Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Toba

Hadithi 8

Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kupi kunusurika? Akasema: "Shika ulimi wako, na ikutoshe nyumba yako, na lia kwa ajili ya makosa yako

عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ رضي الله عنه قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ مَا النَّجَاةُ؟ قَالَ: «امْلِكْ عَلَيْكَ لِسَانَكَ، وَلْيَسَعْكَ بَيْتُكَ، وَابْكِ عَلَى خَطِيئَتِكَ».
Kutoka kwa Ukba bin Aamir Al-Juhaniy -radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kupi kunusurika? Akasema: "Shika ulimi wako, na ikutoshe nyumba yako, na lia kwa ajili ya makosa yako".
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Ukba bin Aamiri alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu sababu za muumini kuokoka katika dunia na Akhera? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Shikamana na mambo matatu: La kwanza: Hifadhi ulimi wako katika yale yasiyokuwa na kheri ndani yake, na kuzungumza kila shari, na usitamke ila la kheri. La pili: Baki nyumbani kwako ili umuabudu Mwenyezi Mungu katika nyakati za faragha, na ujishughulishe na kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ibada, na jitenge nyumbani kwako na fitina. La tatu: Lia na ujute na utubie kwa yale uliyoyatenda katika madhambi.

Mafunzo
  1. Pupa ya Maswahaba katika kujua njia za kusalimika.
  2. Kumebainishwa sababu za kusalimika katika Dunia na Akhera.
  3. Himizo la mtu kushughulika na nafsi yake anaposhindwa kumnufaisha mtu mwingine, au akahofia madhara juu ya dini yake na nafsi yake endapo atachanganyikana na watu.
  4. Hapa kuna ishara ya kuipa kipaumbele nyumba, na hasa hasa wakati wa fitina, kwani ni katika nyenzo za kuihifadhi dini.
Marejeo

سنن الترمذي (4/ 208) (2406). مسند أحمد (28/ 654) (17452). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (3/ 15). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1039). مرقاة المفاتيح، لعلي القاري (7/ 3039).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyoosha mkono wake wakati wa usiku ili amsamehe mkosefu wa mchana, na ananyoosha mkono wake wakati wa mchana ili amsamehe mkosaji wa usiku, mpaka jua litakapochomoza kutoka magharibi yake

عَنْ أَبِي مُوسَى رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ اللهَ عَزَّ وَجَلَّ يَبْسُطُ يَدَهُ بِاللَّيْلِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ النَّهَارِ، وَيَبْسُطُ يَدَهُ بِالنَّهَارِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ اللَّيْلِ، حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِهَا».
Na kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyoosha mkono wake wakati wa usiku ili amsamehe mkosefu wa mchana, na ananyoosha mkono wake wakati wa mchana ili amsamehe mkosaji wa usiku, mpaka jua litakapochomoza kutoka magharibi yake."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anakubali toba kutoka kwa waja wake, mja akitenda dhambi wakati wa mchana na akatubia usiku Mwenyezi Mungu hukubali toba yake, na akitenda dhambi usiku na akatubia mchana basi Mwenyezi Mungu hukubali toba yake, Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyoosha mkono wake kwa kuifurahia toba, na kuikubali, na mlango wa toba unabaki wazi mpaka jua lichomoze kutoka magharibi, likiashiria mwisho wa dunia, basi likichomoza mlango wa toba utafungwa.

Mafunzo
  1. Kukubaliwa toba kunaendelea maadamu mlango wake uko wazi, na mlango wake utafungwa wakati jua linapochomoza kutoka magharibi, na kwamba mtu atubu kabla ya msukosuko wa kifo, ambao ni roho kufika kooni.
  2. Kutokata tamaa kwa sababu ya dhambi, kwani msamaha na rehema za Mwenyezi Mungu ni mpana, na mlango wa toba uko wazi.
  3. Masharti ya kutubia: La kwanza: kuacha dhambi, la pili: kujuta kwa kuitenda, na la tatu: kuazimia kutorejea tena, ikiwa ni katika haki za Mwenyezi Mungu, na ikiwa inahusiana na haki za waja, basi kwa ajili ya kupokelewa toba inatakiwa kuwa haki hiyo apewe mmiliki wake au mwenye haki amsamehe.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2113) (2759). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 35). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 103). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 55).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila mwanadamu ni mkosefu, na mbora wa wakosefu ni wale wenye kutubia

عن أنس بن مالك رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «كلُّ بني آدم خَطَّاءٌ، وخيرُ الخَطَّائِينَ التوابون».
Kutoka kwa Anas bin Malik- Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Allah- Rehma na amani ziwe juu yake- "Kila mwanadamu ni mkosefu, na mbora wa wakosefu ni wale wenye kutubia".
Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Ahmad - Imepokelewa na AddaaramyDarajaNi nzuri
Maelezo

Haepukani mwanadamu na kukosea, kwa jinsi alivyoumbwa kutokana na udhaifu, na kutokumtii msimamizi wake katika kutekeleza yale aliyomtaka ayafanye, na kuacha yale aliyomkataza, lakini yeye Mtukufu amefungua mlango wa toba kwa waja wake, na akaeleza kuwa mbora wa wakosefu ni wale wenye kukithirisha toba.

Mafunzo
  1. Katika mambo ya mwanadamu ni kukosea na kuingia katika dhambi. La msingi kwa muumini atakapojiiingiza katika maasi afanye haraka kuleta toba.
Marejeo

سنن الترمذي، محمد بن عيسى الترمذي، تحقيق وتعليق: أحمد محمد شاكر ومحمد فؤاد عبد الباقي وإبراهيم عطوة عوض، شركة مكتبة ومطبعة مصطفى البابي الحلبي، مصر الطبعة الثانية، 1395هـ - 1975 م. سنن ابن ماجه: ابن ماجه أبو عبد الله محمد بن يزيد القزويني، تحقيق: محمد فؤاد عبد الباقي، دار إحياء الكتب العربية، فيصل عيسى البابي الحلبي. مسند الإمام أحمد بن حنبل المحقق: شعيب الأرنؤوط - عادل مرشد، وآخرون إشراف: د عبد الله بن عبد المحسن التركي، مؤسسة الرسالة الطبعة الأولى، 1421 هـ - 2001 م. سنن الدارمي، عبد الله بن عبد الرحمن الدارمي، دار المغني للنشر والتوزيع، المملكة العربية السعودية، الطبعة: الأولى، 1412 هـ - 2000 م. مشكاة المصابيح، محمد بن عبد الله الخطيب التبريزي، المحقق: محمد ناصر الدين الألباني، المكتب الإسلامي، بيروت، الطبعة الثالثة، 1985. منحة العلام في شرح بلوغ المرام:تأليف عبد الله الفوزان، طبعة دار ابن الجوزي، الطبعة الأولى 1428هـ. توضيح الأحكام شرح بلوغ المرام: تأليف عبد الله البسام، مكتبة الأسدي، مكة المكرمة، الطبعة الخامِسَة، 1423 هـ - 2003 م. فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام للشيخ ابن عثيمين، المكتبة الإسلامية القاهرة، تحقيق صبحي رمضان وأم إسراء بيومي، الطبعة الأولى 1427هـ. - سبل السلام، محمد بن إسماعيل الصنعاني، دار الحديث، بدون طبعة وبدون تاريخ. - فيض القدير شرح الجامع الصغير، المؤلف: عبد الرؤوف المناوي القاهري، المكتبة التجارية الكبرى، مصر، الطبعة الأولى، 1356هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

“Ewe mwanadam, maadamu unaniomba na kunitumainia, nitakusamehe uliyo nayo wala sitojali

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ مَا دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ عَلَى مَا كَانَ فِيكَ وَلاَ أُبَالِي، يَا ابْنَ آدَمَ لَوْ بَلَغَتْ ذُنُوبُكَ عَنَانَ السَّمَاءِ ثُمَّ اسْتَغْفَرْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ، وَلاَ أُبَالِي، يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ لَوْ أَتَيْتَنِي بِقُرَابِ الأَرْضِ خَطَايَا ثُمَّ لَقِيتَنِي لاَ تُشْرِكُ بِي شَيْئًا لأَتَيْتُكَ بِقُرَابِهَا مَغْفِرَةً».
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: “Amesema Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka: “Ewe mwanadam, maadamu unaniomba na kunitumainia, nitakusamehe uliyo nayo wala sitojali Ewe mwanadam lau madhambi yako yangefika mawinguni kisha ukaniomba msamaha ningekusamehe wala sijali Ewe mwanadam, lau ungenijia na thamani ya dhambi za dunia, kisha ukakutana nami bila kunishirikisha na chochote, ningekuletea msamaha ujazo sawa na ardhi".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Hadithil Qudsi (tukufu): Ewe mwanadam, madam unaniomba na kutaraji rehema yangu, wala hujakata tamaa; Nitayasitiri madhambi yako na kuyafuta, bila kujali, hata kama madhambi na maasi haya ni katika madhambi makubwa. Ewe mwanadam! Lau madhambi yako yangekuwa mengi sana kiasi cha kuijaza nafasi ya baina ya mbingu na ardhi mpaka kiasi cha kufikia upenyo wake na kufunika pembe zake, kisha ukaniomba msamaha, basi ningekufutia na kukusamehe madhambi yote, bila kujali wingi wake. Ewe mwanadam: Lau ungenijia mimi baada ya kufa ukiwa na madhambi na maasi ujazo wa ardhi, na ukafa haliyakuwa unanipwekesha hukunishirikisha na chochote; Ningekutana na madhambi na maasi haya nikiijaza ardhi kwa msamaha; kwa sababu mimi ni mwingi wa msamaha, na ninasamehe madhambi yote isipokuwa shirki.

Mafunzo
  1. Upana wa huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na msamaha wake na fadhila zake.
  2. Ubora wa tauhidi, nakuwa Mwenyezi Mungu anawasamehe madhambi pamoja na maasi wenye kumpwekesha.
  3. Hatari ya ushirikina nakuwa Mwenyezi Mungu hawasamehe washirikina.
  4. Amesema bin Rajab: Hadithi hii inakusanya sababu tatu za kusamehewa dhambi: Ya kwanza: Kuomba dua pamoja na matumaini, ya pili: Kutaka msamaha na kuomba toba, ya tatu: Kufa katika tauhidi.
  5. Hadithi hii ni katika yale anayoyasimulia Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Mola wake Mlezi, na inaitwa Hadithil Qudsi (tukufu) Hadithi ya kiuungu, na maneno yake na maana yake ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu ila hayana sifa za Qur'ani ambazo inasifika nazo kuliko kitu kingine chochote, kama vile kumuabudu Mwenyezi Mungu kupitia kisomo chake, na kuwa na twahara kwa ajili yake, na kutoa changamoto na miujiza na kadhalika.
  6. Dhambi zina aina tatu: Ya kwanza: Kumshirikisha Mwenyezi Mungu; Na dhambi hili haisamehe Mwenyezi Mungu Mtukufu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu amemharamishia Pepo". Ya pili: Ni mja kujidhulumu mwenyewe katika yale yaliyo kati yake na Mola wake Mlezi, kama madhambi na maasi; Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu huyasamehe hayo, na kuyaachilia mbali akitaka. Ya tatu: Ni madhambi ambayo Mwenyezi Mungu haachi chochote katika hayo, nayo ni dhulma ya waja wao kwa wao, hivyo ni lazima kulipiza kisasi.
Marejeo

سنن الترمذي (5/ 509) (3540). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية، لإسماعيل الأنصاري (ص93). شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص397).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Liepukeni chafu hili alilolikataza Mwenyezi Mungu, atakayetumbukia katika hilo basi ajifiche kwa stara ya Mwenyezi Mungu na atubie kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu atakayetufungulia ukurasa wake tutamsimamishia kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَامَ بَعْدَ أَنْ رَجَمَ الْأَسْلَمِيَّ فَقَالَ: «اجْتَنِبُوا ‌هَذِهِ ‌الْقَاذُورَةَ الَّتِي نَهَى اللَّهُ عَنْهَا فَمَنْ أَلَمَّ فَلْيَسْتَتِرْ بِسِتْرِ اللَّهِ وَلْيُتُبْ إِلَى اللَّهِ، فَإِنَّهُ مَنْ يُبْدِ لْنَا صَفْحَتَهُ نُقِمْ عَلَيْهِ كِتَابَ اللَّهِ عز وجل».
Kutoka kwa Abdallah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisimama baada ya kumuadhibu kwa kumpiga mawe Al-Aslami, akasema: "Liepukeni chafu hili alilolikataza Mwenyezi Mungu, atakayetumbukia katika hilo basi ajifiche kwa stara ya Mwenyezi Mungu na atubie kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu atakayetufungulia ukurasa wake tutamsimamishia kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu".
Imepokelewa na Hakim na BayhaqyDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Omari radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisimama baada ya kumpopoa mawe Maaizi bin Malik Al-Aslami radhi za Allah ziwe juu yake, kwa adhabu ya zinaa, akawahutubia watu, na akasema: Jiepusheni na chafu hili na yote yanayotia kinyaa na machafu miongoni mwa maasi aliyoyakataza Mwenyezi Mungu, na atakayeangukia na akafanya chochote basi ni wajibu kwake mambo mawili: La kwanza: Ajifiche katika mahali alipomsitiri Mwenyezi Mungu, na asimueleze yeyote kuhusu maasi yake. La pili: Afanye haraka kutubia kwa Mwenyezi Mungu na wala asiendelee, na yatakayeonekana wazi maasi yake basi tutamsimamishia sheria iliyotajwa ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mwenyezi kwa maasi hayo.

Mafunzo
  1. Himizo la mja mkosefu kujisitiri, na atubie dhambi kwa yale yaliyo baina yake na Mola wake Mlezi.
  2. Mipaka ya Mwenyezi Mungu inapomfikia kiongozi mkuu ni lazima atekeleze adhabu hiyo.
  3. Ulazima wa kuyaepuka maasi, na kutubia dhidi yake.
Marejeo

المستدرك على الصحيحين للحاكم (4/ 272) (7615). السنن الكبرى للبيهقي (8/ 572). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (8/ 435). فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (5/ 370). توضِيحُ الأحكَامِ مِن بُلوُغ المَرَام، للبسام (6/ 249). شرح الزرقاني على موطأ الإمام مالك (4/ 235).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakuna mtu yeyote atakayetenda dhambi, kisha akasimama akajitwaharisha, kisha akaswali, kisha akamuomba Allah msamaha, isipokuwa Mwenyezi Mungu humsamehe

‌عن عَلِيٍّ قَالَ: إِنِّي كُنْتُ رَجُلًا إِذَا سَمِعْتُ مِنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَدِيثًا نَفَعَنِي اللهُ مِنْهُ بِمَا شَاءَ أَنْ يَنْفَعَنِي بِهِ، وَإِذَا حَدَّثَنِي رَجُلٌ مِنْ أَصْحَابِهِ اسْتَحْلَفْتُهُ، فَإِذَا حَلَفَ لِي صَدَّقْتُهُ، وَإِنَّهُ حَدَّثَنِي ‌أَبُو بَكْرٍ، وَصَدَقَ أَبُو بَكْرٍ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «مَا مِنْ رَجُلٍ يُذْنِبُ ذَنْبًا، ثُمَّ يَقُومُ فَيَتَطَهَّرُ، ثُمَّ يُصَلِّي، ثُمَّ يَسْتَغْفِرُ اللهَ، إِلَّا غَفَرَ اللهُ لَهُ»، ثُمَّ قَرَأَ هَذِهِ الْآيَةَ: {وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنْفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ} [آل عمران: 135].
Kutoka kwa Ally amesema: Hakika mimi nilikuwa ni mtu kila nikisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hadithi Mwenyezi Mungu ananinufaisha kwa hadithi hiyo kwa kiasi alichotaka kuninufaisha, na akinihadithia yeyote katika Masahaba zake ninamuapisha, akiniapia ninamuamini, na siku moja alinihadithia Abubakari, na Abubakari akasema ukweli, akasema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakuna mtu yeyote atakayetenda dhambi, kisha akasimama akajitwaharisha, kisha akaswali, kisha akamuomba Allah msamaha, isipokuwa Mwenyezi Mungu humsamehe", Kisha akasoma aya hii: "Na wale ambao wakifanya machafu au wakizidhulumu nafsi zao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakaomba msamaha kutokana na madhambi yao" [Al-Imran: 135].
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuna mja yeyote atakayetenda dhambi, akatawadha vizuri, kisha akasimama na akaswali rakaa mbili kwa nia ya kuomba toba kutokana na dhambi lake hili, kisha akamuomba Allah msamaha, isipokuwa Mwenyezi Mungu humsamehe. Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasoma kauli yake Mtukufu: "Na wale ambao wakitenda dhambi kubwa au wakizidhulumu nafsi zao kwa kutenda dhambi chini ya hizo, wanaikumbuka ahadi ya Mwenyezi Mungu ya malipo mema kwa wanaomtii na malipo mabaya kwa wanaomuasi na wanaelekea kwa Mola wao hali ya kutubia wakawa wanamuomba Awasamehe madhambi yao na wakawa wana yakini kwamba hapana anayesamehe madhambi isipokuwa Mwenyezi Mungu. Na wao kwa sababu hiyo hawaendelei kwenye maasi, na wao wanajua kwamba wakitubia Mwenyezi Mungu Atawakubalia toba yao". [Surat Al-Imran: 135].

Mafunzo
  1. Himizo la kuswali kisha kuomba msamaha baada ya kutenda dhambi.
  2. Upana wa msamaha wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kukubali kwake toba na msamaha.
Marejeo

سنن أبي داود (2/ 630) (1521)، سنن الترمذي (1/ 431) (406)، السنن الكبرى للنسائي (10/ 51) (11012)، سنن ابن ماجه (2/ 403) (1395)، مسند أحمد (1/ 179) (2)، فتح الباري لابن حجر (11/ 99)، النهاية في غريب الحديث والأثر (ص 674).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu na Mtukufu, halali, na wala haimstahikii kulala

عَنْ أَبِي مُوسَى رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَامَ فِينَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِخَمْسِ كَلِمَاتٍ، فَقَالَ: «إِنَّ اللهَ عَزَّ وَجَلَّ لَا يَنَامُ، وَلَا يَنْبَغِي لَهُ أَنْ يَنَامَ، يَخْفِضُ القِسْطَ وَيَرْفَعُهُ، يُرْفَعُ إِلَيْهِ عَمَلُ اللَّيْلِ قَبْلَ عَمَلِ النَّهَارِ، وَعَمَلُ النَّهَارِ قَبْلَ عَمَلِ اللَّيْلِ، حِجَابُهُ النُّورُ -وَفِي رِوَايَةٍ: النَّارُ- لَوْ كَشَفَهُ لَأَحْرَقَتْ سُبُحَاتُ وَجْهِهِ مَا انْتَهَى إِلَيْهِ بَصَرُهُ مِنْ خَلْقِهِ».
Kutoka kwa Abuu Mussa radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alisimama kwetu Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa maneno matano, akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu na Mtukufu, halali, na wala haimstahikii kulala, hushusha mizani ya uadilifu na huinyanyua, yanapandishwa kwake matendo ya usiku kabla ya matendo ya mchana, na matendo ya mchana kabla ya matendo ya usiku, pazia lake ni nuru, -na katika riwaya nyingine-: Lau kama angeliondoa, basi utukufu wa uso wake ungeunguza viumbe vyake mpaka pale ambapo macho yake yanafikia."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alisimama Mtume rehema na amani ziwe juu yake akihutubia kwa Maswahaba zake kwa sentensi tano kamilifu, nazo ni: Ya kwanza: Kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka halali. Ya pili: Haiwezekani katika haki yake kulala; kulingana na ukamilifu wa usimamizi wake na uhai wake. Ya tatu: Ya kwamba Yeye Mtukufu anashusha mizani na kuinyanyua kulingana na vile vinavyopimwa miongoni mwa matendo ya waja yanayopanda kwake juu, na zinapimwa riziki zao zinazoshuka katika Ardhi, riziki ambayo ndiyo sehemu na fungu la kila kiumbe huishusha Yeye Mtukufu na kumfanya awe masikini, na huipandisha na kumfanya awe tajiri. Ya nne: Hupandishwa kwake waliyoyafanya waja usiku kabla ya mchana unaofuata baada yake, na amali zao za mchana kabla ya amali za usiku unaofuata baada yake; Malaika wanaohifadhi matendo ya waja hupanda na matendo ya usiku baada ya kumalizika kwake katika mwanzo wa mchana, na wanapanda na amali za mchana baada ya kumalizika kwake katika mwanzo wa usiku. Ya tano: Pazia lake Mtukufu linalozuia kumuona ni nuru au moto, laiti angelifunua basi mwangaza wa uso wake ungeunguza kila kitu mpaka pale linapoishia jicho lake katika viumbe vyake; mwangaza wa uso wake ni nuru yake na utukufu wake na mng'ao wake. Na makadirio: Nikuwa, lau angeliondoa na kukifunua kinachozuia kumuona ambacho ni pazia, na akajitokeza wazi nuru ya uso wake ingeliunguza kila kitu mpaka linapoishia jicho lake katika viumbe vyake; navyo ni viumbe vyote; kwa sababu jicho lake Aliyetakasika na kutukuka limezingira viumbe vyote.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa kutowezekana kulala kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwakuwa hilo ni katika mapungufu, na yeye ametakasika na hayo.
  2. Mwenyezi Mungu Mtukufu anamtukuza amtakaye na anamdhalilisha amtakaye, na anamuongoza amtakaye na anampoteza amtakaye katika waja wake.
  3. Matendo hunyanyuliwa kwa Mwenyezi Mungu kila mchana na usiku, na katika hilo kuna himizo kwa waja wamchunge Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka katika usiku wao na mchana wao.
  4. Hadithi inaonyesha uadilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na uzuri wa upangiliaji wake wa mambo ya viumbe wake, na hakuna shaka kuwa hii ni katika sifa za ukamilifu wake Aliyetakasika na kuwa juu.
  5. Kumethibitishwa pazia lake Aliyetakasika na kutukuka, nayo ni nuru inayokinga baina yake na baina ya viumbe wake, na lau isingekuwa hiyo wanageliungua.
  6. Amesema Aajurri: Hakika watu wa haki humsifu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kile alichojisifu mwenye Mtukufu, na kwa kile alichomsifu nacho Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, na kwa kile walichomsifia Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, na huu ndio msimamo wa wanachuoni katika wale walioamua kufuata sheria na hawakuzusha. Mwisho wa kunukuu. Watu wa sunna (wanaofuata mafundisho ya Mtume) wanamthibitishia Mwenyezi Mungu kile alichojithibitishia yeye mwenyewe katika majina na sifa, pasina kupotosha wala kukanusha wala kuuliza namna yake wala kupiga mfano, na wanamkanushia Mwenyezi Mungu yale aliyoyakanusha kwake, na wananyamaza kwa yale ambayo hayakukanushwa wala kuthibitishwa, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakuna kitu kama mfano wake, na Yeye ni msikivu mwenye kuona".
  7. Nuru ambayo ndiyo sifa yake Aliyetakasika na kutukuka si nuru ambayo amejikinga nayo, nuru aliyojikinga nayo imeumbwa, nuru ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni nuru inayoendana naye Yeye na dhati yake, hakuna kitu kama mfano wake, na alichokiona Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakikuwa kingine zaidi ya pazia linalokuwa kati ya Mwenyezi Mungu na waja wake.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 161) (179). شرح المرقاة (1/128). فتح المنعم (1/581). البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (5/ 82).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Nipeni ahadi ya utiifu ya kuwa msimshirikishe Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na wala msiibe, na wala msizini

عَنْ عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، وَكَانَ شَهِدَ بَدْرًا، وَهُوَ أَحَدُ النُّقَبَاءِ لَيْلَةَ العَقَبَةِ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ، وَحَوْلَهُ عِصَابَةٌ مِنْ أَصْحَابِهِ: «بَايِعُونِي عَلَى أَلَّا تُشْرِكُوا بِاللَّهِ شَيْئًا، وَلاَ تَسْرِقُوا، وَلاَ تَزْنُوا، وَلاَ تَقْتُلُوا أَوْلاَدَكُمْ، وَلاَ تَأْتُوا بِبُهْتَانٍ تَفْتَرُونَهُ بَيْنَ أَيْدِيكُمْ وَأَرْجُلِكُمْ، وَلاَ تَعْصُوا فِي مَعْرُوفٍ، فَمَنْ وَفَى مِنْكُمْ فَأَجْرُهُ عَلَى اللَّهِ، وَمَنْ أَصَابَ مِنْ ذَلِكَ شَيْئًا فَعُوقِبَ فِي الدُّنْيَا فَهُوَ كَفَّارَةٌ لَهُ، وَمَنْ أَصَابَ مِنْ ذَلِكَ شَيْئًا ثُمَّ سَتَرَهُ اللَّهُ فَهُوَ إِلَى اللَّهِ، إِنْ شَاءَ عَفَا عَنْهُ وَإِنْ شَاءَ عَاقَبَهُ» فَبَايَعْنَاهُ عَلَى ذَلِكَ.
Kutoka kwa Ubada bin Swamiti radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa miongoni mwa walioshuhudia vita vya Badri, naye alikuwa ni mmoja wa vigogo katika usiku wa Aqaba: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema na pembezoni mwake kukiwa na jopo la Maswahaba zake: "Nipeni ahadi ya utiifu ya kuwa msimshirikishe Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na wala msiibe, na wala msizini, na wala msiwauwe watoto wenu, na wala msilete uzushi mtakouzua kwa mikono yenu na miguu yenu, na wala msiasi katika wema, basi atakayeyatimiza hayo miongoni mwenu basi malipo yake yatakuwa juu ya Mwenyezi Mungu, na atakayetenda lolote katika hayo akaadhibiwa katika dunia basi hiyo ndiyo kafara kwake, na atakayetenda lolote katika hayo kisha Mwenyezi Mungu akamsitiri basi hilo litabakia kwa Mwenyezi Mungu akitaka atamsamehe na akitaka atamuadhibu" Tukampa ahadi ya utiifu juu ya hayo.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Ubada bin Swamiti radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa ni miongoni mwa walioshuhudia vita vya Bardi kuu, naye akiwa kiongozi wa watu wake waliokuja kutoa mkono wa ahadi ya uaminifu kwa ajili ya kumnusuru Mtume rehema na amani ziwe juu yake usiku wa Aqaba ambayo iko Mina, wakati Mtume akiwa Makka kabla ya kuhama kwake kwenda Madina, ni kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa kakaa na Maswahaba zake akawataka wamuahidi juu ya mambo haya: La kwanza: Wasishirikishe katika ibada za Mwenyezi Mungu kitu chochote hata kikiwa kidogo. La pili: Wasiibe. La tatu: Wasifanye uchafu wa zinaa. La nne: Wasiwauwe watoto wao; wa kiume kwa kuhofia ufakiri na umasikini au watoto wa kike kwa kuhofia fedheha. La tano: Wasilete uongo wataoutengeneza baina ya mikono yao na miguu yao, kwa sababu matendo mengi hutokea kupitia hivi viwili hata kama viungo vingine vitashiriki. La sita: Wasimuasi Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika jambo jema. Atakayethubutu miongoni mwao katika ahadi na akashikamana nayo basi malipo yake yako kwa Mwenyezi Mungu, na atakayefanya lolote miongoni mwa hayo yaliyotajwa -kasoro ushirikina- akaadhibiwa katika dunia kwa kusimamishiwa adhabu juu yake basi hilo ndio kafara yake, na kwa hilo dhambi lake litaondoka, na atakayefanya lolote miongoni mwa hayo kisha Mwenyezi Mungu akamsitiri basi huyu jambo lake liko kwa Mwenyezi Mungu; akitaka atamsamehe na akitaka atamuadhibu, wote waliokuwepo wakampa ahadi ya utiifu juu ya hayo.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa mambo yaliyoambatana na ahadi ya Aqaba ya kwanza huko Makka kabla hawajafaradhishiwa Jihadi.
  2. Amesema As-Sanadi: Kauli yake: "Katika wema": Haifichikani kuwa amri zake zote ni wema na haifikiriki kuwa na kinyume chake, kauli yake: "katika wema" hii ilikuwa ni kwa ajili ya kutanabahisha sababu ya kutii na kwamba hakuna kumtii kiumbe katika jambo lisilokuwa jema, na kwamba ni sharti katika utii kuwe na wema katika ahadi, na si utii wa moja kwa moja.
  3. Amesema Muhammadi bin Suleiman Attaimi na wengineo: Ametaja swala la mauaji ya watoto pekee; kwa sababu ni mauaji na ni kukata ukoo, hivyo kutilia umuhimu katazo hilo kunakuwa na mkazo zaidi, na ni kwa sababu hilo lilikuwa limezagaa sana kwao, jambalo ni kuwazika watoto wa kike na kuwauwa watoto wa kiume kwa kuhofia umasikini, au kawataja maalumu; ili wasijitetee kwa hilo.
  4. Amesema Nawawi: Ujumla wa hadithi hii umeondolewa kwa kauli yake Mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa", Mwenye kuritadi anapouawa kwa sababu ya kutoka katika dini kuuawa hakuwi kafara kwake.
  5. Amesema Al-Kadhi Iyadhi: Wamesema wanachuoni wengi kuwa adhabu za kisheria ni kafara.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 12) (18). صحيح مسلم (3/ 1333) (1709). إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (1/ 99). عمدة القاري شرح صحيح البخاري (24/ 277).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com