Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Si halali kwa mwanamke wa kiislamu kusafiri mwendo wa usiku mmoja, isipokuwa awe pamoja na mwanaume mwenye uharamu wa kumuoa (ndugu yake)

عن أبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا يَحِلُّ لِامْرَأَةٍ مُسْلِمَةٍ تُسَافِرُ مَسِيرَةَ لَيْلَةٍ إِلَّا وَمَعَهَا رَجُلٌ ذُو حُرْمَةٍ مِنْهَا».
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Si halali kwa mwanamke wa kiislamu kusafiri mwendo wa usiku mmoja, isipokuwa awe pamoja na mwanaume mwenye uharamu wa kumuoa (ndugu yake)".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ni haramu kwa mwanamke wa kiislamu kusafiri mwendo wa usiku mmoja isipokuwa awe pamoja na mwanaume katika maharimu wake.

Mafunzo
  1. Amesema bin Hajari: Kutofaa kwa mwanamke kusafiri pasina maharim (ndugu), ni makubaliano ya wanachuoni isipokuwa katika Hija na Umra, na kutoka katika mji wa ushirikina, na wako waliolifanya hilo kuwa ni katika masharti ya Hija.
  2. Ukamilifu wa sheria ya Uislamu, na pupa yake juu ya kumlinda mwanamke na kumchunga.
  3. Kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho kunapelekea kunyenyekea sheria za Mwenyezi Mungu, na kusimama katika mipaka yake.
  4. Maharimu wa mwanamke ni mume wake au mtu wa haramu kwake kumuoa milele kwa sababu ya ukaribu wa kiukoo, au kunyonya, au ukwe, na anatakiwa awe muislamu, aliyebaleghe, mwenye akili timamu, mkweli, mwaminifu; kwa sababu lengo la maharimu ni kumlinda mwanamke na kumchunga na kusimamia mambo yake.
  5. Amesema Baihaqi: Kuhusu riwaya zilizokuja katika muda wa safari anaosafiri mwanamke ndani yake pamoja na maharimu: Na kilichopo nikuwa kila kinachoitwa safari mwanamke anakatazwa kusafiri pasina mume au maharimu, sawa sawa ziwe ni siku tatu au mbili au moja, au kaagizwa au kinginecho; kwa sababu ya riwaya ya bin Abbasi ambayo haikubagua, na ndio riwaya za mwisho za Imam Muslim zilizotangulia: "Asisafiri mwanamke isipokuwa awe pamoja na maharimu" Na hii inakusanya yote yanayoitwa safari. Mwisho, na hadithi hii ilikuwa kulingana na hali ya muulizaji na mji wake.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 43) (1088). صحيح مسلم (2/ 977) (1339). تيسير العلام، لعبد الله البسام (ص374). تنبيه الأفهام شرح عمدة الإحكام، لابن عثيمين (3/ 501). خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص178).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Adabu na Hukumu za Safari.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com