Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Nilimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu kutazama ghafla, akaniamrisha nigeuze jicho langu

عَنْ جَرِيرِ بْنِ عَبْدِ اللهِ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: سَأَلْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ نَظَرِ الْفُجَاءَةِ فَأَمَرَنِي أَنْ أَصْرِفَ بَصَرِي.
Imepokelewa kutoka kwa Jariri bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu kutazama ghafla, akaniamrisha nigeuze jicho langu.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Jariri bin Abdullah Mwenyezi Mungu amuwie radhi, alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mwanaume kumwangalia mwanamke wa kando ghafla bila kukusudia? Basi akamuamrisha rehema na amani ziwe juu yake kuwa aelekeze uso wake pembeni upande wa pili mara anapojua hilo, na hatokuwa na dhambi juu yake.

Mafunzo
  1. Himizo la kuinamisha macho.
  2. Tahadhari ya kutazama kwa muda katika yale yaliyoharamishwa kuyatazama jicho linapodondokea ghafla na pasina kukusudia.
  3. Ndani ya hadithi kuna uharamu kwa kuwatazama wanawake, jambo ambalo waliishi nalo Maswahaba, kwa ushahidi wa kuwa Jariri radhi za Allah ziwe juu yake alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa endapo litaangukia jicho lake katika kumtazama mwanamke pasina kukusudia, je hukumu yake itakuwa sawa na aliyekusudia kutazama?.
  4. Na pia inaonyesha namna sheria ilivyotilia maanani masilahi ya waja, kwa kuwaharamishia kuwatazama wanawake, kwakuwa swala hilo linaambatana na maovu ya dunia na Akhera.
  5. Kurejea Maswahaba kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kumuuliza katika yale yanayowatatiza, na hivi ndivyo inavyotakiwa kwa watu wote kurejea kwa wanachuoni wao na kuwauliza katika yale yanayowatatiza.
Marejeo

صحيح مسلم (3/ 1699) (2159). نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1117). بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (3/ 145). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 362).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Kuzitakasa Nafsi.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com