Sharti zenye haki zaidi kwenu nyinyi kuzitekeleza ni zile mlizohalalishia tupu
عن عقبة بن عامر رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «أَحَقُّ الشُّرُوطِ أَنْ تُوفُوا بِهِ مَا اسْتَحْلَلْتُمْ بِهِ الْفُرُوجَ».
Imepokewa kutoka kwa Uqbah Bin Aamir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake: "Sharti zenye haki zaidi kwenu nyinyi kuzitekeleza ni zile mlizohalalishia tupu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa sharti bora kabisa kwa kutekelezwa ni zile zilizokuwa sababu ya uhalali wa kustarehe na mwanamke, nazo ni zile sharti za halali anazozitaka mwanamke wakati wa kufunga ndoa.
Mafunzo
- Uwajibu wa kutekeleza sharti ambazo amezitilia umuhimu mmoja kati ya wanandoa wawili kwa mwenzie, isipokuwa sharti itakayoharamisha halali au kuhalalisha haramu.
- Kutekeleza sharti za ndoa kumetiliwa mkazo kuliko sharti zote; kwa sababu huambatana na kuhalalisha tupu.
- Ukubwa wa nafasi ya ndoa katika Uislamu, kiasi ambacho umetilia mkazo juu ya kutimiza sharti zake.
Marejeo
صحيح البخاري (3/ 190) (2721). صحيح مسلم (2/ 1035) (1418). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (2/ 63). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص573).