عن جابر رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «أَفْضَلُ الذِّكْرِ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَأَفْضَلُ الدُّعَاءِ: الْحَمْدُ لِلهِ».
Imepokelewa Kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Dhikiri bora ni: Laa ilaaha Illa llaah: Na dua bora ni: Al-hamdulillah".
Imepokelewa na Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn MajahDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Anatueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa dhikiri bora ni: "Laa ilaaha illa llaah" Na maana yake, hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa dua bora ni "Al-hamdulillaah"; Nayo inamaanisha kukiri kuwa mneemeshaji ni Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka-, mwenye kustahiki sifa nzuri zilizokamilika.
Mafunzo
- Himizo la kukithirisha kumtaja Allah kwa neno la tauhidi (Laa ilaaha illa llaah), na kuomba kupitia himidi (Shukurani kwa Allah).
Marejeo
سنن الترمذي (5/ 393) (3383).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (2/ 984).
زاد المعاد في هدي خير العباد، ابن قيم الجوزية (1/ 36).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن سَمُرَة بن جندبٍ رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «أَحَبُّ الْكَلَامِ إِلَى اللهِ أَرْبَعٌ: سُبْحَانَ اللهِ، وَالْحَمْدُ لِلهِ، وَلَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَاللهُ أَكْبَرُ، لَا يَضُرُّكَ بِأَيِّهِنَّ بَدَأْتَ».
Imepokewa kutoka kwa Jundubi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Maneno yanayopendeka zaidi kwa Allah ni manne: Sub-haanallah, Al-hamdulillaah, na Laa ilaaha illa llaah, na Allahu Akbar, haidhuru ikiwa utaanza na lolote kati ya hao".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa maneno yanayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni manne.
Sub-haanallaah: Na hili linamaanisha kumtakasa Mwenyezi Mungu na kila aina ya mapungufu.
Na Al-hamdulillaah: Nako ni kumsifu Allah kwa ukamilifu uliotimia pamoja na kumpenda na kumtukuza.
Na Laa ilaaha illa llaah: Yaani: Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allah.
Na Allahu Akbaru: Yaani: Ni Mtukufu mno, na ni Mtakatifu mno kuliko kila kitu.
Nakuwa fadhila zake na kupata thawabu zake si lazima kuyapangilia wakati wa kuyatamka.
Mafunzo
- Wepesi wa sheria, kiasi kwamba haidhuru kwa neno lipi kati ya hayo utaanza nalo.
Marejeo
صحيح مسلم (3/ 1685) (2137)، (4/ 2093) (2731)، (4/ 2072) (2695).
توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 540).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 411).
فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 477).
سبل السلام بشرح بلوغ المرام، للصنعاني (2/ 706).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «كَلِمَتَانِ خَفِيفَتَانِ عَلَى اللِّسَانِ، ثَقِيلَتَانِ فِي الْمِيزَانِ، حَبِيبَتَانِ إِلَى الرَّحْمَنِ: سُبْحَانَ اللهِ الْعَظِيمِ، سُبْحَانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Maneno mawili mepesi mno katika ulimi, ni mazito mno katika mizani, yanapendeka mno kwa Al-Rahmani (Mwingi wa rehema) Ni: Sub-haanallahil Adhwiim, Sub-haanallaahi wabihamdihi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-kuhusu maneno mawili anayoyatamka mwanadamu bila uzito wowote na kwa hali yoyote, nakuwa maneno hayo malipo yake ni makubwa katika mizani, nakuwa Mola wetu Mlezi Mwingi wa rehema -Aliyetakasika na kutukuka- anayapenda:
Sub-haanallahil Adhwiim, Sub-haanallahi wabihamdihi; Kwakuwa yamekusanya sifa miongoni mwa sifa za Allah kumsifu kwa Utukufu na ukamilifu, na kumtakasa kutokana na mapungufu -Aliyetakasika na kutukuka-.
Mafunzo
- Dhikri tukufu zaidi ni ile inayokusanya kati ya kumtakasa Allah pamoja na kumtukuza.
- Kumebainishwa upana wa rehama ya Allah kwa waja wake, kwani Yeye analipa kwa amali ndogo thawabu nyingi.
Marejeo
صحيح البخاري (8/ 86) (6406).
صحيح مسلم (4/ 2072) (2694).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 480).
فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 519).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَا جَلَسَ قَوْمٌ مَجْلِسًا لَمْ يَذْكُرُوا اللَّهَ فِيهِ وَلَمْ يُصَلُّوا عَلَى نَبِيِّهِمْ إِلاَّ كَانَ عَلَيْهِمْ تِرَةً، فَإِنْ شَاءَ عَذَّبَهُمْ وَإِنْ شَاءَ غَفَرَ لَهُمْ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hawajawahi kukaa watu kikao chochote wakawa hawakumtaja Mwenyezi Mungu ndani yake, na wala hawakumsalia Nabii wao, isipokuwa itakuwa ni hasara juu yao, akitaka atawaadhibu na akitaka atawasamehe".
ImepokAbu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu AlkubraaDarajaSahihi
Maelezo
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kughafilika kumtaja Mwenyezi Mungu, nakuwa hawatokaa watu katika kikao chochote na wakawa hawakumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake, na wakawa hawakumsalia Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake isipokuwa kikao hicho kitakuwa ni hasara na majuto juu yao na mapungufu siku ya Kiyama, akitaka atawaadhibu kwa madhambi yao yaliyotangulia na uzembe wao uliofuata, na akitaka atawasamehe ikiwa ni fadhila na rehema kutoka kwake.
Mafunzo
- Himizo la kufanya dhikiri na fadhila zake.
- Fadhila za vikao ambavyo anatajwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake, na kumtaja Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, nakwamba vikao ambavyo havina hayo ni vikao vibaya kwa watu siku ya Kiyama.
- Tahadhari iliyotajwa ya kughafilika kumtaja Mwenyezi Mungu haishii katika vikao pekee, bali inaenea katika sehemu zingine, amesema Nawawi: Ni machukizo kwa atakayekaa mahali aondoke bila kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake.
- Masikitiko yatakayotokea siku ya Kiyama: Ima ni kwa sababu ya kupoteza malipo na thawabu kwa kutofaidika na wakati kwa kumtii Mwenyezi Mungu, na ima ni kwa madhambi na adhabu kwa kuutumia wakati kwa kumuasi Mwenyezi Mungu.
- Tahadhari hii ni pale kughafilika kutakapokuwa ni kwa mambo ya halali, je, ni vipi vikiwa vikao vya haramu ambavyo ndani yake kuna utesi na usengenyaji na mengineyo?!.
Marejeo
سنن أبي داود (7/ 221) (4855).
سنن الترمذي (5/ 391) (3380).
السنن الكبرى للنسائي (9/ 155) (10163).
توضيح الأحكام من بلوغ المرام، لعبد الله البسام (7/ 524).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 396).
فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 464).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «لَأَنْ أَقُولَ: سُبْحَانَ اللهِ، وَالْحَمْدُ لِلهِ، وَلَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَاللهُ أَكْبَرُ، أَحَبُّ إِلَيَّ مِمَّا طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمْسُ».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kusema kwangu: Sub-haanallaah, na Alhamdulillaah, na Laa ilaaha illa llaah, na Allaahu Akbaru, kunapendeka sana kwangu kuliko vitu vyote vilizochomozewa na jua".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kumtaja Allah Mtukufu kwa maneno haya matukufu ni bora kuliko dunia na vilivyomo, na utajo huo ni kusema:
"Sub-haana llaah": Ni kumtakasa Mwenyezi Mungu kutokana na mapungufu.
"Alhamdulillaah": Ni kumsifia kwa sifa za ukamilifu pamoja na kumpenda na kumtukuza.
"Laa ilaaha illa llaah": Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu.
"Allaahu Akbaru: Mkubwa na Mtukufu kuliko kila kitu.
Mafunzo
- Himizo la kumtaja Mwenyezi Mungu, nakuwa hilo linapendeka zaidi kuliko vyote vilivyochomozewa na jua.
- Himizo la kukithirisha dhikiri; kwakuwa ndani yake kuna malipo na fadhila kubwa.
- Starehe za dunia ni ndogo na matamanio yake ni yenye kuondoka.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2072) (2695).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 496).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 485).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (2/ 970).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل المبارك (ص772).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَن أَبي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ قَالَ: رَضِيتُ بِاللَّهِ رَبًّا، وَبِالْإِسْلَامِ دِينًا، وَبِمُحَمَّدٍ رَسُولًا، وَجَبَتْ لَهُ الْجَنَّةُ».
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake, yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayesema nimeridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, na kuwa Uislamu ni dini, na Muhammadi kuwa Mtume, basi atastahiki kwake Papo".
Imepokelewa na Abu DaudDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema: "Nimemridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola" na Mungu na Mlezi na Mmiliki, na bwana na Mtengenezaji, "na Uislamu" kwa hukumu zake zote kwanzia amri zake na makatazo yake "kuwa Dini" mila na sheria, itikadi na utii, "na Muhammadi kuwa Mtume" na Nabii; kwa yote aliyotumwa kwayo na akatufikishia, isipokuwa itamstahikia kwake Pepo.
Mafunzo
- Himizo la kusema dua hii, na kumebainishwa thawabu zinazoambatana nayo.
- Kumridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, kunaambatana na mtu kutomuabudu asiyekuwa yeye Mtukufu.
- Kumridhia Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake kuwa Nabii na Mtume, kunaambatana na kumtii rehema na amani ziwe juu yake na kutii sunna zake.
- Kuridhia Uislamu kuwa dini ni kuridhia yale aliyoyachagua Mwenyezi Mungu kwa waja wake.
- Sunna ya kusema dua hii wakati wa shahada mbili baada kusikia Adhana, kama ilivyokuja katika riwaya zingine.
- Na imekuja katika hadithi nyingine sunna ya kuomba dua hii wakati wa asubuhi na jioni.
Marejeo
سنن أبي داود (2/ 635) (1529).
شرح أبي داود للعيني (5/ 439).
شرح سنن أبي داود لابن رسلان (7/ 348).
المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (3/ 710).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com