Alimkosa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Thabiti bin Kaisi radhi za Allah ziwe juu yake, akamuulizia, mtu mmoja akasema: Mimi naweza kukupatia habari zake, na sababu ya kukosekana kwake, akamwendea akamkuta akiwa na huzuni na kainamisha kichwa chake nyumbani kwake, akamuuliza: Umepatwa na nini? Thabiti akamueleza shari aliyonayo; kwa sababu yeye alikuwa akinyanyua sauti yake juu ya sauti ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na Mwenyezi Mungu kamuonya mwenye kufanya hivyo kwa kubatilika matendo yake, na kwamba yeye ni katika watu wa motoni. Yule bwana akarejea kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na akamueleza hilo, na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamuamrisha arudi kwa Thabiti na ampe habari njema, yakuwa yeye si miongoni mwa watu wa motoni bali ni katika watu wa peponi, na hii ni kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye sauti ya juu kimaumbile, nakuwa yeye ndiye alikuwa mzungumzaji wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na ni mzungumzaji wa Answari (Watu wa Madina).
- Kumebainishwa ubora wa Thabiti bin Kaisi radhi za Allah ziwe juu yake nakuwa ni katika watu wa peponi.
- Kuwajali Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Masahaba na kuwafuatilia.
- Hofu ya Masahaba radhi za Allah ziwe juu yao ya kuogopa kuporomoka matendo yao.
- Uwajibu wa kuwa na adabu wakati wa kuzungumza na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- enzi za uhai wake, na kupunguza sauti wakati wa kusikia mafundisho yake baada ya kifo chake.
صحيح البخاري (4/ 201) (3613)، صحيح مسلم (1/ 110) (119)، فتح الباري لابن حجر (6/ 620)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (16/ 146)، النهاية في غريب الحديث والأثر (ص 183).