Alikuja kiongozi wa waumini Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake katika jiwe jeusi katika kona ya Kaaba akalibusu, kisha akasema: Hakika mimi ninajua kuwa wewe ni jiwe, haudhuru wala haunufaishi, na lau kama mimi nisingelimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikubusu basi nisingekubusu.
- Hapa kuna sheria ya kulibusu jiwe jeusi kwa wenye kuizunguka Al-Kaaba pale wanapolifikia, ikiwezekana hilo kwa wepesi.
- Makusudio ya kulibusu jiwe jeusi ni kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Amesema Nawawi: Maana yake nikuwa halina uwezo wa kunufaisha wala kudhuru, nakuwa hilo ni jiwe lililoumbwa kama viumbe vingine ambavyo havidhuru wala havinufaishi, na akalitangaza wazi hilo Omari katika msimu; ili wakashuhudie waliohudhuria katika miji yao, na walihifadhi toka kwake hilo waliohudhuria katika msimu, wanaotoka katika nchi mbali mbali.
- Ibada zote zinasimama katika msingi wa sheria; haifanyiki katika ibada hizo ila ile aliyoiweka Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuwa ni sheria.
- Ikithibiti ibada kuwa ni sahihi itatekelezwa hata kama hekima yake haikujulikana; kwa sababu watu kuitekeleza na kutii kwao kwa kuifanyia kazi ni katika hekima zilizotakiwa.
- Katazo la kubusu vitu ambavyo sheria haikusema kuwa tuvibusu kwa lengo la kuviabudu, kama mawe na mengineyo.
صحيح البخاري (2/ 149) (1597). صحيح مسلم (2/ 925) (1270). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص394). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (3/ 527).