Amelaaniwa mwenye kumuingilia mke wake kinyume na maumbile
Anamtahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwanaume kumuingilia mkewe katika utupu wake wa nyuma; kuwa amelaaniwa na amefukuzwa kutoka katika rehema ya Mwenyezi Mungu, nalo ni dhambi katika madhambi makubwa.
- Uharamu wa kuwaingilia nyuma wanawake.
- Kustarehe na mke sehemu yoyote katika mwili wake isiyokuwa nyuma inafaa.
- Muislamu anamuingilia mwanamke katika tupu yake ya mbele kama alivyomuamrisha Mwenyezi Mungu; na ama kwa nyuma kuna kuharibu maumbile, na kupoteza kizazi, na kwenda kinyume na asili salama ya viumbe hai, na kuna madhara makubwa kati ya wanandoa.
سنن أبي داود (3/ 489) (2162). السنن الكبرى للنسائي (8/ 200) (8966). مسند أحمد (15/ 457) (9733). نيل الأوطار، للشوكاني (6/ 237). سبل السلام، للصنعاني (2/ 202). توضِيحُ الأحكَامِ مِن بُلوُغ المَرَام، للبسام (5/ 346). فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (4/ 535).