Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa yeyote atakayefanya dhambi zinazohitaji adhabu ya kisheria, kama vile uzinzi au wizi, na akapata adhabu hiyo na ikatekelezwa duniani, basi adhabu hiyo itamfutia dhambi hiyo na kumuondolea adhabu ya Akhera. Hii ni kwa sababu Allah ni mkarimu na mwenye rehema, na hawezi kumuhukumu mja wake kwa adhabu moja mara mbili. Na ikiwa Allah amemsitiri mja wake duniani na hakumuhukumu kwa dhambi hiyo, na akamsamehe na kumghufiria, basi Allah Mtukufu ni mkarimu na mbora zaidi hawezi kurudi katika adhabu ya dhambi aliyoisamehe na kuifuta."
- Ukubwa wa uadilifu wa Mwenyezi Mungu na ukarimu wake na rehema yake.
- Kutekeleza adhabu za kisheria katika dunia hufuta dhambi.
- Atakayetumbukia katika dhambi ambalo ndani yake ni lazima ajisitiri na kujificha kwa sitara ya Mwenyezi Mungu, na afanye haraka kufanya toba ya kweli.
سنن الترمذي (4/ 312) (2626). سنن ابن ماجه (3/ 627) (2604). مرشد ذوي الحجا والحاجة إلى سنن ابن ماجه والقول المكتفى على سنن المصطفى (15/ 224). التيسير بشرح الجامع الصغير (2/ 399). فيض القدير (6/ 65).