عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «أَكْمَلُ الْمُؤْمِنِينَ إِيمَانًا أَحْسَنُهُمْ خُلُقًا، وَخَيْرُكُمْ خَيْرُكُمْ لِنِسَائِهِمْ».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Muumini iliyekamilika zaidi imani yake ni yule mwenye tabia nzuri zaidi kuliko wengine, na mbora wenu ni yule mbora wenu kwa wake zake".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba mtu aliyekamilika zaidi kiimani ni yule itakayekuwa nzuri tabia yake, na hii kwa kuwa na uso mkunjufu, na kutenda mema, na maneno mazuri, na kuacha maudhi.
Na muumini bora kuliko wote ni yule mbora kwa wake zake, kama mke wake na mabinti zake na dada zake na ndugu zake wengine wa kike; kwa sababu wao ndio watu wenye haki zaidi kutendewa tabia nzuri.
Mafunzo
- Ubora wa tabia njema nakuwa tabia njema ni katika imani.
- Matendo ni katika imani, na imani huzidi na kupungua.
- Heshima ya Uislamu kwa mwanamke na himizo la kumtendea wema.
Marejeo
سنن أبي داود (7/ 70) (4682).
سنن الترمذي (2/ 454) (1162).
مسند أحمد ط الرسالة (12/ 364) (7402).
سلسلة الأحاديث الصحيحة وشيء من فقهها وفوائدها، للألباني (1/ 573).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 362).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 130).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (5/ 234).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَبْدِ اللَّهِ بنِ عُمرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «كُلُّكُمْ رَاعٍ فَمَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ، فَالأَمِيرُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْهُمْ، وَالرَّجُلُ رَاعٍ عَلَى أَهْلِ بَيْتِهِ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْهُمْ، وَالمَرْأَةُ رَاعِيَةٌ عَلَى بَيْتِ بَعْلِهَا وَوَلَدِهِ وَهِيَ مَسْئُولَةٌ عَنْهُمْ، وَالعَبْدُ رَاعٍ عَلَى مَالِ سَيِّدِهِ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْهُ، أَلاَ فَكُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ».
Kutoka kwa Abdillah Bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yao: Yakwamba Mtume -Rehema na amani za Allah ziwe juu yake- amesema: "Kila mmoja miongoni mwenu ni mchunga hivyo ataulizwa kuhusu raia wake, kiongozi anayewaongoza watu ni mchunga naye ndiye atakayeulizwa kuhusu wao, na mwanaume ni mchunga kwa watu wa nyumbani kwake naye ndiye wa kuulizwa kuhusu wao, na mwanamke ni mchunga katika nyumba ya mumewe na watoto wake naye ndiye atakayeulizwa kuhusu wao, na mja ni mchunga juu ya mali ya bosi wake, naye ndiye atakayeulizwa juu ya mali hiyo, tambueni kuwa kila mmoja kati yenu ni mchunga na kila mmoja ataulizwa kuhusu raia wake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume rehema na amani zimfikie kuwa kila muislamu katika jamii anamajukumu anayoyasimamia na anayoyabeba, Imamu na kiongozi ni mchunga katika majukumu aliyopewa na Allah kuyasimamia, anatakiwa kuhifadhi sheria zao, na kuwalinda dhidi ya mwenye kuwafanyia uadui, na kumpiga vita adui yao, na kutopoteza haki zao, Na mwanaume kwa watu wa nyumba yake amelazimishwa kuwasimamia kwa matumizi, na kuishi nao vizuri, na kuwasomesha na kuwaadabisha, Na mwanamke katika nyumba ya mumewe ni mchunga kwa kuipangilia vizuri nyumba yake, na kuwalea watoto wake, naye ataulizwa kuhusu hilo, Na mfanyakazi mmilikiwa na mwajiriwa ataulizwa katika mali ya bosi wake kwa kusimamia kuhifadhi kile kilicho mkononi mwake, na huduma zake, naye ataulizwa kuhusu hilo, kila mmoja ni mchunga katika vile alivyopewa kuvichunga, na kila mmoja ataulizwa kuhusu raia wake.
Mafunzo
- Majukumu katika jamii ya kiislamu ni ya watu wote, na kila mmoja ni kulingana na nafasi yake na uwezo wake na majukumu yake.
- Ukubwa wa majukumu ya mwanamke, na hii ni kwa kusimamia haki za nyumba ya mume wake na majukumu yake kwa watoto wake.
Marejeo
صحيح البخاري (3/ 150) (2554).
صحيح مسلم (3/ 1459) (1829).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 369).
إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري، القسطلاني (4/ 326).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ إِيَاسِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي ذُبَابٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا تَضْرِبُوا إِمَاءَ اللَّهِ» فَجَاءَ عُمَرُ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: ذَئِرْنَ النِّسَاءُ عَلَى أَزْوَاجِهِنَّ، فَرَخَّصَ فِي ضَرْبِهِنَّ، فَأَطَافَ بِآلِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نِسَاءٌ كَثِيرٌ يَشْكُونَ أَزْوَاجَهُنَّ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَقَدْ طَافَ بِآلِ مُحَمَّدٍ نِسَاءٌ كَثِيرٌ يَشْكُونَ أَزْوَاجَهُنَّ، لَيْسَ أُولَئِكَ بِخِيَارِكُمْ».
Kutoka kwa Jabiri bin Abdillah -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiwapige vijakazi wa Mwenyezi Mungu" Akaja Omari kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Hivi sasa wanawake wamepata ujasiri kwa waume zao, basi akaruhusu kuwapiga, baada ya muda wakaanza kuzunguka katika familia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake wanawake wengi wakiwashitakia waume zao, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika wamekuja katika familia za Muhammad wanawake wengi wakiwashitakia waume zao, (wanaume) hao si bora kati yenu".
Imepokelewa na Abu Daud na Ibn MajahDarajaSahihi
Maelezo
Alikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwapiga wanawake, akaja kiongozi wa Waumini Omari bin Khattwabi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wanawake wamepata ujasiri kwa waume zao, na wamekuwa na tabia mbovu. Akaruhusu rehema na amani ziwe juu yake kuwapiga kipigo kisichojeruhi inapopatikana sababu ya hilo, kama kukataa kwao kutimiza wajibu wao kwa waume zao na kuwaasi, na mfano wa hayo. Baada ya hapo wakaja wanawake kwa wake wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakishitakia kupigwa na waume zao kipigo chenye kujeruhi, na matumizi mabaya ya ruhusa hii, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Wanaume hao, wanaowapiga wake zao kipigo chenye kujeruhi, si watu bora kwenu.
Mafunzo
- Kumebainishwa fadhila za kuishi vizuri na wanawake, na kwamba kuwavumilia na kufumbia macho yale yanayojitokeza kwao ni bora kuliko kuwapiga.
- Alifanya Mwenyezi Mungu Mtukufu kipigo kuwa hatua ya mwisho katika suluhisho la ujeuri, akasema: "Na wale mnaochelea kutoka kwao katika utiifu, waaidhini (wanasihini), na wahameni katika malazi, na wapigeni. Basi wakiwatii, msitafute njia yoyote dhidi yao. Hakika, Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu, Mkubwa" [An-Nisaai: 34], na njia hizi tatu zimepangwa kwa utaratibu, na si zote kwa wakati mmoja, ataanza kwa nasaha na mawaidha, na kumkubusha, ikiwa itazaa matunda basi Alhamdulillaah, na isipoleta tija amuhame kitandani,, isipoleta tija, ampige kipigo cha kuadabisha nasi cha kulipa kisasi.
- Mwanaume ni msimamizi katika nyumba yake, anawajibu wa kuwalea na kuwaadabisha kwa hekima na mawaidha mazuri.
- Inafaa msomi kujirudi katika majibu yake; pale anapojua matokeo yake na mwisho wake.
- Inafaa kuweka kikao cha majadiliano na kiongozi au mwanachuoni, endapo alipatwa madhara anayeshitaki.
Marejeo
سنن أبي داود (3/ 479) (2146).
سنن ابن ماجه (3/ 152) (1985).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 363).
مرقاة المفاتيح، لعلي القاري (5/ 2127).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ مُعَاوِيَةَ الْقُشَيْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، مَا حَقُّ زَوْجَةِ أَحَدِنَا عَلَيْهِ؟، قَالَ: «أَنْ تُطْعِمَهَا إِذَا طَعِمْتَ، وَتَكْسُوَهَا إِذَا اكْتَسَيْتَ، أَوِ اكْتَسَبْتَ، وَلَا تَضْرِبِ الْوَجْهَ، وَلَا تُقَبِّحْ، وَلَا تَهْجُرْ إِلَّا فِي الْبَيْتِ»
Kutoka kwa Muawia Al-Qushairi radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni zipi haki za mke wa mmoja wetu juu yake?, Akasema: "Ni umlishe pale unapokula, na umvishe unapovaa, au utakapopata kipato, na wala usipige uso, na wala usitoe maneno machafu, na wala usihame isipokuwa ndani ya nyumba".
Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni zipi haki za mke juu ya mume wake? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akataja mambo kadhaa, miongoni mwa hayo ni:
La kwanza: Usijipendelee kwa chakula ukamuacha yeye; bali umlishe kama ulivyo kula wewe.
La pili: Usijipendelee kwa mavazi mazuri, bali umvishe utakapovaa wewe, na ukipata kipato na ukaweza.
La tatu: Usipige ila kuwe na sababu na haja ya kufanya hivyo, na akihitaji kumpiga ima kwa kumuadabisha au kwa kuacha kwake mambo ya faradhi, basi kiwe ni kipigo kisichovunja wala kujeruhi; na uso haupigwi;kwa sababu uso ndio kiungo kitukufu zaidi na kilicho wazi zaidi na kimekusanya viungo vitukufu, na viungo laini.
La nne: Usitukane au kusema: Mwenyezi Mungu auchafue uso wako; usimnasibishe yeye wala chochote katika mwili wake na ubaya ambao ni kinyume na uzuri; kwa sababu Mwenyezi Mungu ndiye aliutengeneza uso wa mwanadamu na mwili wake, na akakipa umbile zuri kila kiumbe, na kutukana umbile kunarudi katika kumtukana muumbaji, Mwenyezi Mungu atuepushe na hilo.
La tano: Usihame ila kitandani, na wala usiondoke hapo, na wala usimhamishie katika nyumba nyingine; na huenda hilo ni katika mambo yaliyozoeleka kutokea baina ya wanandoa.
Mafunzo
- Pupa ya Maswahaba juu ya kutaka kujua haki zilizo juu yao na kuzitekeleza kwao kwa wengine, na kujua haki zao pia.
- Uwajibu wa kutoa matumizi na mavazi na makazi kwa mwanamke juu ya mume wake.
- Katazo la kutoa kasoro ya kimaumbile ima kwa maana au kwa wazi.
- Katika machafu yaliyokatazwa ni kusema: Wewe unatoka katika kabila chafu, na unatoka katika familia mbaya, au mfano wa hayo.
Marejeo
سنن أبي داود (3/ 476) (2142).
سنن ابن ماجه (3/ 56) (1850).
مسند أحمد (33/ 213) (20011).
فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (5/ 184).
سبل السلام، للصنعاني (2/ 322).
توضِيحُ الأحكَامِ مِن بُلوُغ المَرَام، للبسام (6/ 44).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص204).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (8/ 169).
التَّنويرُ شَرْحُ الجَامِع الصَّغِيرِ، للأمير الصنعاني (5/ 369).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ كَانَتْ لَهُ امْرَأَتَانِ فَمَالَ إِلَى إِحْدَاهُمَا، جَاءَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَشِقُّهُ مَائِلٌ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayekuwa na wake wawili akaegemea kwa mmoja wao atakuja siku ya Kiyama upande wake mmoja ukiwa umepinda".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayekuwa na mke zaidi ya mmoja, akawa hakufanya uadilifu baina ya wake zake uadilifu unaowezekana, ikiwemo kuwafanyia usawa katika matumizi na makazi na mavazi na malazi, nikuwa adhabu yake siku ya Kiyama nusu ya mwili wake itakuwa imepinda, na kupinda kwake ni adhabu kwake kwa sababu ya dhulma yake, kama alivyopinda katika muamala wake.
Mafunzo
- Uwajibu wa mgao kwa mwanaume baina ya wake zake, na ni haramu kwake kuegemea kwa mmoja wao na kuwaacha wengine, katika yale anayoyaweza miongoni mwa matumizi, na malazi, na kukutana nao kwa wema, na mfano wa hayo.
- Kufanya usawa katika mgao na mfano wa hayo, katika yale anayoyamiliki mtu, ama yale asiyoyamiliki kama mapenzi na kuegemea kwa moyo, hayo hayaingii katika hadithi, na ndio yaliyokusudiwa katika kauli yake Mtukufu: "Na kwamwe hamtoweza kutenda uadilifu kati ya wanawake hata mkifanya pupa (juu ya hilo) [An-Nisaa: 129].
- Malipo huendana na namna ya matendo, kwa sababu mwanaume alipoegemea upande mmoja duniani kwa mwanamke mmoja akamuacha mwingine, atakuja siku ya Kiyama moja kati pande zake ukiwa umepinda umepishana na mwingine.
- Kuheshimu haki za waja, nakuwa haki hizo hazisameheki; kwa sababu zimejengeka katika uchoyo na kulipizana.
- Inapendeza kuishia mke mmoja, mwanaume akihofia kutowatendea uadilifu wake zake; ili asiangukie katika madhaifu katika dini; amesema Mtukufu: "Ikiwa mtahofia kutowafanyia uadilifu basi (bakini na) mmoja" [An-Nisaa: 3].
Marejeo
سنن أبي داود (3/ 469) (2133).
سنن النسائي (7/ 63) (3942).
سنن الترمذي (2/ 434) (1141).
سنن ابن ماجه (3/ 143) (1969).
مسند أحمد (13/ 320) (7936).
توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (5/ 449).
فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (4/ 631).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (7/ 463).
عون المعبود شرح سنن أبي داود، ومعه حاشية ابن القيم، محمد أشرف العظيم آبادي (6/ 121).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com