Alikuwa kiongozi wa waumini Othmani bin Affani radhi za Allah ziwe juu yake anaposimama juu ya kaburi analia sana, mpaka analowanisha ndevu zake, akaulizwa: Unakumbuka pepo na moto na wala haulii kwa shauku ya pepo wala hofu ya moto! na unalia kwa sababu ya kaburi? Akasema: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alieleza kuwa hakika kaburi ndio kituo cha kwanza katika vituo vya Akhera, mtu akisalimika na akaepukana na mabaya yaliyomo basi vituo vinavyofuata baada yake ni vyepesi mno, na asiposalimika kutokana na adhabu zake; basi adhabu zinazofuata baada yake ni kali kuliko hizo.
- Kumebainishwa hofu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyokuwa nayo Othmani radhi za Allah ziwe juu yake, pamoja nakuwa yeye ni miongoni mwa waliobashiriwa pepo.
- Sheria ya kulia wakati wa kukumbuka misukosuko ya kaburi na Kiyama.
- Kumethibitishwa neema za kaburi na adhabu zake.
- Tishio la adhabu za kaburi.
سنن الترمذي (4/ 142) (2308). سنن ابن ماجه (5/ 333) (4267). مشكاة المصابيح، للتبريزي (1/ 48). تحفة الأحوذي بشرح جامع الترمذي، المباركفوري (6/ 490). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (1/ 215).