil wasiilata wal fadhwiila, wab'ath-huu maqaaman mahmuudanil ladhii wa a'ttah, (Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wa wito huu uliotimia, na swala iliyosimama, mpe Muhammad utetezi na fadhila, na umfufue mahali pakusifiwa ulipomuahidi) basi utakuwa halali kwake utetezi wangu siku ya Kiyama
  7. Atakapo sema Muadhini: Allahu Akbaru Allahu Akbaru, kisha akasema mmoja wenu: Allahu Akbaru Allahu Akbaru
  8. Mtakapo msikia muadhini basi semeni mfano wa yale anayo yasema, kisha mnitakie rehema
  9. Ewe Bilali, simamisha swala, tupe raha kwayo
  10. Kati ya kila adhana mbili kuna swala, kati ya kila adhana mbili kuna swala" Kisha akasema katika mara ya tatu: "Kwa atakayetaka

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com