Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Adhabu ya mwenye kuritadi.

Hadithi 2

Msiadhibu kwa adhabu ya Mwenyezi Mungu

عَنْ عِكْرِمَةَ: أَنَّ عَلِيًّا رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ حَرَّقَ قَوْمًا، فَبَلَغَ ابْنَ عَبَّاسٍ فَقَالَ: لَوْ كُنْتُ أَنَا لَمْ أُحَرِّقْهُمْ لِأَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لاَ تُعَذِّبُوا بِعَذَابِ اللَّهِ»، وَلَقَتَلْتُهُمْ كَمَا قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ بَدَّلَ دِينَهُ فَاقْتُلُوهُ».
Kutoka kwa Ikrima: Ya kwamba Ally radhi za Allah ziwe juu yake aliwachoma watu fulani, zikamfikia taarifa Bin Abbas akasema: Lau ningelikuwa mimi nisingewachoma, kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema: "Msiadhibu kwa adhabu ya Mwenyezi Mungu", na ningewaua tu kama alivyosema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayebadili dini yake basi muuweni".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Alijitahidi Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake akawachoma watu fulani kwa moto, miongoni mwa mazandiki walioritadi kutoka katika Uislamu, zikamfikia taarifa Abdallah bin Abbas radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, akamuunga mkono kwa kuwauwa kwake; lakini akakemea kuwachoma kwa moto. Na akasema: Lau ningelikuwa katika nafasi yake nisingeliwachoma kwa moto; kwa sababu yeye rehema na amani ziwe juu yake alibainisha kuwa haadhibu kwa moto isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa moto, lakini inatosha tu kuwauwa, kwani alisema rehema na amani ziwe juu yake: Atakayeritadi kutoka katika Uislamu na akabadili dini yake kwa dini nyingine basi muuweni.

Mafunzo
  1. Uwajibu wa kumuuwa aliyeritadi kutoka katika dini yake kwa makubaliano ya wanachuoni, nayo inakuwa kwa sharti zake, na haruhusiwi yeyote kufanya hivyo isipokuwa kiongozi na hakimu.
  2. Kauli yake: "Atakayebadili dini yake, basi muuweni" Yaani: Atakayeritadi kutoka katika Uislamu: Hii ni huku ya watu wote kwa wanaume na wanawake.
  3. Aliyeritadi haachwi katika kuritadi kwake bali ataitwa katika Uislamu, asipokubali ndio atauliwa.
  4. Katika hadithi hii kuna katazo la kuadhibu kwa moto, na kwamba mipaka ya sheria haitekelezwi kwa moto.
  5. Ubora wa bin Abbasi radhi za Allah ziwe juu yao, na upana wa elimu yake na utambuzi wake wa hadithi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  6. Hapa kuna adabu ya kumkemea aliyekosea.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 61) (3017). عمدة القاري شرح صحيح البخاري، لبدر الدين العيني (14/ 264). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (8/ 364). توضيح الأحكام شرح بلوغ المرام، لعبد الله البسام (6/ 204). فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (5/ 218). الإفصاح عن معاني الصحاح، لابن هبيرة (3/ 190). التوضيح لشرح الجامع الصحيح، لابن الملقن (18/ 58). نيل الأوطار، للشوكاني (7/ 225).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Walikuja watu kutoka kabila la Ukli au Uraina, wakauchukia mjini Madina

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَدِمَ أُنَاسٌ مِنْ عُكْلٍ أَوْ عُرَيْنَةَ، فَاجْتَوَوْا المَدِينَةَ فَأَمَرَهُمُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِلِقَاحٍ، وَأَنْ يَشْرَبُوا مِنْ أَبْوَالِهَا وَأَلْبَانِهَا، فَانْطَلَقُوا، فَلَمَّا صَحُّوا قَتَلُوا رَاعِيَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَاسْتَاقُوا النَّعَمَ، فَجَاءَ الخَبَرُ فِي أَوَّلِ النَّهَارِ، فَبَعَثَ فِي آثَارِهِمْ، فَلَمَّا ارْتَفَعَ النَّهَارُ جِيءَ بِهِمْ، فَأَمَرَ فَقَطَعَ أَيْدِيَهُمْ وَأَرْجُلَهُمْ، وَسُمِرَتْ أَعْيُنُهُمْ، وَأُلْقُوا فِي الحَرَّةِ، يَسْتَسْقُونَ فَلاَ يُسْقَوْنَ، قَالَ أَبُو قِلاَبَةَ: فَهَؤُلاَءِ سَرَقُوا وَقَتَلُوا، وَكَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ، وَحَارَبُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ.
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Walikuja watu kutoka kabila la Ukli au Uraina, wakauchukia mjini Madina, kwa sababu hali ya hewa ya Madina haikuwafaa. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawaamuru waende katika ngamia wa zaka na wanywe mikojo yake na maziwa yake. Wakaondoka, na baada ya afya yao kurejea, wakamuua mchungaji wa ngamia wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na wakaiba ngamia hao. Habari zikamfikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake mapema asubuhi, basi akatuma watu kuwafuatilia, na wakapatikana kabla ya mchana. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaamuru mikono na miguu yao ikatwe, macho yao yakachomwa moto, na wakatupwa kwenye jangwa la mawe (Al-Harra). Wakawa wakiomba maji, lakini hawakupewa. Abu Qilaba anasema: Watu hawa walifanya wizi, wakafanya mauaji, walitoka katika Uislamu baada ya kuwa Waislamu, na walitangaza vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Walikuja watu kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kutoka katika kabila la Ukli na Uraina wakiwa ni Waislamu, wakapatwa na ugonjwa na maradhi mazito kwao, yakavimba matumbo yao, wakachukia kuishi Madina kwa sababu chakula hakikuwapendeza wala hali ya hewa. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawaamuru waende katika ngamia za sadaka, na wanywe mikojo na maziwa yake. Wakaenda, na walipopona, na wakanenepa, na rangi zao zikarejea kuwa nzuri, wakamuua mchungaji wa ngamia wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na wakachukua ngamia. Habari hiyo ilifika asubuhi na mapema, ndipo Mtume akatuma kikosi cha kuwafuata. Wakawakamata, wakati wa jua kupanda juu wakaletwa wakiwa mateka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Mtume akaamuru mikono yao na miguu yao ikatwe, na macho yao yakatobolewa, kwa sababu walimtendea hivyo mchungaji. Kisha wakatupwa kwenye eneo lenye joto (al-Harra), wakawa wakiwaomba maji lakini hawakupewa mpaka walipokufa. Amesema Abuu Qilaba: Ni kwamba wao waliiba, na wakaua, na wakakufuru baada ya imani yao, na wakampiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Mafunzo
  1. Usafi wa mkojo wa kila kinacholiwa nyama yake.
  2. Sheria ya kujitibu kwa maziwa ya ngamia na mikojo yake.
  3. Sheria ya kufananisha katika kisasi, na katazo la kusulubu litachukuliwa pale panapokuwa hakuna mfanano na kisasi.
  4. Kuua kundi la watu kwa sababu ya mtu mmoja ni sawa, iwe walimuuwa kwa hila au kwa wizi wa kutumia silaha.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 56) (233). صحيح مسلم (3/ 1296) (1671). إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (1/ 298). عمدة القاري شرح صحيح البخاري (3/ 154). التوضيح لشرح الجامع الصحيح (4/ 455). النهاية في غريب الحديث والأثر (1/ 318).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com