Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Majaribio hayaachi kumpata muumini wa kiume na muumini wa kike katika nafsi yake, na watoto wake, na mali yake mpaka atakapokutana na Mwenyezi Mungu ilhali hana dhambi hata moja."
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa: “Balaa na mtihani havikomi kwa muumini wa kiume na wa kike, katika afya yake na mwili wake, na kwa watoto wake, kama magonjwa, kifo, uasi na mengineyo, na katika mali yake kutiwa umasikini, kutoweka kwa biashara, kuibiwa, kuvurugika kwa maisha na dhiki katika riziki, na ugumu wa maisha, mpaka Mwenyezi Mungu atamfutia dhambi zake zote kwa mateso haya, ili atakapokutana na Mwenyezi Mungu atakuwa kasafishika na madhambi na maovu yote aliyoyafanya.
Mafunzo
Miongoni mwa huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake waumini ni kuwafutia madhambi yao katika dunia yao kupitia matatizo ya dunia na maafa yake.
Balaa pekee linafuta madhambi ila kwa sharti la imani, hivyo akisubiri mja na akawa hakulalamika basi analipwa.
Himizo la subira katika mambo yote, katika yale ayapendayo na anayoyachukia, awe na subira mpaka atekeleze aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu, na awe na subira mpaka akae mbali na yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu, akitaraji malipo ya Mwenyezi Mungu na kuogopa adhabu yake.
Kauli yake: “Kwa muumini mwanaume na mwanamke,” kuongeza neno “muumini wa kike” ndani yake ni ushahidi wa kutiliwa mkazo zaidi kwa wanawake. Vinginevyo, lau angesema: "Kwa muumini wa kiume," mwanamke angejumuishwa ndani yake; Kwa sababu hii si mahsusi kwa wanaume, basi ikiwa dhiki itampata mwanamke, naye anaahidiwa malipo kama hayo kwa kufutiwa madhambi na makosa.
Hili ni miongoni mwa mambo yanayomtia faraja mtu kwa yale anayokumbana nayo katika maumivu kila mara yanayosababishwa na mabalaa.
Marejeo
سنن الترمذي (4/ 204) (2399).
مسند أحمد (13/ 248) (7859).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 113).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص51).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 273).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 80).
Kutoka kwa Suhaib -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Ajabu iliyoje ya jambo la muumini, hakika jambo lake lote ni kheri, na hakuna hilo kwa yeyote ila kwa muumini, akipatwa na jambo lenye kufurahisha anashukuru ikawa hilo ni kheri kwake, na akipatwa na madhara anasubiri likawa hilo ni kheri kwake."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anastaajabu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, jambo na hali za muumini kwa namna ya kufurahishwa; Hii ni kwa sababu hali zake zote ni kheri, na sivyo hivyo kwa yeyote isipokuwa Muumini. Mambo mazuri yakimpata, anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo, analipwa kwa kushukuru. Ukimpata msiba husubiri na hutaraji malipo kwa Mwenyezi Mungu, na hupata malipo ya subira, hivyo anakuwa katika malipo kwa kila hali.
Mafunzo
Fadhila ya kushukuru nyakati za kheri na kuwa na subira wakati wa dhiki, mwenye kufanya hivyo atapata kheri zote za Dunia na Akhera, na asiyeshukuru juu ya neema, na wala havumilii juu ya msiba atakosa ujira na kupata mzigo (wa dhambi).
Fadhila ya Imani, na kwamba malipo kwa kila hali ni kwa watu wenye imani.
Kushukuru nyakati za kheri na subira wakati wa shida ni miongoni mwa sifa za waumini.
Kuamini maamuzi na Kadari za Mwenyezi Mungu humfanya Muumini kuridhika kabisa na hali zake zote, tofauti na kafiri ambaye hukasirika mara kwa mara pindi anapopatwa na madhara, na akipata neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu huacha kumtii Mwenyezi Mungu, na huenda mbali zaidi na kuzitumia katika kumuasi.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2295) (2999).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 82).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 197).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 59).
Imepokewa Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: Nuuman akashusha vidole vyake masikioni mwake-" "Hakika halali iko wazi, na hakika haramu iko wazi na kati ya halali na haramu kuna mambo yenye kutatiza, hawayajui mambo hayo wengi miongoni mwa watu, atakaye yaepuka mambo yenye kutatiza, basi atakuwa kaihifadhi dini yake na heshima yake, na atakayeingia katika mambo yenye kutatiza atakuwa kaingia katika haramu, ni kama mfano wa mchunga mifugo mwenye kuchungia kando kando ya mipaka wanahofiwa (mifugo wake) kuingia humo, tambueni na hakika kila Mfalme ana mipaka yake, na tambueni kuwa mipaka ya Mwenyezi Mungu ni makatazo yake, na tambueni kuwa katika mwili kuna kipande cha nyama, kikitengemaa mwili mzima unatengemaa, na kikiharibika, mwili mzima unaharibika, tambueni kipande hicho ni moyo."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kanuni kuu katika mambo, nakuwa zinagawanyika sehemu tatu katika sheria: Halali ya wazi, na haramu ya wazi, na mambo yenye kutatiza, hukumu yake haiko wazi upande wa uhalali na uharamu, watu wengi hawajui hukumu yake.
Atakayeacha mambo hayo yenye kutatiza kwake, dini yake itasalimika kwa kuwa mbali na kuingia katika haramu, na heshima yake itasalimika kutokana na maneno ya watu, kwa yale wanayoweza kumuaibisha kwa kuyafanya kwake haya yenye kutatiza. Na asiyeyaepuka yenye kutatiza atakuwa kaitumbukiza nafsi yake, ima katika haramu, au watu kumkosea heshima yake. Na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kapiga mfano ili abainishe hali ya mwenye kuyafanya mambo yenye kutatiza, nakuwa yeye ni sawa na mchunga mifugo, mwenye kuchunga karibu na ardhi ambayo kaihifadhi mwenye ardhi hiyo, inahofiwa mifugo yake kulisha katika mipaka hii kwa sababu ya ukaribu wake, na hivyo hivyo mwenye kufanya mambo yenye utata ndani yake, basi kwa kufanya hivyo anakuwa karibu na haramu na anahofiwa kutumbukia ndani yake. Na baada yake akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa katika kiwiliwili kuna kipande cha nyama (Nacho ni moyo) mwili hutengemaa kwa kutengemaa kwake, na huharibika kwa kuharibika kwake.
Mafunzo
Himizo la kuacha yenye kutatiza, ambayo hukumu yake haijabainika.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 20) (52).
صحيح مسلم (3/ 1219) (1599).
التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثا النووية (ص18).
شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص105).
فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للعباد (ص41).
فتح الباري لابن حجر (4/ 291).
شرح النووي على مسلم (11/ 28).
kutoka kwa Abdullahi bin Amry -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alishika Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- bega langu, na akasema: "Kuwa duniani kama msafiri au mpitanjia", Na alikuwa bin Omari akisema: Ukishinda mchana usisubiri asubuhi, na ukiamka asubuhi usisubiri jioni, na chukua fursa ya kuitumia vizuri afya yako kwa ajili ya maradhi yako, na uhai wako kwa ajili ya kifo chako.
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Ibn Omari Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, ameeleza kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimshika begani - nacho ni kiungo cha juu cha mkono na bega - akamwambia: Kuwa katika dunia hii kana kwamba wewe ni mgeni aliyekuja katika nchi ambapo hakuwa na makazi yake, na hakuna wakazi wa kumkaribisha wala familia tegemezi, wala mahusiano ambayo ni sababu ya hili, kuwa shupavu zaidi kuliko mgeni huyu ambaye ni mpita njia anayepita njiani kuelekea katika nchi yake. Kwa sababu mgeni anaweza kuishi katika nchi ya kigeni na akawa mkazi ndani yake, tofauti na msafiri anayetaka kwenda nchini kwake, haja yake huwa ni kupumzika ili apate wepesi na sio kukaa, na kuwa na hamu ya kuwasili katika nchi yake kama vile msafiri hahitaji zaidi ya yale yatakayomfikisha mwisho wa safari yake, halikadhalika muumini katika ulimwengu huu hahitaji zaidi ya yale yatakayomfikisha mahali pazuri.
Akazifanyia kazi bin Omari nasaha hizi na alikuwa akisema: Ukiamka usisubiri jioni, na ukishinda mpaka jioni usisubiri asubuhi, na ihesabu nafsi yako kuwa katika wafu walioko makaburini, na kwakuwa umri haukosi moja katika ya mawili, afya na maradhi; fanya haraka siku za afya yako kwa kufanya ibada kwa ajili ya maradhi yako; na tumia fursa ya matendo mema katika wakati wa afya kabla maradhi hayajakuzuia, na faidika na uhai wako katika dunia, kusanya ndani yake yale yatakayokunufaisha baada ya kifo chako.
Mafunzo
Mwalimu kuweka kiganja chake juu ya bega la mwanafunzi wakati wa kujifunza ni kwa ajili ya kujiliwaza, na kutoa angalizo.
Ni vizuri kuanza kwa nasaha na maelekezo kwa mtu ambaye hajaomba hivyo.
Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kupiga mifano hai yanye kutosheleza, kwa kauli yake: "Kuwa katika dunia kana kwamba ni mgeni au mpitanjia"
Tofauti ya watu katika safari yao ya kwenda Akhera; mpitanjia, hii ni daraja ya juu ya kuipa nyongo dunia kuliko daraja la mgeni.
Kumebainishwa ufupi wa mipango, na maandalizi ya kifo.
Hadithi haimaanishi kuacha riziki na kuharamisha ladha za dunia; lakini inamaanisha ni himizo la kuipa nyongo dunia, na kuihama.
Kwenda mbio katika matendo mema kabla hajashindwa mtu kuyafanya, na kifo au maradhi vikamzuia.
Fadhila za Abdallah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake, kiasi kwamba aliathirika kwa mawaidha kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Makazi ya waumini ni Pepo, muumini ni mgeni katika dunia, na ni msafiri kuelekea Akhera, asiufungamanishe moyo wake na kitu chochote katika mji wa ugenini, bali moyo wake umefungamana na nchi ambayo anarejea kwayo, na kukaa kwake katika dunia ni ili akidhi mahitaji yake na maandalizi yake kwa ajili ya kurejea katika nchi yake.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 89) (6416).
التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية، لإسماعيل الأنصاري (ص90).
شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص390).
فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للنووي وابن رجب (ص131).
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: " Msihusudiane, na wala msipandishiane bei, na wala msichukiane, na wala msitengane, na wala wasiuze baadhi yenu juu ya biashara ya wengine, na kuweni waja wa Mwenyezi Mungu ndugu muislamu ni ndugu wa muislamu, asimdhulumu, na wala asimsaliti, na wala asimdharau, ucha Mungu uko hapa" Na huku akiashiria katika kifua chake mara tatu "Yamtosha mtu kuwa ni shari kwake kwa kumdharau ndugu yake muislamu, kila muislamu kwa muislamu mwenzake ni haramu damu yake, na mali yake, na heshima yake".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alimuusia Mtume rehema na amani ziwe juu yake muislamu kwa ndugu yake muislamu kumtendea mazuri, na akabainisha baadhi ya yale yanayomlazimu katika wajibu na adabu kwao; na miongoni mwa hayo: Wasia wa kwanza: Msihusudiane kwa kutamani baadhi yenu neema za wengine ziwaondokee. Wa pili: Wala msipandishiane, kwa kuzidisha katika bidhaa hali yakuwa hana nia ya kununua; isipokuwa anataka kumnufaisha muuzaji, au kumdhuru mnunuzi. Ya tatu: Msichukiane; nako ni kutaka kuleta madhara, kitu ambacho ni kinyume na mapenzi; isipokuwa kuchukiana kutakapokuwa ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; hapo ni wajibu. Ya nne: Msitengane, nako ni kila mmoja miongoni mwenu kumpa mgongo na kisogo ndugu yake, na akampuuza na kumhama. Ya tano: Wasiuze baadhi yenu juu ya biashara ya wengine, kwa mtu kumwambia aliyenunua bidhaa: Nina bidhaa kama hiyo kwa bei nafuu kuliko hiyo, au nina bidhaa bora kuliko hiyo na kwa bei hiyo hiyo. Kisha akausia rehema na amani ziwe juu yake kwa usia wa ujumla, akasema: Na kuweni kama ndugu kwa kuyaacha yaliyotajwa katika makatazo, na kwa kujitolea mapenzi na huruma na upole na kusikilizana na kusaidizana katika mambo ya kheri, ikiwa ni pamoja na kusafisha mioyo na kunasihiana kwa kila hali. Na miongoni mwa mambo yanayojenga udugu huu: Asimdhulumu ndugu yake muislamu na wala asimfanyie uadui. Na wala asiache ndugu yake muislamu akadhulumiwa akamsaliti katika mahali ambapo anaweza kumtetea na akapata haki yake, na akamuondolea dhulma. Na asimdharau na akamuona duni na akamtazama kwa jicho la kumshusha thamani na kumkejeli; na hilo ni matokeo ya kiburi kilichopo ndani ya moyo. Kisha akabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mara tatu kuwa ucha Mungu uko moyoni, na atakayekuwa na ucha Mungu ndani ya moyo wake unaopelekea katika tabia njema, na kumuogopa Mwenyezi Mungu na kumchunga, basi hawezi kumdharau muislamu, na yamtosha kwake kuwa na mambo ya shari na tabia chafu kwa kumdharau ndugu yake muislamu; na hilo ni kwa sababu ya kiburi kilichopo moyoni mwake. Kisha akasisitiza rehema na amani ziwe juu yake hayo yaliyopita kuwa kila muislamu kwa muislamu mwenzake ni haramu: Damu yake: Kwa kumfanyia uadui akamuuwa, au chini ya hapo kama kumjeruhi au kumpiga na mfano wake, na vile vile mali yake: Kwa kuichukuwa pasina haki, na vile vile heshima yake: Kwa kumtukana yeye mwenyewe au ukoo wake.
Mafunzo
Amri ya kutekeleza jambo lolote linalopelekea udugu wa kiimani, na katazo la kufanya kinyume chake miongoni mwa kauli na vitendo.
Nguzo ya ucha Mungu ndani ya moyo ni kumtambua Mwenyezi Mungu, na kumuogopa na kumchunga, una ucha Mungu huu ndio unaozaa matendo mema.
Kupinda kwa wazi kunaonyesha udhaifu wa ucha Mungu wa moyo.
Katazo la kumuudhi muislamu kwa aina yoyote ile, kwa kauli au kitendo.
Si katika husuda muislamu kutamani awe kama mwenzake, bila kutamani neema hiyo iondoke kwa mwenzake, na hii huitwa kufurahia neema ya mwenzio (na kuitamani pia uipata); na hii inafaa, kwani inasaidia watu kushindana katika mambo ya kheri.
Mwanadamu katika tabia zake hapendi yeyote amzidi katika chochote miongoni mwa fadhila, ikiwa atapenda iondoke neema hiyo kwa mwenzake hiyo itakuwa ni husuda mbaya, na ikiwa atapenda kushindana basi hiyo inaitwa kufarahia neema kunako faa.
Si katika kuuza muislam juu ya biashara ya ndugu yake kwa kumuweka wazi mteja kuwa kadanganywa katika kununua tena uongo mbaya; bali hili ni katika sehemu ya nasaha, kwa sharti iwe matokeo yake ni kumnasihi ndugu yake mnunuzi, na si kumdhuru muuzaji, kwani matendo huhukumiwa kwa nia.
Si katika kuuza muislamu juu ya biashara ya ndugu yake ikiwa muuzaji na mnunuzi hawajakubaliana na wala kiwango cha thamani hakijapitishwa.
Si katika kuchukiana kuliko katazwa ndani ya hadithi: Kuchukia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, bali hilo ni wajibu, na ni katika misingi mizito ya imani.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 1986) (2564).
التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية، لإسماعيل الأنصاري (ص79).
شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص339).
فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، النووي وابن رجب (ص118).
الأحاديث الأربعون النووية وعليها الشرح الموجز المفيد، لعبد الله المحسن (ص67).
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema: Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mtazameni aliyeko chini yenu, na wala msimtazame aliyeko juu yenu, kwa kufanya hilo, hilo litakufanyeni msidharau neema za Allah mlizonazo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemuamrisha muislamu kumtazama katika mambo ya dunia katika nafasi na mali na cheo na mengineyo yule ambaye ana hali ya chini zaidi, na asimtazame katika mambo ya dunia yake yule aliyeko juu yake na bora zaidi kuliko yeye, kwa kumtazama aliyeko chini ni bora na kunastahiki zaidi kumfanya asidharau na kuzidogesha neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yake.
Mafunzo
Kutosheka ni miongoni mwa tabia tukufu za muumini, nayo ni katika alama za kuridhia makadirio ya Mwenyezi Mungu.
Amesema bin Jariri: Hii ni hadithi iliyokusanya aina nyingi za kheri; kwa sababu mtu anapoona mtu aliyefadhilishwa katika dunia basi hutamani apate mfano wake, na kuyadogesha aliyonayo katika neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na anapata tamaa ya kuongeza ili amfikie huyo au amkaribie, hili ndilo liliopo kwa watu wengi, na ama akimtazama katika mambo ya kidunia yule aliye chini yake katika yale yaliyodhihiri kwake katika neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu anazomzidi, akamshukuru na akanyenyekea, na akafanya kheri ndani yake.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 102) (6490).
صحيح مسلم (4/ 2275) (2963).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (7/ 261).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 534).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص316).
توضيح الأحكام من بلوغ المرام ، لعبد الله البسام (7/ 287).
منحة العلام شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 17).
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Neema mbili wamepoteza thamani yake watu wengi: Afya na wakati".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu neema mbili kubwa miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu kuwa wanapata hasara ndani yake watu wengi, kiasi kwamba wanazitumia mahali pasipostahiki; kwani mwanadamu zikikusanyika kwake neema ya afya na wakati, akazidiwa na uvivu wa kufanya ibada basi kapata hasara; na ndio hali ya watu wengi, na akiutumia muda wake na afya yake katika kumtii Mwenyezi Mungu basi atakuwa kapata faida; hii ni kwa sababu dunia ndio shamba la Akhera, na wakati hufuatiwa na shughuli, na afya hufuatiwa na maradhi, na lau kusingekuwa na chochote zaidi ya uzee basi ungetosha.
Mafunzo
Kumfananisha mtu mzima na mfanya biashara, na afya na muda kavifananisha na mtaji; atakayeutumia vizuri mtaji wake atapata faida, na atakayeupoteza basi atapata hasara na kujuta.
Amesema bin Khaazin: Neema ni kila anachoneemeka nacho mtu na anapata ladha kwacho, na udanganyifu, ni mtu kununua kitu kwa thamani kubwa, au kukiuza kwa thamani isiyolingana na kilichouzwa; atakayekuwa na afya katika mwili wake na akawa na wakati na hana la kumshughulisha, na akawa hakwenda mbio kuitumikia Akhera yake huyu ni sawa na aliyefanya biashara yenye udanganyifu.
Kuwa na pupa ya kufaidika na afya na wakati kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na Kutukuka, na kufanya kheri kabla ya kutoweka kwake.
Kushukuru neema za Mwenyezi Mungu kunakuwa kwa kuzitumia katika kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Amesema Kadhi Abubakari bin Al-Arabi: Kumepatikana tofauti kuwa ni ipi neema ya kwanza kwa mja, kukasemwa: Ni imani, na kukasemwa: Ni uhai, na kukasemwa: Ni afya, na ya kwanza ndio bora kwa sababu ndio neema ya kiujumla, na ama uhai na afya hizo ni neema za kidunia, na wala haziwezi kuwa neema halisia isipokuwa zitakapoambatana na imani, na hapo ndipo wanapohadaika watu wetu, yaani inapotea faida yao au inapungua, atakayeiendekeza nafsi yake yenye kuamrisha maovu, na yenye kudumu katika starehe, akaacha kuhifadhi mipaka ya Mwenyezi Mungu, na kudumu na ibada, basi huyu atakuwa kahadaika, na vile vile atakapokuwa hana la kumshughulisha, kwa sababu aliyeshughulishwa anaweza kuwa na udhuru tofauti na mwenye nafasi; basi huyu hana udhuru na hoja itasimama juu yake.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 88) (6412).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 131).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 65).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 180).
تحفة الأحوذي بشرح جامع الترمذي، للمباركفوري (6/ 485).
Imepokelewa kutoka kwa Jariri bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu kutazama ghafla, akaniamrisha nigeuze jicho langu.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Jariri bin Abdullah Mwenyezi Mungu amuwie radhi, alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mwanaume kumwangalia mwanamke wa kando ghafla bila kukusudia? Basi akamuamrisha rehema na amani ziwe juu yake kuwa aelekeze uso wake pembeni upande wa pili mara anapojua hilo, na hatokuwa na dhambi juu yake.
Mafunzo
Himizo la kuinamisha macho.
Tahadhari ya kutazama kwa muda katika yale yaliyoharamishwa kuyatazama jicho linapodondokea ghafla na pasina kukusudia.
Ndani ya hadithi kuna uharamu kwa kuwatazama wanawake, jambo ambalo waliishi nalo Maswahaba, kwa ushahidi wa kuwa Jariri radhi za Allah ziwe juu yake alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa endapo litaangukia jicho lake katika kumtazama mwanamke pasina kukusudia, je hukumu yake itakuwa sawa na aliyekusudia kutazama?.
Na pia inaonyesha namna sheria ilivyotilia maanani masilahi ya waja, kwa kuwaharamishia kuwatazama wanawake, kwakuwa swala hilo linaambatana na maovu ya dunia na Akhera.
Kurejea Maswahaba kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kumuuliza katika yale yanayowatatiza, na hivi ndivyo inavyotakiwa kwa watu wote kurejea kwa wanachuoni wao na kuwauliza katika yale yanayowatatiza.
Marejeo
صحيح مسلم (3/ 1699) (2159).
نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1117).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (3/ 145).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 362).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com