Kutoka kwa MughIira Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika safari, nikanyoosha mikono ili nimvue viatu vyake (khufu), akasema: "Ziache, kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi", akafuta juu yake.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika moja ya safari zake akatawadha, alipofikia kuosha miguu miwili alinyoosha Mughira bin Shu'ba Radhi za Allah ziwe juu yake mikono yake ili avue kilichokuwa miguuni kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika khufu (viatu mithili ya soksi) ili Mtume aoshe miguu yake! Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ziache na wala usizivue, kwani mimi niliingiza miguu yangu ndaniya khufu mbili nikiwa katika twahara, Akafuta Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya khufu zake badala ya kuosha miguu miwili.
Mafunzo
Sheria ya kufuta juu ya khufu mbili inakuwa wakati wa kutia udhu kwa ajili ya hadathi ndogo, ama kuoga kwa ajili ya hadathi kubwa ni lazima kuosha miguu.
Kufuta kunakuwa mara moja kwa kupitisha mkono ulioloana juu ya khufu nasi chini yake.
Ni sharti wakati wa kufuta juu ya khufu iwe kuzivaa kwake ni baada ya udhu kamili ambao aliosha miguu yake wakati huo kwa maji, na khufu ziwe twahara (safi) na zifunike mahali panapolazimika kuoshwa katika miguu, na kuwe kufuta ni katika hadathi ndogo si katika janaba au chochote kinachowajibisha kuoga, na kufuta kuwe katika muda uliopangwa kisheria nao ni usiku na mchana kwa mwenyeji na siku tatu kwa msafiri.
Kitapimwa katika khufu mbili kila chenye kusitiri miguu miwili kama soksi na kinginecho, inafaa kufuta juu yake.
Uzuri wa tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na mafundisho yake, kiasi kwamba alimzuia Mughira kumvua, na akamueleza sababu: Kuwa alizivaa akiwa twahara; ili nafsi yake itulizane, na ajue hukumu ya hilo.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 52) (206).
صحيح مسلم (1/ 230) (274).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص50).
الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 36).
خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص27).
عن أبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا يَحِلُّ لِامْرَأَةٍ مُسْلِمَةٍ تُسَافِرُ مَسِيرَةَ لَيْلَةٍ إِلَّا وَمَعَهَا رَجُلٌ ذُو حُرْمَةٍ مِنْهَا».
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Si halali kwa mwanamke wa kiislamu kusafiri mwendo wa usiku mmoja, isipokuwa awe pamoja na mwanaume mwenye uharamu wa kumuoa (ndugu yake)".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ni haramu kwa mwanamke wa kiislamu kusafiri mwendo wa usiku mmoja isipokuwa awe pamoja na mwanaume katika maharimu wake.
Mafunzo
Amesema bin Hajari: Kutofaa kwa mwanamke kusafiri pasina maharim (ndugu), ni makubaliano ya wanachuoni isipokuwa katika Hija na Umra, na kutoka katika mji wa ushirikina, na wako waliolifanya hilo kuwa ni katika masharti ya Hija.
Ukamilifu wa sheria ya Uislamu, na pupa yake juu ya kumlinda mwanamke na kumchunga.
Kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho kunapelekea kunyenyekea sheria za Mwenyezi Mungu, na kusimama katika mipaka yake.
Maharimu wa mwanamke ni mume wake au mtu wa haramu kwake kumuoa milele kwa sababu ya ukaribu wa kiukoo, au kunyonya, au ukwe, na anatakiwa awe muislamu, aliyebaleghe, mwenye akili timamu, mkweli, mwaminifu; kwa sababu lengo la maharimu ni kumlinda mwanamke na kumchunga na kusimamia mambo yake.
Amesema Baihaqi: Kuhusu riwaya zilizokuja katika muda wa safari anaosafiri mwanamke ndani yake pamoja na maharimu: Na kilichopo nikuwa kila kinachoitwa safari mwanamke anakatazwa kusafiri pasina mume au maharimu, sawa sawa ziwe ni siku tatu au mbili au moja, au kaagizwa au kinginecho; kwa sababu ya riwaya ya bin Abbasi ambayo haikubagua, na ndio riwaya za mwisho za Imam Muslim zilizotangulia: "Asisafiri mwanamke isipokuwa awe pamoja na maharimu" Na hii inakusanya yote yanayoitwa safari. Mwisho, na hadithi hii ilikuwa kulingana na hali ya muulizaji na mji wake.
Marejeo
صحيح البخاري (2/ 43) (1088).
صحيح مسلم (2/ 977) (1339).
تيسير العلام، لعبد الله البسام (ص374).
تنبيه الأفهام شرح عمدة الإحكام، لابن عثيمين (3/ 501).
خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص178).
Kutoka kwa Abdallah bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake, amesema: Tulipita tukiwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika Hijiri (miji ya Thamudi), akasema kutuambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Msiingie miji ya wale waliozidhulumu nafsi zao, isipokuwa muwe mnalia; kwa kutahadhari msijekupatwa na mfano wa yale yaliyowapata" Kisha akampigia kelele mnyama wake akaongeza mwendo mpaka akapapita.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Alikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipopita katika miji ya Thamudi, kutoingia katika miji ya walioadhibiwa, wale waliozidhulumu nafsi zao au kuiendea miji hiyo, isipokuwa anayeingia kama atakuwa analia kwa kuchukua mazingatio kwao; kwa kuhofia asijekufikwa na mfano wa yale yaliyowafika miongoni mwa adhabu, kisha akampigia kelele mnyama wake akaongeza mbio mpaka akaivuka.
Mafunzo
Kutafakari katika hali za wale aliowaangamiza Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuchukua tahadhari katika yale waliyotumbukia kwayo; na kuchukua tahadhari ya kujisahau kutozingatia alama.
Miji ya hao walioadhibiwa haitakiwi kuishi baada yao, na wala haifanwyi kuwa makazi, kwa sababu atakayeishi hapo hawezi kulia daima, na ilikatazwa kuingia ila kwa sifa hii.
Amesema Nawawi: Hapa kuna himizo la kuchunga wakati wa kupita katika miji ya madhalimu, na sehemu za adhabu, na mfano wake vile vile ni kwenda haraka katika bonde la Muhassiri (Liko Makkah, katika Mina na Muzdalifa); kwa sababu watu wa ndovu waliangamia huko, inatakiwa kwa mwenye kupita katika mfano wa sehemu hizi kuchunga na kuwa na hofu na kulia, na kuchukua mazingatio kwao na maangamizo yao, na aombe kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na hilo.
Katazo na tahadhari yanakusanya nyumba za Thamudi na wengineo wenye kufanana nao katika umma nyinginezo walioteremkiwa na adhabu.
Katazo la kuzifanya sehemu na maeneo haya kuwa sehemu za utalii na matembezi na mfano wake.
Marejeo
صحيح البخاري (4/ 149) (3380).
صحيح مسلم (4/ 2286) (2980).
النهاية في غريب الحديث والأثر (187) (395).
إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (6/ 458) (5/ 368).
البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (45/ 169).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com