عَن أَبِي أُمَامَةَ قَالَ: حَدَّثَنِي عَمْرُو بْنُ عَبَسَةَ رضي الله عنه أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «أَقْرَبُ مَا يَكُونُ الرَّبُّ مِنَ العَبْدِ فِي جَوْفِ اللَّيْلِ الآخِرِ، فَإِنْ اسْتَطَعْتَ أَنْ تَكُونَ مِمَّنْ يَذْكُرُ اللَّهَ فِي تِلْكَ السَّاعَةِ فَكُنْ».
Kutoka kwa Abuu Umama amesema: Alinisimulia Amru bin Abasa radhi za Allah ziwe juu yake kuwa, alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Mahala pa karibu zaidi anapokuwa Mola Mlezi na mja ni katikati ya usiku wa mwisho, ikiwa utaweza kuwa miongoni mwa wanaomtaja Mwenyezi Mungu katika wakati huo basi fanya".
Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na NasaaiDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mola Mtukufu yu karibu zaidi na mja katika theluthi ya mwisho ya usiku, ikiwa utawezeshwa na ukaweza - Ewe Muumini - kuwa miongoni mwa wanaoabudu, na kuswali, na kumtaja Mwenyezi Mungu na kutubia wakati huu, basi ni jambo ambalo unapaswa kulishika na kujitahidi.
Mafunzo
- Muislamu anahimizwa kumtaja Mwenyezi Mungu mwisho wa usiku.
- Nyakati zinazidiana ubora kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu na kuomba dua na kuswali.
- Amesema Muraik: Katika tofauti baina ya kusema kwake: “Mahala pa karibu zaidi anapokuwa Mola Mlezi na mja,” na kusema kwake: “Mahala pa karibu zaidi anapokuwa mja na Mola wake Mlezi ni pale anapokuwa kasujudu”: Kinachokusudiwa hapa ni kuashiria wakati ambapo Mola anakuwa karibu zaidi na mja, yaani katikati ya usiku, na kinachokusudiwa hapo ni kueleza hali ya ukaribu wa mja na Mola ni pale anapokuwa katika hali ya kusujudu.
Marejeo
سنن الترمذي (5/ 537) (3579).
سنن أبي داود (2/ 454) (1277).
سنن النسائي (1/ 279) (572).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1019).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 509).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (17/ 535).
مشكاة المصابيح، للتبريزي (1/ 387).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَيُّهَا النَّاسُ، إِنَّ اللهَ طَيِّبٌ لَا يَقْبَلُ إِلَّا طَيِّبًا، وَإِنَّ اللهَ أَمَرَ الْمُؤْمِنِينَ بِمَا أَمَرَ بِهِ الْمُرْسَلِينَ، فَقَالَ: {يَا أَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا، إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ} [المؤمنون: 51] وَقَالَ: {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ} [البقرة: 172] ثُمَّ ذَكَرَ الرَّجُلَ يُطِيلُ السَّفَرَ أَشْعَثَ أَغْبَرَ، يَمُدُّ يَدَيْهِ إِلَى السَّمَاءِ: يَا رَبِّ، يَا رَبِّ، وَمَطْعَمُهُ حَرَامٌ، وَمَشْرَبُهُ حَرَامٌ، وَمَلْبَسُهُ حَرَامٌ، وَغُذِيَ بِالْحَرَامِ، فَأَنَّى يُسْتَجَابُ لِذَلِكَ؟».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila vizuri, na hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha kwayo Manabii, akasema Allah Mtukufu: "Enyi Mitume! Kuleni katika vile vilivyo vizuri na mtende mema, hakika mimi kwa yale mnayoyafanya ni Mjuzi" [Al-Muuminuun: 51] Na akasema Allah Mtukufu: "Enyi mlioamini! Kuleni katika vizuri miongoni mwa vile tulivyokuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu ikiwa kweli nyinyi mnamuabudu yeye peke yake" [Al-baqara: 172] akasema: Kisha akataja tukio la mtu mmoja mwenye safari ndefu, nywele zake zimetimka, kajaa vumbi, ananyanyua mikono yake kuelekea mbinguni (anasema) Mola wangu Mola wangu! (wakati huo) chakula chake ni cha haramu, na mavazi yake ni ya haramu, na kinywaji chake ni cha haramu, na lishe yake yote ni ya haramu, itawezekana vipi kujibiwa kwa mtu kama huyo?!".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu ni mzuri na ni mtakasifu ametakasika na kila mapungufu na aibu na amesifika kwa yote yaliyokamilika, na wala hakubali katika matendo kauli na itikadi isipokuwa ile itakayokuwa nzuri, nayo ni ile iliyotakaswa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, yenye kwenda sambamba na muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na haitakiwi mtu ajikurubishe kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa hayo, na katika mambo yanayosababisha amali kuwa nzuri kwa muumini ni chakula chake kuwa kizuri, na kiwe kimetokana na halali, kwa hilo amali zake zinakuwa njema, na ndio maana Mwenyezi Mungu aliwaamrisha waumini kwa lile alilowaamrisha Mitume, ikiwemo kula halali na kutenda mema, akasema: "Enyi Mitume! Kuleni katika vilivyo vizuri na mtende mema, hakika mimi kwa yale mnayoyafanya ni Mjuzi" Na akasema: "Enyi mlioamini kuleni katika vizuri katika vile tulivyokuruzukuni".
Kisha akatahadharisha rehema na amani ziwe juu yake kula haramu,ambako kunaharibu matendo na kunazuia kukubalika kwake kwa sababu yoyote ile inayoonekana; ikiwemo:
Ya kwanza: Kuwa na safari ndefu iliyo katika misingi ya kumtii Mwenyezi Mungu kama Hija na Jihadi na kuunga udugu na mengineyo.
Ya pili: Nywele kukaa hovyo kwa kutotanwa, na kubadilika rangi ya ngozi na rangi ya nguo kwa sababu ya udongo, basi mtu huyu anakuwa kadharurika.
Ya tatu: Ananyanyua mikono yake juu mbinguni kwa dua.
Ya nne: Anamuomba Mwenyezi Mungu kupitia majina yake na anang'ang'ania katika hilo: Ewe Mola wangu Ewe Mola wangu!
Na pamoja na sababu hizi za kujibiwa dua hakusikilizwa; na hii ni kwa sababu chakula chake na kinywaji chake na mavazi yake ni vya haramu, na afya yake imetokana na haramu, ni mbali sana kwa mtu mwenye sifa kama hizi kujibiwa, na atajibiwa vipi?!
Mafunzo
- Ukamilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika dhati yake, na sifa zake, na vitendo vyake, na hukumu zake.
- Amri ya kutakasa matendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa kumfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Kutumia maneno yenye kuhamasisha kufanya matendo, kiasi kwamba alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha Mitume", anapojua muumini kuwa hili ni katika yale waliyoamrishwa Mitume basi anapata nguvu na anahamasika kulitekeleza.
- Katika vizuizi vya kujibiwa dua ni kula vya haramu.
- Katika sababu za kujibiwa dua ni mambo matano: La kwanza: Kuwa na safari ndefu, kwakuwa ndani yake kuna kudhoofika, ambayo ni miongoni mwa sababu kubwa za kujibiwa. La pili: Wakati wa kudharurika. La tatu: kunyoosha mikono kuelekea mbinguni. La nne: Kung'ang'ania kwa Mwenyezi Mungu kwa kurudiarudia kusema ewe Mola Mlezi, na ni katika maneno makubwa ambayo hutumika kwa lengo la kutaka kujibiwa. La tano: Kula chakula kizuri na vinywaji vizuri.
- Kula halali nzuri ni katika sababu zinazosaidia kutenda amali njema.
- Amesema Kadhi: Kizuri ni kinyume cha kibaya, akisifiwa Mwenyezi Mungu Mtukufu basi hukusudiwa kuwa ametakasika na mapungufu, na ametukuka hana maafa, na akisifiwa mja moja kwa moja basi hukusudiwa kuwa hana tabia chafu na matendo mabaya, na anajipamba na kinyume cha hayo, na ikisifiwa mali basi hukusudiwa inapokuwa ya halali katika mali bora.
Marejeo
صحيح مسلم (2/ 703) (1015).
التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية، لإسماعيل الأنصاري (ص27).
شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص141).
الأحاديث الأربعين النووية مع ما زاد عليها ابن رجب وعليها الشرح الموجز المفيد (ص22).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «أَقْرَبُ مَا يَكُونُ الْعَبْدُ مِنْ رَبِّهِ وَهُوَ سَاجِدٌ، فَأَكْثِرُوا الدُّعَاءَ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Palipo karibu zaidi kwa mja na Mola wake ni pale anapokuwa kasujudu,Basi zidisheni dua".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa mahala palipo karibu zaidi kwa mja na Mola wake ni pale anapokuwa kasujudu; Na hii ni kwa sababu mwenye kusali huweka kiungo bora na kitukufu kuliko vyote katika mwili wake juu ya Ardhi kwa kujinyenyekeza na kujidhalilisha na kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- anapokuwa kasujudu.
Na ameamrisha -Rehema na amani ziwe juu yake- kukithirisha dua katika sijida, yanakusanyika mambo mawili katika hilo, kujidhalilisha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa kauli na vitendo.
Mafunzo
- Utiifu humzidishia mja ukaribu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Ni Sunna kukithirisha dua katika sijida; kwani ni katika maeneo ya kujibiwa.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 350) (482).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 509).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل المبارك (ص780).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 506).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الدُّعَاءُ لاَ يُرَدُّ بَيْنَ الأَذَانِ وَالإِقَامَةِ».
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maliki -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Dua hairejeshwi (inayoombwa) baina ya adhana na kukimiwa swala".
Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na NasaaiDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake fadhila za dua baina ya adhana na ikama, nakuwa dua hiyo hairejeshwi na inanafasi kubwa ya kujibiwa, basi muombeni Mwenyezi Mungu ndani ya wakati huu.
Mafunzo
- Fadhila za wakati huu kwa ajili kuomba dua.
- Atakapojipamba muombaji kwa adabu za kuomba dua, na akatafuta mahala pake na nyakati zake bora, na akajiepusha na kumuasi Mwenyezi Mungu, na akachukua tahahadhari ya kutotumbukia katika mambo yasiyofaa na yenye kutatiza, na akamdhania vizuri Mwenyezi Mungu: Basi ni rahisi sana kujibiwa, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
- Amesema Al-Munawi kuhusu kujibiwa dua: Yaani: Baada ya kukusanya sharti za dua na nguzo zake na adabu zake, ikiwa kitapelea kitu chochote basi asilaumu ila nafsi yake.
- Ni sunna kuomba dua: Ima zijibiwe haraka dua zake, au aepushiwe katika shari mfano wake, au atunziwe Akhera; na hii ni kulingana na hekima ya Mwenyezi Mungu na huruma yake.
Marejeo
سنن الترمذي (1/ 253) (212).
سنن أبي داود (1/ 392) (521).
السنن الكبرى للنسائي (9/ 32) (9812).
الثمر المستطاب في فقه السنة والكتاب، الألباني (1/ 200).
توضيح الأحكام شرح بلوغ المرام، لعبد الله البسام (1/ 548).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (2/ 309).
فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (1/ 486).
سبل السلام، لمحمد الصنعاني (2/ 707).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إنَّ اللَّهَ طَيِّبٌ لَا يَقْبَلُ إلَّا طَيِّبًا، وَإِنَّ اللَّهَ أَمَرَ المُؤْمِنِينَ بِمَا أَمَرَ بِهِ المُرْسَلِينَ، فَقَالَ تَعَالَى: {يَا أَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنْ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا}، وَقَالَ تَعَالَى: {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ} ثُمَّ ذَكَرَ الرَّجُلَ، يُطِيلُ السَّفَرَ، أَشْعَثَ، أَغْبَرَ، يَمُدُّ يَدَيْهِ إلَى السَّمَاءِ: يَا رَبِّ! يَا رَبِّ! وَمَطْعَمُهُ حَرَامٌ، وَمَشْرَبُهُ حَرَامٌ، وَمَلْبَسُهُ حَرَامٌ، وَغُذِيَ بِالحَرَامِ، فَأَنَّى يُسْتَجَابُ لَذلك».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila vizuri, na hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha kwayo Manabii, akasema Allah Mtukufu: "Enyi Mitume! Kuleni katika vile vilivyo vizuri na mtende mema, hakika mimi kwa yale mnayoyafanya ni Mjuzi" [Al-Muuminuun: 51] Na akasema Allah Mtukufu: "Enyi mlioamini! Kuleni katika vizuri miongoni mwa vile tulivyokuruzukuni, na mumshukuru Mwenyezi Mungu ikiwa kweli nyinyi mnamuabudu yeye peke yake" [Al-baqara: 172] akasema: Kisha akataja tukio la mtu mmoja mwenye safari ndefu, nywele zake zimetimka, kajaa vumbi, ananyanyua mikono yake kuelekea mbinguni (anasema) Mola wangu Mola wangu! (wakati huo) chakula chake ni cha haramu, na mavazi yake ni ya haramu, na kinywaji chake ni cha haramu, na lishe yake yote ni ya haramu, itawezekana vipi kujibiwa kwa mtu kama huyo?!".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu ni mzuri na ni mtakasifu ametakasika na kila mapungufu na aibu na amesifika kwa yote yaliyokamilika, na wala hakubali katika matendo kauli na itikadi isipokuwa ile itakayokuwa nzuri, nayo ni ile iliyotakaswa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, yenye kwenda sambamba na muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na haitakiwi mtu ajikurubishe kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa hayo, na katika mambo yanayosababisha amali kuwa nzuri kwa muumini ni chakula chake kuwa kizuri, na kiwe kimetokana na halali, kwa hilo amali zake zinakuwa njema, na ndio maana Mwenyezi Mungu aliwaamrisha waumini kwa lile alilowaamrisha Mitume, ikiwemo kula halali na kutenda mema, akasema: "Enyi Mitume! Kuleni katika vilivyo vizuri na mtende mema, hakika mimi kwa yale mnayoyafanya ni Mjuzi" Na akasema: "Enyi mlioamini kuleni katika vizuri katika vile tulivyokuruzukuni".
Kisha akatahadharisha rehema na amani ziwe juu yake kula haramu,ambako kunaharibu matendo na kunazuia kukubalika kwake kwa sababu yoyote ile inayoonekana; ikiwemo:
Ya kwanza: Kuwa na safari ndefu iliyo katika misingi ya kumtii Mwenyezi Mungu kama Hija na Jihadi na kuunga udugu na mengineyo.
Ya pili: Nywele kukaa hovyo kwa kutotanwa, na kubadilika rangi ya ngozi na rangi ya nguo kwa sababu ya udongo, basi mtu huyu anakuwa kadharurika.
Ya tatu: Ananyanyua mikono yake juu mbinguni kwa dua.
Ya nne: Anamuomba Mwenyezi Mungu kupitia majina yake na anang'ang'ania katika hilo: Ewe Mola wangu Ewe Mola wangu!
Na pamoja na sababu hizi za kujibiwa dua hakusikilizwa; na hii ni kwa sababu chakula chake na kinywaji chake na mavazi yake ni vya haramu, na afya yake imetokana na haramu, ni mbali sana kwa mtu mwenye sifa kama hizi kujibiwa, na atajibiwa vipi?!
Mafunzo
- Ukamilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika dhati yake, na sifa zake, na vitendo vyake, na hukumu zake.
- Amri ya kutakasa matendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa kumfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Kutumia maneno yenye kuhamasisha kufanya matendo, kiasi kwamba alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha Mitume", anapojua muumini kuwa hili ni katika yale waliyoamrishwa Mitume basi anapata nguvu na anahamasika kulitekeleza.
- Katika vizuizi vya kujibiwa dua ni kula vya haramu.
- Katika sababu za kujibiwa dua ni mambo matano: La kwanza: Kuwa na safari ndefu, kwakuwa ndani yake kuna kudhoofika, ambayo ni miongoni mwa sababu kubwa za kujibiwa. La pili: Wakati wa kudharurika. La tatu: kunyoosha mikono kuelekea mbinguni. La nne: Kung'ang'ania kwa Mwenyezi Mungu kwa kurudiarudia kusema ewe Mola Mlezi, na ni katika maneno makubwa ambayo hutumika kwa lengo la kutaka kujibiwa. La tano: Kula chakula kizuri na vinywaji vizuri.
- Kula halali nzuri ni katika sababu zinazosaidia kutenda amali njema.
- Amesema Kadhi: Kizuri ni kinyume cha kibaya, akisifiwa Mwenyezi Mungu Mtukufu basi hukusudiwa kuwa ametakasika na mapungufu, na ametukuka hana maafa, na akisifiwa mja moja kwa moja basi hukusudiwa kuwa hana tabia chafu na matendo mabaya, na anajipamba na kinyume cha hayo, na ikisifiwa mali basi hukusudiwa inapokuwa ya halali katika mali bora.
Marejeo
صحيح مسلم (2/ 703) (1015).
التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية، لإسماعيل الأنصاري (ص27).
شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص141).
الأحاديث الأربعين النووية مع ما زاد عليها ابن رجب وعليها الشرح الموجز المفيد (ص22).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com