Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Watu wa makaburini.

Hadithi 2

Hakika hao wawili wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa makosa makubwa, ama mmoja wao alikuwa hajistiri na mkojo, na ama mwingine alikuwa akitembea kwa kuchonganisha watu

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ: مَرَّ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِقَبْرَيْنِ، فَقَالَ: «إِنَّهُمَا لَيُعَذَّبَانِ، وَمَا يُعَذَّبَانِ فِي كَبِيرٍ، أَمَّا أَحَدُهُمَا فَكَانَ لاَ يَسْتَتِرُ مِنَ البَوْلِ، وَأَمَّا الآخَرُ فَكَانَ يَمْشِي بِالنَّمِيمَةِ» ثُمَّ أَخَذَ جَرِيدَةً رَطْبَةً، فَشَقَّهَا نِصْفَيْنِ، فَغَرَزَ فِي كُلِّ قَبْرٍ وَاحِدَةً، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، لِمَ فَعَلْتَ هَذَا؟ قَالَ: «لَعَلَّهُ يُخَفِّفُ عَنْهُمَا مَا لَمْ يَيْبَسَا».
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alipita Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika makaburi mawili, akasema: "Hakika hao wawili wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa makosa makubwa, ama mmoja wao alikuwa hajistiri na mkojo, na ama mwingine alikuwa akitembea kwa kuchonganisha watu" Kisha akachukua kuti bichi, akalikata vipande viwili, akapanda katika kila kaburi kipande kimoja, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwa nini umefanya hivi? Akasema: "Huenda yakawapunguzia kinachowapata kwa muda kabla hayajakauka".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alipita Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika makaburi mawili akasema: Hakika watu wa makaburi haya mawili wanaadhibiwa; na wala hawaadhibiwa katika jambo kubwa, hata kama ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, Ama mmoja wao alikuwa hajali katika kuhifadhi mwili wake na nguo zake kutokana na mkojo anapokidhi haja yake, Na mwingine alikuwa akitembea kati ya watu kwa uchonganishi, akinukuu maneno ya mtu mwingine kwa lengo la kuwadhuru na kuleta sintofahamu baina yao na ugomvi kati ya watu.

Mafunzo
  1. Uchonganishi na kuacha kujistiri na mkojo ni katika madhambi makubwa na ni katika sababu za adhabu za kaburini.
  2. Mwenyezi Mungu Mtukufu alifunua baadhi ya mambo yaliyofichikana kama adhabu za kaburini ili kuonyesha alama ya utume wake rehema na amani ziwe juu yake.
  3. Kitendo hiki cha kuchukua tawi na kulipasua vipande viwili na kuviweka juu ya makaburi ni maalumu kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu alimfunulia kuona hali za watu wa makaburi yale mawili, hakiwezi kuwa kipimo cha watu wengine, kwa sababu hakuna ajuaye hali za watu walioko kaburini.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 53) (218). صحيح مسلم (1/ 240) (292). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص43). خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص22). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 29).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika kaburi ndio kituo cha kwanza katika vituo vya Akhera, ikiwa mtu atasalimika nalo basi yajayo baada yake ni mepesi kuliko hili, na asiposalimika nalo basi yajayo baada yake ni magumu kuliko hili

عَن هَانِئ مَوْلَى عُثْمَانَ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: كَانَ عُثْمَانُ إِذَا وَقَفَ عَلَى قَبْرٍ بَكَى حَتَّى يَبُلَّ لِحْيَتَهُ، فَقِيلَ لَهُ: تُذْكَرُ الْجَنَّةُ وَالنَّارُ فَلَا تَبْكِي، وَتَبْكِي مِنْ هَذَا؟ فَقَالَ: إِنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: «إِنَّ الْقَبْرَ أَوَّلُ مَنْزِلٍ مِنْ مَنَازِلِ الْآخِرَةِ، فَإِنْ نَجَا مِنْهُ فَمَا بَعْدَهُ أَيْسَرُ مِنْهُ، وَإِنْ لَمْ يَنْجُ مِنْهُ فَمَا بَعْدَهُ أَشَدُّ مِنْهُ».
Kutoka kwa Haani, mwachwa huru wa Othmani radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Othmani anaposimama juu ya kaburi analia mpaka analowanisha ndevu zake, akaulizwa: Ukikumbuka pepo na Moto wala haulii, na unalia kwa sababu ya hili (kaburi)?! Akasema: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema: "Hakika kaburi ndio kituo cha kwanza katika vituo vya Akhera, ikiwa mtu atasalimika nalo basi yajayo baada yake ni mepesi kuliko hili, na asiposalimika nalo basi yajayo baada yake ni magumu kuliko hili".
Imepokelewa na Tirmidhi na bin MajahDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Alikuwa kiongozi wa waumini Othmani bin Affani radhi za Allah ziwe juu yake anaposimama juu ya kaburi analia sana, mpaka analowanisha ndevu zake, akaulizwa: Unakumbuka pepo na moto na wala haulii kwa shauku ya pepo wala hofu ya moto! na unalia kwa sababu ya kaburi? Akasema: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alieleza kuwa hakika kaburi ndio kituo cha kwanza katika vituo vya Akhera, mtu akisalimika na akaepukana na mabaya yaliyomo basi vituo vinavyofuata baada yake ni vyepesi mno, na asiposalimika kutokana na adhabu zake; basi adhabu zinazofuata baada yake ni kali kuliko hizo.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa hofu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyokuwa nayo Othmani radhi za Allah ziwe juu yake, pamoja nakuwa yeye ni miongoni mwa waliobashiriwa pepo.
  2. Sheria ya kulia wakati wa kukumbuka misukosuko ya kaburi na Kiyama.
  3. Kumethibitishwa neema za kaburi na adhabu zake.
  4. Tishio la adhabu za kaburi.
Marejeo

سنن الترمذي (4/ 142) (2308). سنن ابن ماجه (5/ 333) (4267). مشكاة المصابيح، للتبريزي (1/ 48). تحفة الأحوذي بشرح جامع الترمذي، المباركفوري (6/ 490). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (1/ 215).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com