Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Liepukeni chafu hili alilolikataza Mwenyezi Mungu, atakayetumbukia katika hilo basi ajifiche kwa stara ya Mwenyezi Mungu na atubie kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu atakayetufungulia ukurasa wake tutamsimamishia kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَامَ بَعْدَ أَنْ رَجَمَ الْأَسْلَمِيَّ فَقَالَ: «اجْتَنِبُوا ‌هَذِهِ ‌الْقَاذُورَةَ الَّتِي نَهَى اللَّهُ عَنْهَا فَمَنْ أَلَمَّ فَلْيَسْتَتِرْ بِسِتْرِ اللَّهِ وَلْيُتُبْ إِلَى اللَّهِ، فَإِنَّهُ مَنْ يُبْدِ لْنَا صَفْحَتَهُ نُقِمْ عَلَيْهِ كِتَابَ اللَّهِ عز وجل».
Kutoka kwa Abdallah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisimama baada ya kumuadhibu kwa kumpiga mawe Al-Aslami, akasema: "Liepukeni chafu hili alilolikataza Mwenyezi Mungu, atakayetumbukia katika hilo basi ajifiche kwa stara ya Mwenyezi Mungu na atubie kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu atakayetufungulia ukurasa wake tutamsimamishia kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu".
Imepokelewa na Hakim na BayhaqyDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Omari radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisimama baada ya kumpopoa mawe Maaizi bin Malik Al-Aslami radhi za Allah ziwe juu yake, kwa adhabu ya zinaa, akawahutubia watu, na akasema: Jiepusheni na chafu hili na yote yanayotia kinyaa na machafu miongoni mwa maasi aliyoyakataza Mwenyezi Mungu, na atakayeangukia na akafanya chochote basi ni wajibu kwake mambo mawili: La kwanza: Ajifiche katika mahali alipomsitiri Mwenyezi Mungu, na asimueleze yeyote kuhusu maasi yake. La pili: Afanye haraka kutubia kwa Mwenyezi Mungu na wala asiendelee, na yatakayeonekana wazi maasi yake basi tutamsimamishia sheria iliyotajwa ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mwenyezi kwa maasi hayo.

Mafunzo
  1. Himizo la mja mkosefu kujisitiri, na atubie dhambi kwa yale yaliyo baina yake na Mola wake Mlezi.
  2. Mipaka ya Mwenyezi Mungu inapomfikia kiongozi mkuu ni lazima atekeleze adhabu hiyo.
  3. Ulazima wa kuyaepuka maasi, na kutubia dhidi yake.
Marejeo

المستدرك على الصحيحين للحاكم (4/ 272) (7615). السنن الكبرى للبيهقي (8/ 572). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (8/ 435). فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (5/ 370). توضِيحُ الأحكَامِ مِن بُلوُغ المَرَام، للبسام (6/ 249). شرح الزرقاني على موطأ الإمام مالك (4/ 235).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Toba

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com