Alikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipopita katika miji ya Thamudi, kutoingia katika miji ya walioadhibiwa, wale waliozidhulumu nafsi zao au kuiendea miji hiyo, isipokuwa anayeingia kama atakuwa analia kwa kuchukua mazingatio kwao; kwa kuhofia asijekufikwa na mfano wa yale yaliyowafika miongoni mwa adhabu, kisha akampigia kelele mnyama wake akaongeza mbio mpaka akaivuka.
- Kutafakari katika hali za wale aliowaangamiza Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuchukua tahadhari katika yale waliyotumbukia kwayo; na kuchukua tahadhari ya kujisahau kutozingatia alama.
- Miji ya hao walioadhibiwa haitakiwi kuishi baada yao, na wala haifanwyi kuwa makazi, kwa sababu atakayeishi hapo hawezi kulia daima, na ilikatazwa kuingia ila kwa sifa hii.
- Amesema Nawawi: Hapa kuna himizo la kuchunga wakati wa kupita katika miji ya madhalimu, na sehemu za adhabu, na mfano wake vile vile ni kwenda haraka katika bonde la Muhassiri (Liko Makkah, katika Mina na Muzdalifa); kwa sababu watu wa ndovu waliangamia huko, inatakiwa kwa mwenye kupita katika mfano wa sehemu hizi kuchunga na kuwa na hofu na kulia, na kuchukua mazingatio kwao na maangamizo yao, na aombe kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na hilo.
- Katazo na tahadhari yanakusanya nyumba za Thamudi na wengineo wenye kufanana nao katika umma nyinginezo walioteremkiwa na adhabu.
- Katazo la kuzifanya sehemu na maeneo haya kuwa sehemu za utalii na matembezi na mfano wake.
صحيح البخاري (4/ 149) (3380). صحيح مسلم (4/ 2286) (2980). النهاية في غريب الحديث والأثر (187) (395). إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (6/ 458) (5/ 368). البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (45/ 169).