At-Tawba
یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔
متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا
إِنَّ عِدَّةَ ٱلشُّهُورِ عِندَ ٱللَّهِ ٱثْنَا عَشَرَ شَهْرًا فِى كِتَـٰبِ ٱللَّهِ يَوْمَ خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ مِنْهَآ أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ۚ ذَٰلِكَ ٱلدِّينُ ٱلْقَيِّمُ ۚ فَلَا تَظْلِمُوا۟ فِيهِنَّ أَنفُسَكُمْ ۚ وَقَـٰتِلُوا۟ ٱلْمُشْرِكِينَ كَآفَّةً كَمَا يُقَـٰتِلُونَكُمْ كَآفَّةً ۚ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلْمُتَّقِينَ 36
{36} Yeye Mtukufu anasema, "Hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu;" yaani, katika hukumu ya Mwenyezi Mungu na majaliwa yake "ni miezi kumi na miwili." Nayo ni miezi hii inayojulikana "katika andiko la Mwenyezi Mungu." Yaani katika hukumu yake ya kimajaliwa, "tangu alipoumba mbingu na ardhi," na akaufanya usiku wake na mchana wake, na akaweka nyakati zake maalumu kwa hivyo akavigawanya katika miezi hii kumi na miwili: "Katika hiyo iko minne mitakatifu." Nayo ni Rajab al-Fard, na Dhul-Qa'dah, na Dhul-Hijjah, na Muharram. Na iliitwa kuwa mitakatifu kwa sababu ya ukubwa wa utakatifu wake, na kwa sababu ni haramu kupigana vita ndani yake. "Basi msidhulumu nafsi zenu humo." Inawezekana kwamba "ndani yake" inamaanisha miezi hii kumi na miwili yote, na kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu aliiweka ili kuwa vipimo kwa waja wake, na kwamba iimarishwe na utiifu kwake, na ashukuriwe Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuwaneemesha kwayo, na kuipa uharamu huo kwa ajili ya masilahi ya waja wake. Basi na watahadhari kuzidhulumu nafsi zao ndani yake. Na inawezekana kwamba "ndani yake" inairudia hii miezi minne mitakatifu tu, na kwamba hili ni katazo kwao kufanya dhuluma ndani yake hasa, pamoja na kukataza kufanya dhuluma katika kila wakati, kwa sababu ya kuongezeka kwa uharamu wake na kwa kuwa udhalimu ndani yake ni mkubwa zaidi kuliko katika miezi mingine. Na katika hayo ni kukataza kupigana vita ndani yake, kulingana na kauli ya yule aliyesema: Uharamu wa Kupigana vita katika miezi mitakatifu haukufutiliwa mbali, kwa kufanyia kazi maandiko ya jumla yanayokataza kupigana vita ndani yake. Na miongoni mwao kuna aliyesema: Hakika uharamu wa kupigana vita ndani yake ulifutiliwa mbali, kwa kuchukua ujumla wa mfano wa kauli yake, "Na piganeni na washirikina wote kama wanavyopigana nanyi nyote." Yaani, piganeni na aina zote za washirikina na wale waliomkufuru Mola Mlezi wa walimwengu wote, wala msimchague yeyote mkampiga vita na mkamuacha mwingine. Bali wafanyeni wote kuwa maadui zenu kama walivyokuwa wao hivyo kwenu, kwani waliwafanya watu wa Imani wote kuwa maadui zao, na hawaachi kuwafikishia chochote cha uovu. Na inawezekana kwamba "wote" ni hali inayohusiana na "na." Kwa hivyo maana yake inakuwa ni: Na piganeni nyote na washirikina. Kwa inakuwa ndani yake ulazima wa waumini wote kutoka kwenda katika vita. Lakini uwezekano wa maana hii ulifutwa na kauli yake, "Na Waumini hawakuwa ni kutoka kwenda wote," hadi mwisho wa aya. "Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamungu" kwa msaada wake, na nusura yake, na kuunga kwake mkono. Basi na mfanye bidii katika kutumia uchamungu katika siri zenu na mambo yenu ya wazi, na kutekeleza utiifu kwake, hasa wakati wa kupigana vita na makafiri. Kwani katika hali hii huenda muumini akaacha kutumia uchamungu katika kuamiliana na makafiri, maadui wapiganao nao.