At-Talaaq
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
ٱللَّهُ ٱلَّذِى خَلَقَ سَبْعَ سَمَـٰوَٰتٍ وَمِنَ ٱلْأَرْضِ مِثْلَهُنَّ يَتَنَزَّلُ ٱلْأَمْرُ بَيْنَهُنَّ لِتَعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ وَأَنَّ ٱللَّهَ قَدْ أَحَاطَ بِكُلِّ شَىْءٍ عِلْمًۢا 12
{12} Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema kwamba ameziumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, na ardhi saba na vilivyomo ndani yake na vilivyomo baina yake, na akateremsha amri ambayo ni sheria na hukumu za dini alizoziteremsha kwa Mitume wake ili kuwakumbusha na kuwaaidhi waja wake, pamoja na amri za kiulimwengu na zile za mipango ya Mwenyezi Mungu ambazo kwazo Yeye huwaendesha viumbe. Yote haya ni ili waja wamjue na wajue kwamba uweza wake umekizunguka kila kitu na elimu yake imekizingira kila kitu. Kwa hivyo, ikiwa watamjua kwa majina yake mazuri na sifa zake takatifu, watamwabudu, watampenda, na watatimiza haki zake, na hayo ndiyo lengo lililokusudiwa katika uumbaji na amri: Kumjua Mwenyezi Mungu na kumuabudu. Basi wakafanya hayo wale waliowezeshwa miongoni mwa waja wema wa Mwenyezi Mungu, nao madhalimu wakayapa kisogo.
Imekamilika tafsiri ya sura hii, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu.