Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema: Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mtazameni aliyeko chini yenu, na wala msimtazame aliyeko juu yenu, kwa kufanya hilo, hilo litakufanyeni msidharau neema za Allah mlizonazo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemuamrisha muislamu kumtazama katika mambo ya dunia katika nafasi na mali na cheo na mengineyo yule ambaye ana hali ya chini zaidi, na asimtazame katika mambo ya dunia yake yule aliyeko juu yake na bora zaidi kuliko yeye, kwa kumtazama aliyeko chini ni bora na kunastahiki zaidi kumfanya asidharau na kuzidogesha neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yake.
Mafunzo
Kutosheka ni miongoni mwa tabia tukufu za muumini, nayo ni katika alama za kuridhia makadirio ya Mwenyezi Mungu.
Amesema bin Jariri: Hii ni hadithi iliyokusanya aina nyingi za kheri; kwa sababu mtu anapoona mtu aliyefadhilishwa katika dunia basi hutamani apate mfano wake, na kuyadogesha aliyonayo katika neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na anapata tamaa ya kuongeza ili amfikie huyo au amkaribie, hili ndilo liliopo kwa watu wengi, na ama akimtazama katika mambo ya kidunia yule aliye chini yake katika yale yaliyodhihiri kwake katika neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu anazomzidi, akamshukuru na akanyenyekea, na akafanya kheri ndani yake.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 102) (6490).
صحيح مسلم (4/ 2275) (2963).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (7/ 261).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 534).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص316).
توضيح الأحكام من بلوغ المرام ، لعبد الله البسام (7/ 287).
منحة العلام شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 17).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com