Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Mahala pa karibu zaidi anapokuwa Mola Mlezi na mja ni katikati ya usiku wa mwisho

عَن أَبِي أُمَامَةَ قَالَ: حَدَّثَنِي عَمْرُو بْنُ عَبَسَةَ رضي الله عنه أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «أَقْرَبُ مَا يَكُونُ الرَّبُّ مِنَ العَبْدِ فِي جَوْفِ اللَّيْلِ الآخِرِ، فَإِنْ اسْتَطَعْتَ أَنْ تَكُونَ مِمَّنْ يَذْكُرُ اللَّهَ فِي تِلْكَ السَّاعَةِ فَكُنْ».
Kutoka kwa Abuu Umama amesema: Alinisimulia Amru bin Abasa radhi za Allah ziwe juu yake kuwa, alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Mahala pa karibu zaidi anapokuwa Mola Mlezi na mja ni katikati ya usiku wa mwisho, ikiwa utaweza kuwa miongoni mwa wanaomtaja Mwenyezi Mungu katika wakati huo basi fanya".
Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na NasaaiDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mola Mtukufu yu karibu zaidi na mja katika theluthi ya mwisho ya usiku, ikiwa utawezeshwa na ukaweza - Ewe Muumini - kuwa miongoni mwa wanaoabudu, na kuswali, na kumtaja Mwenyezi Mungu na kutubia wakati huu, basi ni jambo ambalo unapaswa kulishika na kujitahidi.

Mafunzo
  1. Muislamu anahimizwa kumtaja Mwenyezi Mungu mwisho wa usiku.
  2. Nyakati zinazidiana ubora kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu na kuomba dua na kuswali.
  3. Amesema Muraik: Katika tofauti baina ya kusema kwake: “Mahala pa karibu zaidi anapokuwa Mola Mlezi na mja,” na kusema kwake: “Mahala pa karibu zaidi anapokuwa mja na Mola wake Mlezi ni pale anapokuwa kasujudu”: Kinachokusudiwa hapa ni kuashiria wakati ambapo Mola anakuwa karibu zaidi na mja, yaani katikati ya usiku, na kinachokusudiwa hapo ni kueleza hali ya ukaribu wa mja na Mola ni pale anapokuwa katika hali ya kusujudu.
Marejeo

سنن الترمذي (5/ 537) (3579). سنن أبي داود (2/ 454) (1277). سنن النسائي (1/ 279) (572). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1019). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 509). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (17/ 535). مشكاة المصابيح، للتبريزي (1/ 387).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Sababu za Kujibiwa Dua.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com