Makundi matatu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliyaombea dua mbaya ya pua zao kugusa mchanga kwa udhalili na unyonge na hasara: Kundi la kwanza: Yule atakayetajwa mbele yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake na akawa hakumswalia, kwa kusema: Swalla llaahu a'laihi wasallam (Rehema na amani ziwe juu yake) na mfano wake. La pili: Ni yule atakayeupata mwezi wa Ramadhani kisha mwezi ukamalizika kabla hajasamehewa kwa uzembe wake wa kufanya mambo ya kheri. La tatu: Ni mtu atakayewapata wazazi wake wakiwa watu wazima, na hawakuwa sababu ya yeye kuingia peponi kwa sababu ya kuwaasi kwake na uzembe wake katika kutekeleza haki zao.
- Amesema As-Sanadi: Kiuhalisia nikuwa kila mmoja katika hawa kapata jambo ambalo lau kama si uzembe basi angepata fungu kubwa katika kheri, wakati alipofanya uzembe mpaka likampita hilo basi atakuwa amefeli na kupata hasara.
- Himizo la kumswalia Mtume rehema na amani ziwe juu yake kila linapotajwa jina lake.
- Himizo la kujitahidi na kujikaza katika ibada ndani ya mwezi wa Ramadhani.
- Himizo la kufanya juhudi kubwa katika kuwatendea wema wazazi wawili na kuwakirimu, hasa hasa wakati wa uzee.
سنن الترمذي (5/ 513) (3545). مسند أحمد (12/ 421) (7451). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 411). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 963). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (2/ 744). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 485). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص767).