Kutoka kwa Omari -radhi za Allah ziwe juu yake-: Ya kwamba siku moja alikuja katika jiwe jeusi akalibusu, kisha akasema: Hakika mimi ninajua kuwa wewe ni jiwe, haudhuru wala haunufaishi, na lau kama nisingemuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikubusu basi nisingekubusu.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Alikuja kiongozi wa waumini Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake katika jiwe jeusi katika kona ya Kaaba akalibusu, kisha akasema: Hakika mimi ninajua kuwa wewe ni jiwe, haudhuru wala haunufaishi, na lau kama mimi nisingelimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikubusu basi nisingekubusu.
Mafunzo
Hapa kuna sheria ya kulibusu jiwe jeusi kwa wenye kuizunguka Al-Kaaba pale wanapolifikia, ikiwezekana hilo kwa wepesi.
Makusudio ya kulibusu jiwe jeusi ni kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Amesema Nawawi: Maana yake nikuwa halina uwezo wa kunufaisha wala kudhuru, nakuwa hilo ni jiwe lililoumbwa kama viumbe vingine ambavyo havidhuru wala havinufaishi, na akalitangaza wazi hilo Omari katika msimu; ili wakashuhudie waliohudhuria katika miji yao, na walihifadhi toka kwake hilo waliohudhuria katika msimu, wanaotoka katika nchi mbali mbali.
Ibada zote zinasimama katika msingi wa sheria; haifanyiki katika ibada hizo ila ile aliyoiweka Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuwa ni sheria.
Ikithibiti ibada kuwa ni sahihi itatekelezwa hata kama hekima yake haikujulikana; kwa sababu watu kuitekeleza na kutii kwao kwa kuifanyia kazi ni katika hekima zilizotakiwa.
Katazo la kubusu vitu ambavyo sheria haikusema kuwa tuvibusu kwa lengo la kuviabudu, kama mawe na mengineyo.
Marejeo
صحيح البخاري (2/ 149) (1597).
صحيح مسلم (2/ 925) (1270).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص394).
تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (3/ 527).
Imepokelewa Kutoka kwa Jundub -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kabla ya kufariki kwake kwa siku tano naye akisema: "Hakika mimi ninajivua dhima kwa Mwenyezi Mungu, kwa mimi kuwa na mwandani (Mtu mwenye mapenzi ya dhati zaidi) miongoni mwenu, hakika Allah Mtukufu kanifanya mimi kuwa mwandani wake, kama alivyomfanya Ibrahim kuwa mwandani, na lau kama ningelijifanyia mwandani katika umma wangu basi ningemfanya Abubakari kuwa mwandani, tambueni kuwa; Hakika wale waliokuwa kabla yenu walikuwa wakiyafanya makaburi ya Manabii wao na wema wao kuwa misikiti, tambueni vyema (kuweni makini)! yakuwa Msijelifanya kaburi langu kuwa msikiti, hakika nakukatazeni msifanye hilo".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alinieleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nafasi yake mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, nakuwa nafasi yake imefikia kiwango cha juu kabisa cha mapenzi, kama alichopata Ibrahim -Amani iwe juu yake-, na kwa ajili hiyo alikanusha kuwa na mwandani zaidi ya Allah; Kwa sababu moyo wake umejaa mapenzi ya Allah Mtukufu na kumtukuza kwake na kumtambua kwake, hivyo hauwezi kupata nafasi kwa yeyote zaidi ya Allah, Na lau kama angelijifanyia mwandani katika viumbe basi angelikuwa ni Abubakari. Kisha akatahadharisha kwa kuchupa mipaka inayofaa katika mapenzi kama walivyofanya Mayahudi na Wakristo katika makaburi ya Manabii wao na wema wao mpaka wakayageuza kuwa miungu ya kishirikina inayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, na wakajenga juu ya makaburi yao misikiti na mahekalu, na akaukataza -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake wasijekufanya mfano vitendo vyao.
Mafunzo
Ubora wa Abubakari -Radhi za Allah ziwe juu yake-, nakuwa yeye ndiye Swahaba bora na mtu bora kwa kuushika ukhalifa wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baada ya kifo chake.
Kujenga misikiti juu ya makaburi ni katika maovu ya umma zilizopita.
Katazo la kuyafanya makaburi kuwa sehemu za ibada kwa ajili ya kuswalia hapo au kuyaelekea na kujengwa juu yake misikiti au makuba, kwa tahadhari ya kutoangukia katika ushirikina kwa sababu ya hilo.
Tahadhari ya kuchupa mipaka kwa watu wema, kwani hupelekea kwenye ushirikina.
Uhatari wa yale aliyoyatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kiasi kwamba aliyatilia mkazo kabla ya kifo chake kwa siku tano.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 377) (532).
شرح النووي على مسلم (5/ 13).
الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص188).
الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص172).
Imepokelewa kutoka kwa Baraa -Radhi za Allah ziwe juu yake: Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake Alisema kuhusu maanswari (watu wa Madina): Hawampendi ila mtu muumini, na hawamchukii ila mnafiki, atakayewapenda Answaar na Mwenyezi Mungu atampenda, na atakayewachukia Mwenyezi Mungu atamchukia".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa, kuwapenda Manswari katika watu wa Madina, ni alama ya ukamilifu wa imani; na hii ni kwa sababu ya kuwahi kwao kuutetea Uislamu na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kuleta amani pia, na kwenda kwao mbio kuwapa hifadhi waislamu, na kutoa kwao mali zao na nafsi zao katika njia ya Mwenyezi Mungu, nakuwa kuwachukia ni alama ya unafiki. Kisha akaweka wazi -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayewapenda Manswari Mwenyezi Mungu humpenda, na atakayewachukia Mwenyezi Mungu humchukia.
Mafunzo
Kuna nafasi kubwa ya Manswari, kuwapenda kwao ni alama ya imani na ni kujiweka mbali na unafiki.
Kuwapenda vipenzi wa Mwenyezi Mungu na kuwatetea ni sababu ya Mwenyezi Mungu kumpenda mja.
Fadhila na ubora wa wale waliotangulia katika Uislamu.
Marejeo
صحيح البخاري (5/ 32) (3783).
صحيح مسلم (1/ 85) (75).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 447).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص257).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (6/ 258).
شرح النووي على مسلم (2/ 63).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 350).
Imesimuliwa kutoka kwa Abuu Huraira, Mwenyezi Mungu amridhie, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake, alisema siku ya (vita vya) Khaibar: "Hakika nitampa bendera hii mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Mwenyezi Mungu ataleta ufunguzi kupitia mikono yake". Akasema Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- sikuwa napenda uongozi wakati huo, fikra zikanipelekea kuwa na matarajio ya kuitwa kwa ajili ya bendera hiyo, akamuita Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Ally bin Abii Twalib -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akampa bendera hiyo, na akasema: "Nenda na usigeuke mpaka Mwenyezi Mungu akufungulie" Akatembea Ally mwendo kidogo kisha akasimama na wala hakugeuka kisha akazungumza kwa sauti ya juu: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kwa lipi niwapige watu? Akasema: "Pigana nao mpaka washuhudie kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wakifanya hivyo watakuwa wamekinga kwako damu zao na mali zao isipokuwa kwa haki yake, na hesabu yao iko juu ya Mwenyezi Mungu".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Aliwaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba kuhusu ushindi wa waislamu kesho dhidi ya Mayahudi wa mji wa Khaibar ambao ni mji uko karibu na Madina, na hii ni kupitia mkono wa mtu atakayempa bendera, nayo ni bendera inayofanywa na jeshi kama nembo, na mtu huyu miongoni mwa sifa zake nikuwa anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda pia.
Na alieleza Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake kuwa hapendi uongozi na hapendi kuwa yeye ndiye anayelengwa isipokuwa kwa siku hiyo; kwa kutaraji yampate aliyoyasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Omari akanyanyua mwili wake ili auone Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kutaraji kuwa anaweza kuitwa kwa ajili ya hilo, na akiwa na pupa na tamaa ya kuchukua bendera hiyo.
Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuita Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake akampa bendera, na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaamrisha jeshi litembee, na lisiondoke katika vita baada ya kukutana na maadui sawa iwe ni kwa mapumziko au kwa kusitisha au kutuliza vita, mpaka Mwenyezi Mungu amfungulie ngome hizi kwa ufunguzi na ushindi.
Akatembea Ally radhi za Allah ziwe juu yake, kisha akasimama isipokuwa hakugeuka; ili asiende kinyume na amri ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, basi Ally radhi za Allah ziwe juu yake akanyanyua sauti yake: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nipigane na watu kwa lipi?.
Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Pigana nao mpaka washuhudie kuwa hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ikiwa watalikubali hilo, na wakaingia ndani ya Uislamu; watakuwa wamezizuia kwako damu zao na mali zao, na zitakuwa haramu kwako, isipokuwa kwa haki yake, yaani: Isipokuwa kama watafanya uhalifu au kosa la jinai watakalostahiki kuuawa kwa kosa hilo kwa mujibu wa hukumu za Uislamu, na hesabu yao itakuwa kwa Mwenyezi Mungu.
Mafunzo
Maswahaba walikuwa wakichukia uongozi kwa sababu ndani yake kuna majukumu makubwa.
Inafaa kuchunguza na kufuatilia kwa ajili ya kuhakiki uzuri wa jambo.
Kiongozi mkuu anatakiwa kumpa maelekezo kamanda wa jeshi katika namna ya kuchukua maamuzi katika kiwanja cha mapambano.
Maswahaba wa Mtume kushikamana na usia wake na kwenda mbio kuutekeleza.
Anayetatizwa na jambo katika yale aliyoelekezwa basi anauliza.
Miongoni mwa dalili za unabii wake rehema na amani ziwe juu yake ni kutoa kwake habari ya ushindi juu ya Mayahudi, kiasi ambacho alieleza kuhusu kuufungua mji wa Khaibar na ikatokea kama alivyoeleza.
Himizo la kuyaendea haraka yale aliyoyaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Hairuhusiwi kumuua aliyetamka shahada mbili isipokuwa yakionekana kwake yanayopelekea kuuawa.
Hukumu za Uislamu zinakwenda katika yale yanayodhihiri kwa watu, na Mwenyezi Mungu ndiye anayesimamia siri zao.
Lengo kubwa la Jihadi ni watu kuingia katika Uislamu.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 1871) (2405).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 127).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 45).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 174).
عن جابر رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «لن يدخلَ النارَ رجلٌ شَهِد بدرًا والحُدَيْبِيَة».
Kutoka kwa Jaabir radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Hatoingia motoni mtu aliyeshuhudia vita vya Badri na Hudaibia".
Imepokelewa na Ahmad na asili yake ipo katika Sahih MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba hatoingia motoni aliyehudhuria vita vya Badri vilivyotokea katika mwaka wa pili wa Hijiria (kalenda ya kiislamu) akipigana pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wala aliyehudhuria suluhu ya Hudaibia, na ndani yake kukiwa na uungaji mkono wa ridhaa (Baiatu ridhiwani) uliotokea katika mwaka wa sita wa Hijiria.
Mafunzo
Hapa kuna fadhila ya watu wa Badri na Hudaibia, na kwamba wao hawatoingia motoni.
Kumebainishwa kwamba Mwenyezi Mungu amechukua dhamana ya dhulma zao, na kuwawezesha kufa katika imani, na kuwaingiza peponi pasina kutanguliwa na adhabu ya moto, hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu humpa amtakaye na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kubwa.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 1942) (2495) .
مسند أحمد (23/ 410) (15262).
المصباح المنير في غريب الشرح الكبير، لأحمد الفيومي (1/ 123).
فيض القدير شرح الجامع الصغير، للمناوي (5/ 302).
المنهاج شرح صحيح مسلم بن الحجاج، للنووي (16/ 57).
عن العِرْباضِ بن ساريةَ رضي الله عنه قال: قام فينا رسول الله صلى الله عليه وسلم ذات يوم، فوَعَظَنا مَوعظةً بليغةً وَجِلتْ منها القلوبُ، وذَرَفتْ منها العيونُ، فقيل: يا رسول الله، وعظتَنَا موعظةَ مُودِّعٍ فاعهد إلينا بعهد. فقال: «عليكم بتقوى الله، والسمع والطاعة، وإن عبدًا حبشيًّا، وسترون من بعدي اختلافًا شديدًا، فعليكم بسنتي وسنة الخلفاء الراشدين المهديين، عَضُّوا عليها بالنواجِذ، وإياكم والأمور المحدثات، فإن كل بدعة ضلالة».
Na kutoka kwa Irbadhi bin Sariya -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Siku moja alisimama kwetu sisi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akatupa mawaidha makali mno, nyoyo zilisisimka kwayo, na macho yalibugujikwa machozi, pakasemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Umetuwaidhi mawaidha ya mwenye kuaga, tuachie usia. Akasema: " Shikamaneni na kumcha Mwenyezi Mungu, na usikivu na utii, hata kama (mzungumzaji) atakuwa mtumwa tena muhabeshi (Muethiopia), na mtakuja kuona baada yangu hitilafu nyingi, basi shikamaneni na Sunna zangu na Sunna za makhalifa (watawala) waongofu, zing'ateni (mzikamatilie) kwa magego, na tahadharini sana na mambo ya kuzushwa, kwani kila uzushi ni upotevu".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwapa mawaidha Masahaba, mawaidha makali, nyoyo ziliogopa kwa mawaidha hayo, na macho yalibugujikwa machozi, Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kana kwamba mawaidha haya ni ya mwenye kuaga, kwa sababu waliona ni jinsi gani alivyokuwa na umakini mkubwa katika mawaidha, wakaomba usia, ili washikamane nao baada yake, akasema: Nakuusieni kumcha Allah Mtukufu, nako ni kwa kutekeleza wajibu na kuacha maharamisho. Na usikivu na utii, yaani: Kwa wenye mamlaka juu yenu, hata kama kiongozi wenu au aliyekutawaleni ni mtumwa, yaani mtu dhalili akawa kiongozi juu yenu, msilibeze hilo, na mtiini, kwa kuchelea kuamsha fitina, bila shaka atakayeishi umri mrefu miongoni mwenu ataona hitilafu nyingi, Kisha akawabainishia njia ya kutoka katika hitilafu hii, nayo ni kwa kushikamana na sunna yake na sunna za mahalifa wanne waongofu baada yake, Abuubakari Swiddiq, na Omari bin Khattwab, na Othman bin Affan, na Ally bin Abii Twalib, radhi za Allah ziwe juu yao wote, na kuzing'ata kwa magego, yaani meno ya mwisho: Anakusudia kwa kauli hii yaani kufanya bidii katika kubaki katika sunna na kushikamana nazo, Na akawatahadharisha na mambo ya kuzushwa yaliyobuniwa ndani ya Dini, kwani kila uzushi ni upotevu.
Mafunzo
Umuhimu wa kushikamana na sunna na kuifuata.
Kuyatilia umuhimu mawaidha na kulainisha nyoyo.
Amri ya kuwafuata mahalifa wanne waongofu baada yake, nao ni Abuubakari na Omari, na Othman, na Ally radhi za Allah ziwe juu ya wote.
Katazo la kuzua katika Dini, nakuwa uzushi wote ni upotofu.
Usikivu na utii kwa atakayesimamia mambo ya waumini katika yale yasiyokuwa maasi.
Umuhimu wa kumcha Mwenyezi Mungu Mtukufu katika nyakati na hali zote.
Hitilafu lazima itokee katika umma huu, na wakati wa kutokea kwake ni lazima kurejea katika Sunna za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na mahalifa waongofu.
Marejeo
الأربعون النووية (ص: 89) (ح28)، سنن أبي داود (7/ 16) (4607)، سنن الترمذي (4/ 408) (2676)، سنن ابن ماجه (1/ 28) (42)، مسند أحمد (28/ 367) (17142)، تحفة الأحوذي (7/ 366)، عون المعبود وحاشية ابن القيم (12/ 235)، شرح الأربعين النووية للعثيمين (ص: 278).
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- siku moja alimkosa Thabiti bin Kaisi, mtu mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mimi naweza kukupa taarifa zake, akamfuata akamkuta akiwa amekaa nyumbani kwake, akiwa ameinamisha kichwa chake, akasema: Ni jambo gani limekusibu? Akasema: Ni shari, alikuwa akinyanyua sauti yake juu ya sauti ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, tayari yameporomoka matendo yake, naye ni katika watu wa motoni, akarudi yule bwana kwa Mtume akamweleza kuwa kasema kadhaa wa kadhaa, mara ya pili akarudi kwake akiwa habari njema, akasema: "Nenda kwamwambie: Wewe si miongoni mwa watu wa motoni, bali ni katika watu wa peponi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Alimkosa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Thabiti bin Kaisi radhi za Allah ziwe juu yake, akamuulizia, mtu mmoja akasema: Mimi naweza kukupatia habari zake, na sababu ya kukosekana kwake, akamwendea akamkuta akiwa na huzuni na kainamisha kichwa chake nyumbani kwake, akamuuliza: Umepatwa na nini? Thabiti akamueleza shari aliyonayo; kwa sababu yeye alikuwa akinyanyua sauti yake juu ya sauti ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na Mwenyezi Mungu kamuonya mwenye kufanya hivyo kwa kubatilika matendo yake, na kwamba yeye ni katika watu wa motoni.
Yule bwana akarejea kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na akamueleza hilo, na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamuamrisha arudi kwa Thabiti na ampe habari njema, yakuwa yeye si miongoni mwa watu wa motoni bali ni katika watu wa peponi, na hii ni kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye sauti ya juu kimaumbile, nakuwa yeye ndiye alikuwa mzungumzaji wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na ni mzungumzaji wa Answari (Watu wa Madina).
Mafunzo
Kumebainishwa ubora wa Thabiti bin Kaisi radhi za Allah ziwe juu yake nakuwa ni katika watu wa peponi.
Kuwajali Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Masahaba na kuwafuatilia.
Hofu ya Masahaba radhi za Allah ziwe juu yao ya kuogopa kuporomoka matendo yao.
Uwajibu wa kuwa na adabu wakati wa kuzungumza na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- enzi za uhai wake, na kupunguza sauti wakati wa kusikia mafundisho yake baada ya kifo chake.
Marejeo
صحيح البخاري (4/ 201) (3613)، صحيح مسلم (1/ 110) (119)، فتح الباري لابن حجر (6/ 620)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (16/ 146)، النهاية في غريب الحديث والأثر (ص 183).
Kutoka kwa Imrani bin Huswain radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Karne bora ni karne yangu, kisha wale wanaowafuata, kisha wale wanaowafuata" Amesema Imrani: Sijui alitaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadaye karne mbili au tatu, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika baada yenu kutakuja watu wanaofanya hiyana na wala hawaaminiwi, na wanatoa ushahidi na wala hawatakwi ushahidi, na wanatoa nadhiri na wala hawatimizi, na utadhihiri kwao unene".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa tabaka bora la watu waliokusanyika katika zama moja ni tabaka ambalo yuko ndani yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Maswahaba zake, kisha wale wanaowafuata katika waumini wale waliowapata Maswahaba na hawakumpata Mtume wa Mwenyezi Mungu, kisha wale wanaowafuata nao ni wafuasi wa wanafunzi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akapata wasi wasi swahaba katika kutaja wale wanaowafuata kwa karne ya nne. Kisha akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hakika baada yao kuna kizazi (kaumu) watafanya hiyana na wala watu hawatowaamini, na watatoa ushahidi kabla ya kutakwa kutoa ushahidi, na wanatoa nadhiri na wala hawatimizi, na wanachupa mipaka katika ulaji na unywaji mpaka unadhihiri kwao unene.
Mafunzo
Karne na kizazi bora katika umri wote wa dunia ni karne aliyoishi Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Maswahaba zake, na imekuja katika Sahihi Bukhari kutoka kwake rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Nimetumwa katika karne bora zaidi za watoto wa Adam karne moja baada ya nyingine, mpaka nikawa katika karne niliyopo ndani yake".
Amesema bin Hajari: Na hadithi hii imepelekea Maswahaba kuwa bora zaidi kuliko wanafunzi wao (Matabii), na Matabii kuwa bora kuliko wanafunzi wao (Mataabii Taabiina), lakini je, ubora huu ni kulingana na ujumla wao au mtu mmoja mmoja? Hapa ni mahala pa kufanya utafiti, na kwa kauli hiyo ya pili ndio iliyochaguliwa na jopo la wanachuoni.
Ishara ya ulazima wa kufuata njia ya karne tatu za mwanzo; kwani kila ambaye zama zake zitakuwa karibu zaidi na zama za utume basi huyo ndiye anastahiki zaidi kuwa na fadhila na elimu na kuiga na kuongoka kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Nadhiri: Ni mtu mwenye ulazima wa kutekeleza sheria kuilazimisha nafsi yake kwa ibada ambayo sheria haikuifanya kuwa lazima kwa kila kauli iliyoielezea.
Ubaya wa hiyana na kutotimiza nadhiri na kufungamana na dunia.
Ubaya wa kutoa ushahidi pasina kutakwa kuutoa, ikiwa mwenye haki analijua hilo, na ama akiwa hajui linaingia katika kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Hivi je nisikuelezeni mashahidi bora kuliko wote, ni yule anayetoa ushahidi kabla hajaulizwa" Kaipokea Muslim.
Marejeo
صحيح البخاري (3/ 171) (2651).
صحيح مسلم (4/ 1964) (2535)، (3/ 1344) (1719).
النهاية في غريب الحديث والأثر (747).
نيل الأوطار (8/ 341).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com