Dhikiri bora ni: Laa ilaaha Illa llaah: Na dua bora ni: Al-hamdulillah
عن جابر رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «أَفْضَلُ الذِّكْرِ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَأَفْضَلُ الدُّعَاءِ: الْحَمْدُ لِلهِ».
Imepokelewa Kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Dhikiri bora ni: Laa ilaaha Illa llaah: Na dua bora ni: Al-hamdulillah".
Imepokelewa na Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn MajahDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Anatueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa dhikiri bora ni: "Laa ilaaha illa llaah" Na maana yake, hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa dua bora ni "Al-hamdulillaah"; Nayo inamaanisha kukiri kuwa mneemeshaji ni Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka-, mwenye kustahiki sifa nzuri zilizokamilika.
Mafunzo
Himizo la kukithirisha kumtaja Allah kwa neno la tauhidi (Laa ilaaha illa llaah), na kuomba kupitia himidi (Shukurani kwa Allah).
Marejeo
سنن الترمذي (5/ 393) (3383).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (2/ 984).
زاد المعاد في هدي خير العباد، ابن قيم الجوزية (1/ 36).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com