Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-kuhusu maneno mawili anayoyatamka mwanadamu bila uzito wowote na kwa hali yoyote, nakuwa maneno hayo malipo yake ni makubwa katika mizani, nakuwa Mola wetu Mlezi Mwingi wa rehema -Aliyetakasika na kutukuka- anayapenda: Sub-haanallahil Adhwiim, Sub-haanallahi wabihamdihi; Kwakuwa yamekusanya sifa miongoni mwa sifa za Allah kumsifu kwa Utukufu na ukamilifu, na kumtakasa kutokana na mapungufu -Aliyetakasika na kutukuka-.
- Dhikri tukufu zaidi ni ile inayokusanya kati ya kumtakasa Allah pamoja na kumtukuza.
- Kumebainishwa upana wa rehama ya Allah kwa waja wake, kwani Yeye analipa kwa amali ndogo thawabu nyingi.
صحيح البخاري (8/ 86) (6406). صحيح مسلم (4/ 2072) (2694). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 480). فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 519).