Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Adh-kaar za mambo ya Dharura.

Hadithi 8

Hakika mimi ninajua neno ambalo lau kama angelisema yangemuondokea anayaoyapata (katika hasira), lau angesema: Audhubillaahi minash-shaitwani, -Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani- ingemuondokea hasira anayoipata

عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ صُرَدٍ رضي الله عنه قَالَ: كُنْتُ جَالِسًا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَرَجُلاَنِ يَسْتَبَّانِ، فَأَحَدُهُمَا احْمَرَّ وَجْهُهُ، وَانْتَفَخَتْ أَوْدَاجُهُ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنِّي لَأَعْلَمُ كَلِمَةً لَوْ قَالَهَا ذَهَبَ عَنْهُ مَا يَجِدُ، لَوْ قَالَ: أَعُوذُ بِاللَّهِ مِنَ الشَّيْطَانِ، ذَهَبَ عَنْهُ مَا يَجِدُ» فَقَالُوا لَهُ: إِنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «تَعَوَّذْ بِاللَّهِ مِنَ الشَّيْطَانِ»، فَقَالَ: وَهَلْ بِي جُنُونٌ؟
Kutoka kwa Salmaani bin Swurad -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa nimekaa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kukawa na watu wawili wakitukanana, mmoja wao uso wake ulikuwa mwekundu (kwa hasira) na ikavimba mishipa yake ya shingo, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika mimi ninajua neno ambalo lau kama angelisema yangemuondokea anayaoyapata (katika hasira), lau angesema: Audhubillaahi minash-shaitwani, -Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani- ingemuondokea hasira anayoipata" Wakasema kumwambia: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: Jikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani", akasema: Hivi mimi ninawendawazimu?
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Walitukanana na kushutumiana watu wawili mbele ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na ukawa mwekundu uso wa mmoja wao na ikavimba mishipa inayozunguka shingo yake. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika mimi ninajua neno ambalo lau angelisema huyu aliyekasirika basi hasira zingemuondokea, lau angesema: Audhubillaahi mina sh-shaitwanir rajiim - Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyelaaniwa. Wakasema kumwambia: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: Jilinde kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani. Akasema: Hivi mimi ni mwendawazimu?! Alidhania kuwa hajilindi na Shetani isipokuwa mwenye wazimu.

Mafunzo
  1. Pupa ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kutoa muongozo na kuelekeza, panapopatikana sababu zake.
  2. Hasira hutokana na Shetani.
  3. Amri ya kujilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyelaaniwa wakati wa hasira, amesema Mtukufu: "Na ikiwa uchochezi wa Shetani utakuchochea basi omba ulinzi wa Mwenyezi Mungu.." Mpaka mwisho wa Aya.
  4. Tahadhari ya kutoa matusi na yenye kufanana na matusi kama kutoa laana, na chukizo la hayo; kwa sababu mambo haya hupelekea katika uharibifu baina ya watu.
  5. Kunukuu nasaha kumpelekea ambaye hajazisikia ili anufaike nazo.
  6. Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake dhidi ya hasira; kwa sababu husukuma katika shari na ugomvi, na alikuwa rehema na amani ziwe juu yake hakasiriki isipokuwa yanapotendwa maharamisho ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hii ndio hasira nzuri.
  7. Amesema Imam Nawawi katika kauli yake "Kwani unaniona mimi ninawazimu": Kauli hii inaonyesha kuwa msemaji alikuwa ni miongoni mwa wanafiki, au ni katika mabedui wakorofi.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 124) (3282). صحيح مسلم (4/ 2015) (2610). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 110). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص50). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 270). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 78).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Bahili ni yule ambaye nitatajwa mbele yake, akawa hakuniswalia

عَنِ الحُسَينِ بنِ عَلِيٍّ بنِ أَبِي طَالِبٍ رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الْبَخِيلُ مَنْ ذُكِرْتُ عِنْدَهُ فَلَمْ يُصَلِّ عَلَيَّ».
Kutoka kwa Hussein bin Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yao amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Bahili ni yule ambaye nitatajwa mbele yake, akawa hakuniswalia"
Imepokelewa na Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuacha kumtakia rehema wakati wa kusikia jina lake au wasifu wake, na akasema: Bahili kamili ni yule nitakayetajwa mbele yake na akawa hakunitakia rehema; na hili ni kwa sababu ya mambo yafuatayo: La kwanza: Nikuwa ni ubahili kwa kitu ambacho mtu hapati hasara sawa iwe ndogo au kubwa, wala hatoi mali, na wala hatumii nguvu wala juhudi. La pili: Ni kuifanyia ubahili nafsi yake kwa sababu anainyima malipo ya kumtakia rehema Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake: kwa sababu anapojizuia kumtakia rehema atakuwa kafanya ubahili na kakataa kutimiza haki ya wajibu kwake kuitekeleza, kwa kutekeleza amri na akapata malipo. La tatu: Kumtakia rehema ndani yake kuna kutimiza haki za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, yeye ndiye aliyetufundisha, na yeye ndiye aliyetuelekeza, na yeye ndiye aliyetuita kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akaja na wahyi huu, na sheria hii, yeye ndiye sababu ya kuongoka kwetu baada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, atakayeacha kumtakia rehema basi atakuwa kamfanyia ubahili Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake kwa kutompa haki ndogo kabisa miongoni mwa haki zake

Mafunzo
  1. Kuacha kumtakia rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni miongoni mwa alama za ubahili.
  2. Kumtakia rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni katika ibada bora anazojikurubisha kwazo mja katika nyakati zote, na inatiwa mkazo hasa wakati wa kutajwa kwake.
  3. Amesema Imam Nwawi: Mtu akimsalia Mtume rehema na amani ziwe juu yake basi akusanye kati ya kumsalia na kumtakia amani, na wala asiishie katika moja ya haya; Asiseme: "Rehema ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake" Pekee, wala: "Amani iwe juu uake" pekee.
  4. Amesema Abul Aalia katika kauli yake: "Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii" Akasema: Sala ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Mtume wake: Ni kumsifia, na sala ya Malaika na watu: Ni kumuombea dua.
  5. Amesema Al-Hulaimi: Maana ya "Ewe Mwenyezi Mungu msalie Muhammad": Ewe Mwenyezi Mungu mtukuze katika dunia kwa kukuza kutajwa kwake, na kuidhihirisha dini yake, na kuibakiza sheria yake, na Akhera: Kwa kumfanya kuwa mtetezi wa umma wake, na kuyajaza malipo yake na thawabu zake, na kwa kuzionyesha wazi fadhila zake kwa wa mwanzo na wa mwisho kwa kumpa nafasi nzuri, na kwa kumtanguliza mbele kuliko wote waliokaribu nawe watakaoshuhudia Kiyama.
Marejeo

السنن الكبرى للنسائي (7/ 291) (8046). سنن الترمذي (5/ 513) (3546). مسند أحمد (3/ 257) (1736). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 486). فيض القدير شرح الجامع الصغير، لعبدالرؤوف المناوي (2/ 404). مشكاة المصابيح، لمحمد التبريزي (1/ 294). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 965).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayekula chakula, akasema: Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu aliyenilisha chakula hiki, na akaniruzuku, si kwa ujanja wangu wala kwa nguvu zangu, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia

عَنْ سَهْلِ بْنِ مُعَاذِ بْنِ أَنَسٍ عَنْ أَبِيهِ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ أَكَلَ طَعَامًا فَقَالَ: الحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَطْعَمَنِي هَذَا وَرَزَقَنِيهِ مِنْ غَيْرِ حَوْلٍ مِنِّي وَلاَ قُوَّةٍ، غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ».
Kutoka kwa Sahal bin Muadhi bin Anas kutoka kwa baba yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayekula chakula, akasema: Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu aliyenilisha chakula hiki, na akaniruzuku, si kwa ujanja wangu wala kwa nguvu zangu, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Anamhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kula chakula amshukuru Mwenyezi Mungu, kuwa mimi sina uwezo wa kuleta chakula wala kukila isipokuwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na msaada wake, Kisha akatoa habari njema rehema na amani ziwe juu yake kwa yeyote atakayesema hivyo kuwa anastahili msamaha wa Mwenyezi Mungu kwa dhambi zake ndogo ndogo zilizopita.

Mafunzo
  1. Inapendeza kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu mwisho wa chakula.
  2. Kuna ubainifu wa fadhila kubwa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya waja wake, kwa kuwa amewaruzuku na kuwasahilishia riziki, na akalifanya hilo kuwa ni kafara ya kusamehewa madhambi.
  3. Mambo ya waja yote yanatoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na si kwa uwezo wao au nguvu zao, na mja ameamrishwa kufanya sababu.
Marejeo

سنن الترمذي (5/ 452) (3458). سنن أبي داود (6/ 138) (4023). سنن ابن ماجه (4/ 417) (3285). مسند أحمد (24/ 394) (15632). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 602). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، للهلالي (2/ 54). تاج العروس من جواهر القاموس، للزبيدي (28/ 366).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayeshuka mahali akasema: Audhubikalimaatillaahit-taammaati min sharri maa khalaqa (Najilinda kwa maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyotimia kutokana na shari ya vile alivyoviumba) hakitomdhuru kitu mpaka aondoke mahala pake hapo

عن خَوْلَةَ بِنْتَ حَكِيمٍ السُّلَمِيَّةَ قَالتْ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «مَنْ نَزَلَ مَنْزِلًا ثُمَّ قَالَ: أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللهِ التَّامَّاتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ، لَمْ يَضُرَّهُ شَيْءٌ حَتَّى يَرْتَحِلَ مِنْ مَنْزِلِهِ ذَلِكَ».
Kutoka kwa Khaula bint Hakim As-Sulamiyya, amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayeshuka mahali akasema: Audhubikalimaatillaahit-taammaati min sharri maa khalaqa (Najilinda kwa maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyotimia kutokana na shari ya vile alivyoviumba) hakitomdhuru kitu mpaka aondoke mahala pake hapo".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anauelekeza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake katika kushikamana na kukimbilia kwenye tija ambako hutoeka kila chenye kuogofya anachokiogopa mwanadamu pale anaposhuka mahali katika ardhi, sawa sawa awe safarini au matembezini na kwingineko: Kuwa ajikabidhi na atake ulinzi kupitia maneno ya Allah yaliyotimia katika fadhila zake na baraka zake na manufaa yake, yaliyosalimika na kila aibu na mapungufu, kutokana na shari ya kila kiumbe chenye shari, ili awe na amani katika mazingira yake hayo kwa muda wote atakaokuwa hapo kutokana na kila chenye kuudhi.

Mafunzo
  1. Kutaka ulinzi ni ibada, nako ni kule kunakokuwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu au kwa majina yake na sifa zake.
  2. kufaa kutaka ulinzi kupitia majina ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu majina hayo ni sifa miongoni mwa sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu, kinyume na kutaka ulinzi kwa kiumbe yeyote kwani hii ni shirki.
  3. Ubora wa dua hii ni baraka zake.
  4. Kujikinga kupitia adhkari ni sababu ya mja kulindwa na shari.
  5. Kubatilika kutaka ulinzi kutoka kwa asiyekuwa Allah miongoni mwa Majini na wachawi na matapeli na wengineo.
  6. Sheria ya dua hii kusomwa na mwenye kushuka mahali nyumbani au safarini.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2080) (2708). مجموع الفتاوى (6/ 230). القول المفيد على كتاب التوحيد، لابن عثيمين (1/ 253). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص111). الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص122). معجم اللغة العربية المعاصرة، لأحمد مختار (2/ 869).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Msiutukane upepo, mkiona yanayo kuchukizeni katika upepo basi semeni: Ewe Allah tunaomba kheri za upepo huu na kheri zilizomo, na kheri ambazo kwazo umeamrishwa upepo huu, na tunataka hifadhi na ulinzi kutokana na shari zake ,na shari ambazo kwa sababu yake umeamrishwa

عَنْ أُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لاَ تَسُبُّوا الرِّيحَ، فَإِذَا رَأَيْتُمْ مَا تَكْرَهُونَ فَقُولُوا: اللَّهُمَّ إِنَّا نَسْأَلُكَ مِنْ خَيْرِ هَذِهِ الرِّيحِ وَخَيْرِ مَا فِيهَا وَخَيْرِ مَا أُمِرَتْ بِهِ، وَنَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ هَذِهِ الرِّيحِ وَشَرِّ مَا فِيهَا وَشَرِّ مَا أُمِرَتْ بِهِ».
Imepokelewa kutoka kwa Ubaiyya bin Kaab -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiutukane upepo, mkiona yanayo kuchukizeni katika upepo basi semeni: Ewe Allah tunaomba kheri za upepo huu na kheri zilizomo, na kheri ambazo kwazo umeamrishwa upepo huu, na tunataka hifadhi na ulinzi kutokana na shari zake ,na shari ambazo kwa sababu yake umeamrishwa".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo

Amekataza rehema na amani ziwe juu yake kuutukana au kuulani upepo, kwani umeamrishwa kutoka kwa muumba wake, huja kwa rehema na adhabu, na kuutukana ni kumtukana Mwenyezi Mungu muuba wake, na kuchukia maamuzi yake, kisha akaelekeza rehema na amani ziwe juu yake kurejea kwa Mwenyezi Mungu muumba wake kwa kumuomba kheri zake na kheri zilizo ndani yake, na kheri za yale yaliyotumwa, kama kuleta mvua na kuchevusha mimea na mfano wake, na kuomba kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake na shari zilizo ndani yake, na shari zilizotumwa, kama kuharibu mimea na miti na kuangamiza mifugo na kubomoa majengo, na mfano wake, na katika kumuomba Mwenyezi Mungu hilo kuna kutimiza na kuthibitisha kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Mafunzo
  1. Katazo la kutukana upepo; kwa sababu ni kiumbe kilichopangiliwa, hapo matusi yanarudi kwa muumbaji wake na mpangiliaji wake, nayo ni mapungufu katika tauhidi.
  2. Kurejea kwa Mwenyezi Mungu na kuomba kinga kwake kutokana na shari ya vile alivyoumba.
  3. Upepo huamrishwa kwa kheri, na huamrishwa kwa shari.
  4. Amesema bin Baazi: Kuutukana upepo ni miongoni mwa maasi; kwa sababu ni kiumbe kilichopangiliwa, hutumwa kwa kheri na shari; haifai kuutukana, na wala haitakiwi kusema: Mwenyezi mungu aulaani upepo, au Mwenyezi Mungu auangamize upepo, Mwenyezi Mungu asiubariki upepo huu, au mfano wa hayo, bali muumini anafanya yale aliyoelekezwa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  5. Yanalinganishwa na upepo katika uharamu wa kushutumu na kutukana yanayohusu joto na baridi na jua na vumbi na mengineyo katika yale ambayo ni katika viumbe vya Mwenyezi Mungu na uendeshaji wake.
Marejeo

سنن الترمذي (4/ 103) (2252). الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص426). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص382). القول المفيد على كتاب التوحيد، لابن عثيمين (2/ 379).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Amepata hasara mtu nitakayetajwa mbele yake na akawa hakunitakia rehema, na kapata hasara mtu ambaye itaingia Ramadhani mpaka ikatoweka kabla hajasamehewa, na kapata hasara mtu atakayewapata wazazi wake akiwa mtu mzima na wao wakiwa wazee na wakawa hawakumuingiza peponi

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «رَغِمَ أَنْفُ رَجُلٍ ذُكِرْتُ عِنْدَهُ فَلَمْ يُصَلِّ عَلَيَّ، وَرَغِمَ أَنْفُ رَجُلٍ دَخَلَ عَلَيْهِ رَمَضَانُ ثُمَّ انْسَلَخَ قَبْلَ أَنْ يُغْفَرَ لَهُ، وَرَغِمَ أَنْفُ رَجُلٍ أَدْرَكَ عِنْدَهُ أَبَوَاهُ الكِبَرَ فَلَمْ يُدْخِلاَهُ الجَنَّةَ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Amepata hasara mtu nitakayetajwa mbele yake na akawa hakunitakia rehema, na kapata hasara mtu ambaye itaingia Ramadhani mpaka ikatoweka kabla hajasamehewa, na kapata hasara mtu atakayewapata wazazi wake akiwa mtu mzima na wao wakiwa wazee na wakawa hawakumuingiza peponi".
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Makundi matatu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliyaombea dua mbaya ya pua zao kugusa mchanga kwa udhalili na unyonge na hasara: Kundi la kwanza: Yule atakayetajwa mbele yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake na akawa hakumswalia, kwa kusema: Swalla llaahu a'laihi wasallam (Rehema na amani ziwe juu yake) na mfano wake. La pili: Ni yule atakayeupata mwezi wa Ramadhani kisha mwezi ukamalizika kabla hajasamehewa kwa uzembe wake wa kufanya mambo ya kheri. La tatu: Ni mtu atakayewapata wazazi wake wakiwa watu wazima, na hawakuwa sababu ya yeye kuingia peponi kwa sababu ya kuwaasi kwake na uzembe wake katika kutekeleza haki zao.

Mafunzo
  1. Amesema As-Sanadi: Kiuhalisia nikuwa kila mmoja katika hawa kapata jambo ambalo lau kama si uzembe basi angepata fungu kubwa katika kheri, wakati alipofanya uzembe mpaka likampita hilo basi atakuwa amefeli na kupata hasara.
  2. Himizo la kumswalia Mtume rehema na amani ziwe juu yake kila linapotajwa jina lake.
  3. Himizo la kujitahidi na kujikaza katika ibada ndani ya mwezi wa Ramadhani.
  4. Himizo la kufanya juhudi kubwa katika kuwatendea wema wazazi wawili na kuwakirimu, hasa hasa wakati wa uzee.
Marejeo

سنن الترمذي (5/ 513) (3545). مسند أحمد (12/ 421) (7451). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 411). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 963). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (2/ 744). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 485). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص767).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Je, nisikujulisheni kitu bora zaidi kuliko hicho mlichoomba? Mtakapokwenda kulala basi msabihini Mwenyezi Mungu; yaani (Sub-haanallaah) mara thelathini na tatu, na mhimidini (Al-hamdulillaah) mara thelathini na tatu, na mtukuzeni (Allahu Akbar) mara thelathini na nne, kufanya hivyo ni bora zaidi kwenu kuliko mfanyakazi.”

عَنْ عَلِيٍّ رضي الله عنه: أَنَّ فَاطِمَةَ رَضيَ اللهُ عنْها أَتَتِ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ تَشْكُو إِلَيْهِ مَا تَلْقَى فِي يَدِهَا مِنَ الرَّحَى، وَبَلَغَهَا أَنَّهُ جَاءَهُ رَقِيقٌ، فَلَمْ تُصَادِفْهُ، فَذَكَرَتْ ذَلِكَ لِعَائِشَةَ، فَلَمَّا جَاءَ أَخْبَرَتْهُ عَائِشَةُ، قَالَ: فَجَاءَنَا وَقَدْ أَخَذْنَا مَضَاجِعَنَا، فَذَهَبْنَا نَقُومُ، فَقَالَ: «عَلَى مَكَانِكُمَا» فَجَاءَ فَقَعَدَ بَيْنِي وَبَيْنَهَا، حَتَّى وَجَدْتُ بَرْدَ قَدَمَيْهِ عَلَى بَطْنِي، فَقَالَ: «أَلاَ أَدُلُّكُمَا عَلَى خَيْرٍ مِمَّا سَأَلْتُمَا؟ إِذَا أَخَذْتُمَا مَضَاجِعَكُمَا -أَوْ أَوَيْتُمَا إِلَى فِرَاشِكُمَا- فَسَبِّحَا ثَلاَثًا وَثَلاَثِينَ، وَاحْمَدَا ثَلاَثًا وَثَلاَثِينَ، وَكَبِّرَا أَرْبَعًا وَثَلاَثِينَ، فَهُوَ خَيْرٌ لَكُمَا مِنْ خَادِمٍ».
Imepokelewa kutoka kwa Ally -radhi za Allah ziwe juu yake-: ِAlikuja Fatma radhi za Allah ziwe juu yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akimlalamikia juu ya jiwe la kusagia lililokuwa likichubua mikono yake, na zilimfikia taarifa kuwa Mtume amejiwa na mjakazi, lakini alikuwa hajakutana naye, akalieleza hilo kwa Aisha, alipokuja Aisha akamwambia, anasema Fatma: Akaja kwetu hali yakuwa tumekwisha panda kitandani, basi tukaamka tukasimama, akasema: "Haina haja ya kusimama kaeni tu mahala penu" Akaja akakaa kati yangu na Fatma, mpaka nikahisi ubaridi wa miguu yake tumboni kwangu, Mtume akasema: «Je, nisikujulisheni kitu bora zaidi kuliko hicho mlichoomba? Mtakapokwenda kulala basi msabihini Mwenyezi Mungu; yaani (Sub-haanallaah) mara thelathini na tatu, na mhimidini (Al-hamdulillaah) mara thelathini na tatu, na mtukuzeni (Allahu Akbar) mara thelathini na nne, kufanya hivyo ni bora zaidi kwenu kuliko mfanyakazi.”
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Fatima Mwenyezi Mungu amuwie radhi binti wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alilalamikia athari za mashine ya kusagia (Jiwe) aliyoipata mkononi mwake, hivyo alipokuja mtumwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuendea na kumuomba ampe mmoja kati ya watumwa hao, ili amsaidia kwa kazi za nyumbani, lakini hakumkuta Mtume nyumbani kwake, ila alimkuta Aisha Mwenyezi Mungu amuwie radhi, hivyo akamwambia kuhusu hilo, Alipofika rehema na amani ziwe juu yake Aisha akamueleza kuwa Fatma alikuja kwake kumuomba mfanyakazi. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaja kwa Fatma na Ally Mwenyezi Mungu awawie radhi, ndani ya nyumba yao wakiwa wamelala kitandani wakijiandaa kwa usingizi, akakaa katikati yao mpaka Ally radhi za Allah ziwe juu yake akahisi ubaridi wa miguu ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, juu ya tumbo lake, akasema: Hivi nisikufundisheni kilicho bora zaidi kuliko mlichoniomba, kuliko kukupeni mtumishi? Wakasema: Ndio, tufundishe, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Mtakapochukua nafasi zenu za kulala usiku, basi toeni takbira mara thelathini na nne, kwa kusema: Allahu Akbaru, Na toeni tasbihi mara thelathini na tatu, kwa kusema: Sub-haanallaah, Na himidini mara thelathini na tatu, kwa kusema: Al-hamdulillah; Dhikiri hii ni bora sana kwenu nyinyi kuliko kuwa na mtumishi.

Mafunzo
  1. Inapendeza kudumu na dhikiri hi iliyobarikiwa, kama ilivyoripotiwa kuwa Ally radhi za Allah ziwe juu yake hakuiacha amri hii ya Mtume iliyokusanya mambo mengi, mpaka katika usiku wa mapigano ya Swuffin.
  2. Dhikiri hii haisemwi tu wakati wa kulala usiku, na maneno yake kwa mujibu wa Muslim yanatokana na riwaya ya Muadhi kutoka kwa Shu’ba: “Mkichukua vitanda vyenu wakati wa usiku.”
  3. Muislamu akiisahau dhikri hii mwanzoni mwa usiku kisha akaikumbuka mwishoni mwa usiku, hakuna ubaya kuisema; Kwa sababu Ally Mwenyezi Mungu amuwie radhi, msimuliaji wa hadithi, anasema kwamba alisahau kuyasema katika usiku wa mapigano ya Swaffin mwanzoni mwa usiku, kisha akakumbuka na kuyasema kabla ya Alfajiri.
  4. Amesema Al-Muhallab: Ndani ya Hadithi hii kunaonyesha kuwa mtu ailazimishe familia yake kufanya anayojilazimisha yeye, kama kutanguliza maisha ya Akhera kuliko Dunia hii ikiwa wana uwezo wa kufanya hivyo.
  5. Amesema bin Hajar Al-Asqalani: Atakayedumu na dhikiri hii hatadhurika na wingi wa kazi, wala haitakuwa vigumu kwake hata akichoka.
  6. Amesema Al-Aini: Suala la kuwa bora ni ima maana yake ni kuwa inahusiana na Akhera na mfanyakazi duniani, na Akhera ni bora zaidi na yenye kudumu, au ina maana kwamba kuhusiana na kile alichoomba atapata nguvu kwa sababu ya dhikiri hii ambayo itamuwezesha kufanya kazi zaidi kuliko uwezo wa mfanyakazi.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 65) (5361). صحيح مسلم (4/ 2091) (2727). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 531). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 555). شرح صحيح البخاري، لابن بطال (5/ 270). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين. نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 998).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Huyo ni Shetani anaitwa Khinzab, ukimuhisi basi haraka sana taka ulinzi kutoka kwa Allah dhidi yake, na uteme kushotoni kwako mara tatu

عن عُثْمَانَ بْنَ أَبِي الْعَاصِ رضي الله عنه: أنه أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، إِنَّ الشَّيْطَانَ قَدْ حَالَ بَيْنِي وَبَيْنَ صَلَاتِي وَقِرَاءَتِي يَلْبِسُهَا عَلَيَّ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «ذَاكَ شَيْطَانٌ يُقَالُ لَهُ خِنْزَِبٌ، فَإِذَا أَحْسَسْتَهُ فَتَعَوَّذْ بِاللهِ مِنْهُ، وَاتْفُلْ عَلَى يَسَارِكَ ثَلَاثًا»، قَالَ: فَفَعَلْتُ ذَلِكَ فَأَذْهَبَهُ اللهُ عَنِّي.
Kutoka kwa Othman bin Abil Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yake-: Yakwamba yeye alimwendea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika shetani amekaa kati yangu na swala yangu na kisomo changu ananichanganya, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Huyo ni Shetani anaitwa Khinzab, ukimuhisi basi haraka sana taka ulinzi kutoka kwa Allah dhidi yake, na uteme kushotoni kwako mara tatu", anasema: Nikafanya hivyo Mwenyezi Mungu akamuondosha kwangu.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alikuja Othman bin Abil Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yake- kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika Shetani ameziba kati yangu na swala yangu, na amenizuilia na kupata utulivu ndani yake, na amenichanganyia kisomo changu na amenitia wasi wasi ndani yake, Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Huyo ni Shetani aitwaye Khinzab, ukihisi hali hii basi taka kinga kwa Allah, na utake ulinzi kutoka kwa Allah dhidi yake, na uteme mate kushotoni kwako mara tatu, Othman anasema: Nikafanya aliyoniamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Mwenyezi Mungu akaniondolea hali hiyo.

Mafunzo
  1. Umuhimu wa utulivu na kuhudhurisha moyo ndani ya sala, na kuwa Shetani anajitahidi kutia tashiwishi na shaka ndani yake.
  2. Sunna ya kutaka ulinzi kutokana na shetani wakati wa wasi wasi wake ndani ya sala, pamoja na kutema kushoto mara tatu.
  3. Kumebainishwa waliyokuwa nayo Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- katika swala la kurudi kwao kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika yale yanayojitokeza kwao miongoni mwa changamoto ili azitatue.
  4. Maisha ya nyoyo za Masahaba, na kwamba hima yao kubwa ilikuwa ni Akhera.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 1728) (2203)، إكمال المعلم (7/110)، شرح النّووي على مسلم (14/190)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (36/ 136).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com