Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Adhabu.

Hadithi 10

Atakayefanya jambo la kustahiki kuadhibiwa, ikaharakishwa adhabu yake basi Mwenyezi Mungu ni muadilifu zaidi juu ya mja wake (hawezi) kumuadhibu mara mbili akhera

عَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ أَصَابَ حَدًّا فَعُجِّلَ عُقُوبَتَهُ فِي الدُّنْيَا فَاللَّهُ أَعْدَلُ مِنْ أَنْ يُثَنِّيَ عَلَى عَبْدِهِ العُقُوبَةَ فِي الآخِرَةِ، وَمَنْ أَصَابَ حَدًّا فَسَتَرَهُ اللَّهُ عَلَيْهِ وَعَفَا عَنْهُ فَاللَّهُ أَكْرَمُ مِنْ أَنْ يَعُودَ فِي شَيْءٍ قَدْ عَفَا عَنْهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Ally -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayefanya jambo la kustahiki kuadhibiwa, ikaharakishwa adhabu yake basi Mwenyezi Mungu ni muadilifu zaidi juu ya mja wake (hawezi) kumuadhibu mara mbili akhera, na atakayefanya jambo la kustahiki kuadhibiwa, Mwenyezi Mungu akamsitiri na akamsamehe, basi Mwenyezi Mungu ni mkarimu zaidi (hawezi) kurudi katika jambo ambalo alikwishalisamehe".
Imepokelewa na Tirmidhi na bin MajahDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa yeyote atakayefanya dhambi zinazohitaji adhabu ya kisheria, kama vile uzinzi au wizi, na akapata adhabu hiyo na ikatekelezwa duniani, basi adhabu hiyo itamfutia dhambi hiyo na kumuondolea adhabu ya Akhera. Hii ni kwa sababu Allah ni mkarimu na mwenye rehema, na hawezi kumuhukumu mja wake kwa adhabu moja mara mbili. Na ikiwa Allah amemsitiri mja wake duniani na hakumuhukumu kwa dhambi hiyo, na akamsamehe na kumghufiria, basi Allah Mtukufu ni mkarimu na mbora zaidi hawezi kurudi katika adhabu ya dhambi aliyoisamehe na kuifuta."

Mafunzo
  1. Ukubwa wa uadilifu wa Mwenyezi Mungu na ukarimu wake na rehema yake.
  2. Kutekeleza adhabu za kisheria katika dunia hufuta dhambi.
  3. Atakayetumbukia katika dhambi ambalo ndani yake ni lazima ajisitiri na kujificha kwa sitara ya Mwenyezi Mungu, na afanye haraka kufanya toba ya kweli.
Marejeo

سنن الترمذي (4/ 312) (2626). سنن ابن ماجه (3/ 627) (2604). مرشد ذوي الحجا والحاجة إلى سنن ابن ماجه والقول المكتفى على سنن المصطفى (15/ 224). التيسير بشرح الجامع الصغير (2/ 399). فيض القدير (6/ 65).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amefaradhisha faradhi basi msizipoteze, na akaweka mipaka basi msiivuke, na akaharamisha vitu basi msivivamie, na akayanyamazia mambo kwa kukuhurumieni si kwa kusahau basi msiyatafute

عَنْ أَبِي ثَعْلَبَةَ الخُشَنِيِّ جُرْثُومِ بن نَاشِرٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَال: «إِنَّ اللَّهَ فَرَضَ فَرَائِضَ فَلَا تُضَيِّعُوهَا، وَحَدَّ حُدُودًا فَلَا تَعْتَدُوهَا، وَحَرَّمَ أَشْيَاءَ فَلَا تَنْتَهِكُوهَا، وَسَكَتَ عَنْ أَشْيَاءَ رَحْمَةً لَكُمْ غَيْرَ نِسْيَانٍ فَلَا تَبْحَثُوا عَنْهَا».
Kutoka kwa Abuu Tha'laba Al-Khushani Jurthuum bin Naashiri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amefaradhisha faradhi basi msizipoteze, na akaweka mipaka basi msiivuke, na akaharamisha vitu basi msivivamie, na akayanyamazia mambo kwa kukuhurumieni si kwa kusahau basi msiyatafute".
Imepokelewa na Addar- Alqutni katika Sunanu yake na wengineoDarajaAmesema Imamu Nawawi: Hadithi hii ni hasan
Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu amewajibisha mambo na akafaradhisha faradhi basi shikamaneni nazo na wala msifanye uzembe katika hayo kwa kuyaacha au kuzembea ndani yake, na akakuwekeeni vizuizi na makemeo yaliyokadiriwa yanayokuzuieni na kukukemeeni katika yale asiyoyaridhia, msizidishe zaidi ya yale yaliyoamrishwa na sheria, na akaharamisha maharamisho kadhaa msiyachukue na wala msiyakaribie, na yasiyokuwa hayo kayaacha na akayanyamazia kwa kuwahurumia waja wake, hivyo yanabakia katika asili ya uhalali wake basi msiyatafute.

Mafunzo
  1. Hadithi ni ushahidi kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mleta sheria, hivyo amri iko mkononi mwake Yeye Mtukufu.
  2. Hadithi imekusanya kanuni za sheria kwa kutoa hukumu na kuhalalisha, hivyo: Hukumu ya kisheria ima iwe imewachwa bila kusemwa au iwe imeelezwa wazi kwa uwajibu au sunna, na ama katazo kwa lazima au kwa hiari, au yaliyokatazwa kwa uharamu au machukizo, au halali.
  3. Nikuwa aliyoyanyamazia Mwenyezi Mungu akawa hakuyafaradhisha, na hakuyawekea mpaka, na wala hakuyakataza, basi hayo ndio halali.
  4. Uzuri wa ufafanuzi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kiasi ambacho ameileta hadithi kwa migawanyiko hii ya wazi.
  5. Uwajibu wa kuhifadhi faradhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  6. Uharamu wa kuvuka mipaka ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Marejeo

سنن الدارقطني (4396). المعجم الكبير للطبراني (22/221). جامع العلوم والحكم (ص617). شرح الأربعين النووية للعثيمين (ص309). توضيح الأحكام من بلوغ المرام (6/ 210).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com