عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي لله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا يَفْرَكْ مُؤْمِنٌ مُؤْمِنَةً، إِنْ كَرِهَ مِنْهَا خُلُقًا رَضِيَ مِنْهَا آخَرَ» أَوْ قَالَ: «غَيْرَهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hachukii muumini wa kiume tabia za muumini wa kike, akichukia tabia fulani basi ataridhishwa na tabia nyingine" Au alisema: "Tabia tofauti na hiyo"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mume kumchukia sana mke wake hadi kupelekea dhulma, na kumuacha na kumtelekeza; Mwanadamu ana asili ya kutokamilika, na ikiwa atachukia kwake tabia moja mbaya, basi atapata tabia nyingine nzuri; ataridhia kwa tabia hiyo nzuri anayoikubali, na avumilie kwa tabia asizozipenda miongoni mwa tabia mbaya, ambazo humfanya awe mvumilivu na asimchukie kiasi cha kutaka kumuacha.
Mafunzo
- Huu ni wito kwa muumini wa kuja katika haki na uadilifu, na kuhukumu mambo kwa akili katika mgogoro wowote unaotokea baina yake na mke wake, na sio kutoa maamuzi kwa hisia na mihemuko ya muda mfupi.
- Kazi ya muumini si kumchukia mwanamke muumini kabisa mpaka afikie kuachana naye, bali apuuze kile anachochukia kwa kile anachopenda.
- Himizo la kuishi vizuri na kutengeneza urafiki kati ya wanandoa.
- Imani ni msukumo wa maadili mema, hivyo hakuna muumini wa kiume au wa kike asiye na tabia njema; Imani inachochea uwepo wa sifa njema ndani yao.
Marejeo
صحيح مسلم (2/ 1091) (1469).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 359).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 122).
فتح رب البرية بتلخيص الحموية، لابن عثيمين (ص117).
مجموع فتاوى ابن باز (25/ 246).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 282).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن أبي موسى رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «لا نِكَاحَ إِلّا بِوَليٍّ».
Na kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Hakuna ndoa ila kuwe na walii (Msimamizi)".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwanamke haikubaliki ndoa yake ila kwa walii atakayesimamia kufungwa kwa ndoa.
Mafunzo
- Walii ni sharti la kusihi ndoa, ikifanyika bila walii, au mwanamke akajiozesha mwenyewe, haikubaliki.
- Walii ni ndugu wa karibu wa kiume kwa mwanamke, asiozeshwe na walii wa mbali akiwepo walii wa karibu yake.
- Ni sharti kwa walii: Awe mtu mzima (Aliyebalehe), mwanaume, na uwezo wa kupambanua na kujua masilahi ya ndoa, na wawe katika dini moja, msimamizi na msimamiwa, asiyekuwa na sifa hizi hastahiki kuwa msimamizi wa kufungisha ndoa.
Marejeo
سنن أبي داود (3/ 427) (2085).
سنن الترمذي (2/ 392) (1101).
سنن ابن ماجه (3/ 79) (1881).
مسند أحمد (32/ 280) (19518).
البدرُ التمام شرح بلوغ المرام، للمَغرِبي (7/ 57).
إرواء الغليل في تخريج أحاديث منار السبيل، للألباني (6/ 237).
توضِيح الأحكام من بلوغ المَرَام، للبسام (5/ 262).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (7/ 222).
فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (4/ 469).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رَضِي اللهُ عنْها قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَيُّمَا امْرَأَةٍ نَكَحَتْ بِغَيْرِ إِذْنِ مَوَالِيهَا، فَنِكَاحُهَا بَاطِلٌ -ثَلَاثَ مَرَّاتٍ- فَإِنْ دَخَلَ بِهَا فَالْمَهْرُ لَهَا بِمَا أَصَابَ مِنْهَا، فَإِنْ تَشَاجَرُوا فَالسُّلْطَانُ وَلِيُّ مَنْ لَا وَلِيَّ لَهُ».
Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mwanamke yeyote atakayeolewa bila idhini ya walii wake, basi ndoa yake ni batili" Akasema hivyo mara tatu "Ikiwa atamuingilia basi mahari yake ndio itakuwa kwa ajili ya kile alichokifanya kwake, na ikiwa watazozona basi kiongozi ndiye msimamizi wa asiyekuwa na msimamizi".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Alitahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwanamke kujiozesha mwenyewe pasina idhini ya walii wake, nakwamba ndoa yake ni batili, na hilo alilikariri mara tatu, kana kwamba haijatendeka.
Akimuingilia huyu aliyemuoa pasina idhini ya walii wake; hapo mahari kamili itakuwa ni haki yake, kwa lile tendo la ndoa alilolipata katika tupu yake.
Kisha wakizozana mawalii kuwa ni nani mwenye haki ya kufungisha ndoa (na daraja zao zikawa ni sawa) ndoa itafungishwa na yule atakayetangulia miongoni mwao, ikiwa huyu anamtazamo mzuri katika masilahi ya mwanamke huyo, walii akikataa kumuozesha basi hapa mwanamke atakuwa ni sawa nakwamba hana walii; hapa kiongozi au kadhi na mfano wao ndio watakuwa mawalii wake, na vinginevyo hakuna uwalii wa kiongozi anapokuwepo walii.
Mafunzo
- Sharti la kuwa na walii ili kusihi ndoa, na ilielezwa kutoka kwa bin Mundhir kuwa hakuna Swahaba aliyeripotiwa kupingana na hilo.
- Katika ndoa batili mwanamke anastahiki mahari kwa sababu ya kuingiliwa.
- Kiongozi ni walii wa yule asiyekuwa na walii katika wanawake, sawa sawa hilo liwe kwa sababu ya kutokuwepo kwake kabisa, au kwa sababu ya kukataa kumuozesha.
- Kiongozi anazingatiwa kama walii kwa asiyekuwa na walii, katika hali ya kukosekana kwa walii au kushindika kuwepo, na atasimama kadhi badala yake; kwa sababu yeye ndiye mbadala wake katika maswala kama haya.
- Uwalii kwa mwanamke haumaanishi kuwa mwanamke hana haki, bali ana haki, na haifai kwa walii wake kumuozesha ila kwa idhini yake.
- Sharti za ndoa sahihi: Ya kwanza: Kuwaainisha wote wawili, kwa ishara au kwa kuwataja majina au sifa na mfano wake, ya pili: Kuridhia kutoka kwa wote wawili, ya tatu: Mwanamke afungishwe ndoa na walii wake, ya nne: Ndoa iwe na mashahidi.
- Ni sharti kwa walii anayefungisha ndoa: Kwanza awe na akili, la pili: Awe mwanaume, la tatu: Kubalehe, kwa kufikisha kwake umri wa miaka kumi tano, au kwa kujiotea, la nne: Dini iwe moja, hakuna uwalii wa kafiri kwa muislamu wa kiume au wa kike, na vile vile hakuna uwalii wa muislamu kwa kafiri mwanaume au mwanamke, la tano: Uadilifu unaopingana na uovu, na inatosha katika hilo kutazama masilahi ya yule anayesimamia kumuozesha, la sita: Walii awe mwerevu asiwe mpumbavu, nao ni uwezo wa kujua ni nani anayeendana na anayemuozesha, na masilahi ya ndoa.
- Wanachuoni wameweka taratibu za walii kumuozesha mwanamke, haifai kumvuka walii wa karibu isipokuwa wakati wa kukosa kwake sharti, na walii wa mwanamke ni baba yake, kisha wapewa usia wake, kisha babu yake wa upande wa baba na kwenda juu, kisha mwanaye wa kiume, kisha wajukuu zake na kuendelea, kisha kaka yake wa baba na mama, kisha kaka yake wanayechangia baba, kisha watoto wao, kisha baba zake wadogo au wakubwa wa baba na mama mmoja wa baba yake, kisha ami yake wa upande wa baba, kisha watoto wao, kisha ndugu wa karibu kisha anayefuata katika ukoo kama ilivyo katika mirathi, na kiongozi muislamu na anayekaa badala yake kama kadhi ni walii kwa asiyekuwa na walii.
Marejeo
سنن أبي داود (3/ 425) (2083).
سنن الترمذي (2/ 392) (1102).
سنن ابن ماجه (3/ 77) (1879).
مسند أحمد (42/ 199) (25326).
البدرُ التمام شرح بلوغ المرام للمَغرِبي (7/ 62).
توضِيحُ الأحكَامِ مِن بُلوُغ المَرَام، للبسام (5/ 263).
سبل السلام، للصنعاني (2/ 172).
فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (4/ 471).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (7/ 222).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com