سیدھے مواد پر جائیں
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
سورت 9

At-Tawba

یہ تفسیر السعدی کا ایک ترجمہ ہے جیسا IslamHouse.com اسے saadi.islamenc.com پر شائع کرتا ہے، اس سائٹ کے صفحات سے لیا گیا۔ سائٹ یہ نہیں بتاتی کہ اس کا ترجمہ کس نے کیا اور وہ کس چھپے ہوئے ایڈیشن کی پیروی کرتا ہے، اور اس کا متن لینے کی کوئی شرائط بیان نہیں کرتی، اس لیے اسے دکھانے کا حق تصدیق شدہ نہیں۔ کسی نے اسے چھپی ہوئی کتاب سے نہیں ملایا اور کسی عالم نے اس کا جائزہ نہیں لیا۔ ہر حصہ ان آیات کے ساتھ ہے جن پر وہ تبصرہ کرتا ہے، اور وہ آیات Tanzil کا قرآنی متن ہیں، جیسا وہاں ہے؛ جس آیت کی سائٹ اپنی الگ تفسیر نہیں دیتی وہ اپنے سے پہلے کے حصے کے ساتھ ہوتی ہے، اور فہرست ایسی ہر آیت کا نام لیتی ہے۔ سبیل نے اس میں سے کچھ نہیں لکھا اور نہ اس کا ترجمہ کیا۔

متن ماخوذ ازsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 کو لیا گیا

آیت 37

إِنَّمَا ٱلنَّسِىٓءُ زِيَادَةٌ فِى ٱلْكُفْرِ ۖ يُضَلُّ بِهِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ يُحِلُّونَهُۥ عَامًا وَيُحَرِّمُونَهُۥ عَامًا لِّيُوَاطِـُٔوا۟ عِدَّةَ مَا حَرَّمَ ٱللَّهُ فَيُحِلُّوا۟ مَا حَرَّمَ ٱللَّهُ ۚ زُيِّنَ لَهُمْ سُوٓءُ أَعْمَـٰلِهِمْ ۗ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلْكَـٰفِرِينَ 37

{37} An-Nasiu ni kile walichokuwa wakikifanya watu wa zama za kabla ya Uislamu (Jahiliyya) katika miezi mitukufu. Na ilikuwa miongoni mwa uzushi wao ni pale walipoona haja yao ya kupigana vita katika baadhi ya nyakati za miezi mitukufu, wakaona kwa rai zao mbovu kwamba waihifadhi idadi ya miezi mitakatifu ambayo Mwenyezi Mungu alikataza kupigana vita ndani yake, na kwamba waicheleweshe baadhi ya miezi mitakatifu au wailete mbele na waeke mahali pake wowote watakao katika miezi inayoruhusiwa vita ndani yake. Kwa hivyo, wanapouweka pahali pake, wanahalalisha kupigana vita ndani yake, basi wakawa wameufanya mwezi unaoruhusika vita ndani yake kuwa hairuhusiki vita ndani yake. Basi hili ni kama Mwenyezi Mungu alivyojulisha kuwahusu, kwamba hilo ni kuzidi katika ukafiri wao na upotofu wao, kwa sababu ya yanayotahadhariwa yaliyo ndani yake. Miongoni mwake ni kwamba walilizua wao wenyewe, na wakalifanya kuwa katika kiwango sawa na sheria ya Mwenyezi Mungu na dini yake. Lakini Mwenyezi Mungu na Mtume wake wako mbali na hilo. Na miongoni mwake ni kwamba waliipindua Dini, kwa hivyo wakafanya halali kuwa haramu, na haramu kuwa halali. Miongoni mwake ni kwamba walimpotoshea Mwenyezi Mungu na waja wake kwa madai yao hayo, na wakawachanganyia dini yao, na wakatumia hadaa na hila katika Dini ya Mwenyezi Mungu. Na miongoni mwake ni kwamba ada zinazohalifu sheria ikiwa zitaendelea kufanywa, basi ubaya wake utaondoka katika nafsi, na pengine zikadhaniwa kwamba ni ada nzuri, kwa hivyo yakatokea yanayotokea miongoni mwa makosa na upotovu. Na ndiyo maana akasema: "wanapotezwa kwa hilo wale waliokufuru. Wanauhalalisha mwaka mmoja na kuharamisha mwaka mwingine, ili wafanye kuwa sawa idadi ya ile (miezi) aliyoitukuza Mwenyezi Mungu." Yaani, ili waafikiane nayo katika idadi zake, "ndiyo wahalalishe yale aliyoharimisha Mwenyezi Mungu. Wamepambiwa ubaya wa vitendo vyao hivi." Yaani, Mashetani waliwapambia matendo mabaya, kwa hivyo wakayaona kuwa ni mazuri kwa sababu ya itikadi iliyopambwa katika nyoyo zao. "Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu makafiri." Yaani, ambao ukafiri na kukadhibisha vilijipaka katika nyoyo zao, na lau zitawajia kila Ishara, hawawezi kuamini.