Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Katika sunna atakaposema muadhini katika adhana ya Alfajiri: Hayya Alal-fala'h, aseme: Aswalatu khairu mmina nnaum. Yaani: Swala ni bora kuliko usingizi

عَنْ أَنَسٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: مِنَ السُّنَّةِ إِذَا قَالَ الْمُؤَذِّنُ فِي أَذَانِ الْفَجْرِ حَيَّ عَلَى الْفَلَاحِ، قَالَ: الصَّلَاةُ خَيْرٌ مِنَ النَّوْمِ.
Imepokelewa kutoka kwa Anas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake amesema: Katika sunna atakaposema muadhini katika adhana ya Alfajiri: Hayya Alal-fala'h, aseme: Aswalatu khairu mmina nnaum. Yaani: Swala ni bora kuliko usingizi.
Imepokelewa na Ibnu Khuzaymah, Addar- Alqutni na AlbayhaqyDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Anasi bin Maliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kuwa miongoni mwa mambo aliyoyakubali Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika sunna zake, ni Muadhini kusema katika Adhana Alfajiri pekee, baada ya kauli yake: "Hayya a'lal falaah" asema: "Asswalaatu khairuni minan nauum" Yaani swala ni bora kuliko usingizi.

Mafunzo
  1. Kauli yake: "Katika sunna": Yaani: Sunna ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, inahukumu ya kufikishwa kwa Mtume, yaani inanasibishwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  2. Sunna asema Muadhini katika swala ya Alfajiri baada ya: Hayya a'lal falaah: Aseme: Asswalaatu khairun minan nauum, yaani: Swala ni bora kuliko usingizi, mara mbili; kwa sababu swala ya Alfajiri watu wengi hulala, na wanaamka kwenda katika swala kutoka usingizini, ikahusika swala ya Alfajiri pekee pasina swala nyinginezo.
Marejeo

صحيح ابن خزيمة (1/ 233) (386). سنن الدارقطني (1/ 454) (944). السنن الكبرى للبيهقي (1/ 623) (1984). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (1/ 510). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (2/ 239). فتاوى اللجنة الدائمة، اللجنة الدائمة للبحوث العلمية والإفتاء (6/ 62).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Adhana na Iqama.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com