Palipo karibu zaidi kwa mja na Mola wake ni pale anapokuwa kasujudu,Basi zidisheni dua
عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «أَقْرَبُ مَا يَكُونُ الْعَبْدُ مِنْ رَبِّهِ وَهُوَ سَاجِدٌ، فَأَكْثِرُوا الدُّعَاءَ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Palipo karibu zaidi kwa mja na Mola wake ni pale anapokuwa kasujudu,Basi zidisheni dua".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa mahala palipo karibu zaidi kwa mja na Mola wake ni pale anapokuwa kasujudu; Na hii ni kwa sababu mwenye kusali huweka kiungo bora na kitukufu kuliko vyote katika mwili wake juu ya Ardhi kwa kujinyenyekeza na kujidhalilisha na kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- anapokuwa kasujudu.
Na ameamrisha -Rehema na amani ziwe juu yake- kukithirisha dua katika sijida, yanakusanyika mambo mawili katika hilo, kujidhalilisha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kwa kauli na vitendo.
Mafunzo
Utiifu humzidishia mja ukaribu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Ni Sunna kukithirisha dua katika sijida; kwani ni katika maeneo ya kujibiwa.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 350) (482).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 509).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل المبارك (ص780).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 506).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com