Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Mtakaposikia wito (Adhana), basi semeni mfano wa yale ayasemayo muadhini

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا سَمِعْتُمُ النِّدَاءَ، فَقُولُوا مِثْلَ مَا يَقُولُ المُؤَذِّنُ».
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mtakaposikia wito (Adhana), basi semeni mfano wa yale ayasemayo muadhini".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anahimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumjibu muadhini wakati wa kumsikia, na hii ni kwa sisi kusema mfano wa ayasemayo, sentensi kwa sentensi, Anaposema Allaahu Akbaru nasi tunasema Allaahu Akbaru, na anapotamka shahada mbili, nasi tunazitamka baada yake, Linaondolewa tamko la: (Hayya a'las swalaa, Hayya a'lal falaah) hapo tutasema baada yake: Laa haulaa walaa quwwata illaa billaah.

Mafunzo
  1. Atamfuatisha muadhini wa kwanza baada ya kumaliza wa kwanza, hata kama waadhini watakuwa wengi; kwa sababu ya ujumla wa hadithi hii.
  2. Atamjibu muadhini katika hali zake zote, ikiwa atakuwa hayuko chooni au akikidhi haja.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 126) (611). صحيح مسلم (1/ 288) (383). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص120). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 98).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Adhana na Iqama.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com