Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Atakayekula chakula, akasema: Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu aliyenilisha chakula hiki, na akaniruzuku, si kwa ujanja wangu wala kwa nguvu zangu, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia

عَنْ سَهْلِ بْنِ مُعَاذِ بْنِ أَنَسٍ عَنْ أَبِيهِ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ أَكَلَ طَعَامًا فَقَالَ: الحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَطْعَمَنِي هَذَا وَرَزَقَنِيهِ مِنْ غَيْرِ حَوْلٍ مِنِّي وَلاَ قُوَّةٍ، غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ».
Kutoka kwa Sahal bin Muadhi bin Anas kutoka kwa baba yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayekula chakula, akasema: Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu aliyenilisha chakula hiki, na akaniruzuku, si kwa ujanja wangu wala kwa nguvu zangu, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Anamhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kula chakula amshukuru Mwenyezi Mungu, kuwa mimi sina uwezo wa kuleta chakula wala kukila isipokuwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na msaada wake, Kisha akatoa habari njema rehema na amani ziwe juu yake kwa yeyote atakayesema hivyo kuwa anastahili msamaha wa Mwenyezi Mungu kwa dhambi zake ndogo ndogo zilizopita.

Mafunzo
  1. Inapendeza kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu mwisho wa chakula.
  2. Kuna ubainifu wa fadhila kubwa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya waja wake, kwa kuwa amewaruzuku na kuwasahilishia riziki, na akalifanya hilo kuwa ni kafara ya kusamehewa madhambi.
  3. Mambo ya waja yote yanatoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na si kwa uwezo wao au nguvu zao, na mja ameamrishwa kufanya sababu.
Marejeo

سنن الترمذي (5/ 452) (3458). سنن أبي داود (6/ 138) (4023). سنن ابن ماجه (4/ 417) (3285). مسند أحمد (24/ 394) (15632). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 602). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، للهلالي (2/ 54). تاج العروس من جواهر القاموس، للزبيدي (28/ 366).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Adh-kaar za mambo ya Dharura.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com