Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hukumu za uaibishaji.

Hadithi 2

Hapigwi mtu zaidi ya viboko kumi isipokuwa kama itakuwa katika kutelekeza sheria miongoni mwa sharia za Mwenyezi Mungu

عَنْ أَبِي بُرْدَةَ الْأَنْصَارِيِّ رَضيَ اللهُ عنهُ أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «لَا يُجْلَدُ أَحَدٌ فَوْقَ عَشَرَةِ أَسْوَاطٍ إِلَّا فِي حَدٍّ مِنْ حُدُودِ اللهِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hapigwi mtu zaidi ya viboko kumi isipokuwa kama itakuwa katika kutelekeza sheria miongoni mwa sharia za Mwenyezi Mungu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kupigwa mtu yeyote zaidi ya viboko kumi isipokuwa katika maasi, na pia hakuna maelekezo yoyote yaliyokuja katika sheria kueleza idadi maalumu ya viboko au kipigo au adhabu maalumu, na makusudio yake haizidishwi katika kipigo cha kuadabisha zaidi ya viboko kumi, kama kumpiga mke au mtoto.

Mafunzo
  1. Mipaka ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyoiamrisha au aliyoikataza inaadhabu zinazokomesha hayo, ima zimepangwa katika sheria, au zinarudi kukadiriwa kwake katika masilahi anayoyaona hakimu.
  2. Kutia adabu kunakuwa kwa kiasi kidogo, kwa kiasi cha kuelekeza na kuhofisha, kusizidishwe zaidi ya viboko kumi ikibidi kufanya hivyo, na kilichobora zaidi ni kuwaadabisha pasina kuwapiga, bali kwa kuwaelekeza, na kuwafundisha, na kuwaongoza, na kuwatia hamasa, hilo huleta msukumo mkubwa wa kukubali na upole katika kujifunza, na hali katika nafasi hii hutofautiana sana, inapasa mtu afanye kinachofaa.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 174) (6850). صحيح مسلم (3/ 1332) (1708). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص677). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (5/ 465).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hamtazami Mwenyezi Mungu mtu ambaye kamuingilia mwanaume au mwanamke katika tupu yake ya nyuma

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا يَنْظُرُ اللهُ إِلَى رَجُلٍ أَتَى رَجُلًا أَوِ امْرَأَةً فِي دُبُرٍ».
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hamtazami Mwenyezi Mungu mtu ambaye kamuingilia mwanaume au mwanamke katika tupu yake ya nyuma".
Imepokelewa na Tirmidhiy na Nasai katika kitabu AlkubraaDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ahadi kali ya adhabu kuwa Mwenyezi Mungu hatomtazama mtazamo wa huruma mwanaume aliyemuingilia mwanaume mwenzake katika utupu wake wa nyuma, au mwanamke katika utupu wake wa nyuma, nakuwa hilo ni dhambi kubwa katika madhambi makubwa.

Mafunzo
  1. Mwanaume kumwendea mwanaume mwenzake (Ulawiti) ni katika madhambi makubwa.
  2. Kumwendea mwanamke katika tupu yake ya nyuma ni katika madhambi makubwa.
  3. "Hamtazami Mwenyezi Mungu" Yaani: Mtazamo wa huruma au upole, na si makusudio yake: Kutazama kwa ujumla; kwa sababu Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka hakuna chochote kinachofichikana kwake na hakitoweki machoni mwake chochote.
  4. Matendo haya ni katika machafu makubwa na ni hatari sana kwa binadamu; kwakuwa ndani yake kuna kwenda kinyume na maumbile salama ya kibinadamu, na kupungua kwa kizazi, na kuharibu maisha ya ndoa, na kupandikiza uadui na chuki, na kuingia katika maeneo machafu yenye kutia kinyaa.
Marejeo

سنن الترمذي (2/ 457) (1165). السنن الكبرى للنسائي (8/ 197) (8952). توضِيحُ الأحكَامِ مِن بُلوُغ المَرَام، للبسام (5/ 347). فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (4/ 536). تحفة الأحوذي بشرح جامع الترمذي، للمباركفوري (4/ 276).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com