Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyoosha mkono wake wakati wa usiku ili amsamehe mkosefu wa mchana, na ananyoosha mkono wake wakati wa mchana ili amsamehe mkosaji wa usiku, mpaka jua litakapochomoza kutoka magharibi yake

عَنْ أَبِي مُوسَى رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ اللهَ عَزَّ وَجَلَّ يَبْسُطُ يَدَهُ بِاللَّيْلِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ النَّهَارِ، وَيَبْسُطُ يَدَهُ بِالنَّهَارِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ اللَّيْلِ، حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِهَا».
Na kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyoosha mkono wake wakati wa usiku ili amsamehe mkosefu wa mchana, na ananyoosha mkono wake wakati wa mchana ili amsamehe mkosaji wa usiku, mpaka jua litakapochomoza kutoka magharibi yake."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anakubali toba kutoka kwa waja wake, mja akitenda dhambi wakati wa mchana na akatubia usiku Mwenyezi Mungu hukubali toba yake, na akitenda dhambi usiku na akatubia mchana basi Mwenyezi Mungu hukubali toba yake, Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyoosha mkono wake kwa kuifurahia toba, na kuikubali, na mlango wa toba unabaki wazi mpaka jua lichomoze kutoka magharibi, likiashiria mwisho wa dunia, basi likichomoza mlango wa toba utafungwa.

Mafunzo
  1. Kukubaliwa toba kunaendelea maadamu mlango wake uko wazi, na mlango wake utafungwa wakati jua linapochomoza kutoka magharibi, na kwamba mtu atubu kabla ya msukosuko wa kifo, ambao ni roho kufika kooni.
  2. Kutokata tamaa kwa sababu ya dhambi, kwani msamaha na rehema za Mwenyezi Mungu ni mpana, na mlango wa toba uko wazi.
  3. Masharti ya kutubia: La kwanza: kuacha dhambi, la pili: kujuta kwa kuitenda, na la tatu: kuazimia kutorejea tena, ikiwa ni katika haki za Mwenyezi Mungu, na ikiwa inahusiana na haki za waja, basi kwa ajili ya kupokelewa toba inatakiwa kuwa haki hiyo apewe mmiliki wake au mwenye haki amsamehe.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2113) (2759). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 35). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 103). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 55).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Toba

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com