İçeriğe geç
Tafsir As-Saadi - Swahili · As-Saff
Sure 61

As-Saff

Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.

Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı

Ayet 12

يَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَيُدْخِلْكُمْ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ وَمَسَـٰكِنَ طَيِّبَةً فِى جَنَّـٰتِ عَدْنٍ ۚ ذَٰلِكَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ 12

{12} Ndiyo sababu akataja malipo ya huko Akhera, akasema: “Atakusameheni dhambi zenu.” Na hili linajumuisha madhambi madogo na makubwa. Kwa sababu kumuamini Mwenyezi Mungu na kufanya jihad katika njia yake ni mambo yanayofuta madhambi, hata kama ni makubwa, “na atakutieni katika Mabustani yapitiwayo na mito kati yake” yaani, chini ya majengo yake, vyumba vyake, miti yake, mito yake ya maji yasiyovunda, na mito ya maziwa isiyoharibika ladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyosafishwa. Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda, “na maskani mazuri mazuri katika Bustani za milele.” Yaani, zilikusanya uzuri wote wa urefu, kuinuka juu, ujenzi mzuri na mapambo, kiasi kwamba wenye vyumba hivyo katika wale wa juu zaidi wataangaliwa na wakazi wa bustani za mbinguni na waonekane kama nyota inayomeremeta kwenye upeo wa macho wa mashariki au magharibi, na tena mijengo ya bustani za mbinguni baadhi ya matofali yake ni ya dhahabu na zingine ni za fedha, na mahema yake ni ya lulu na marijani, na nyumba zake ni za johari na vito vya thamani zenye rangi nzuri zaidi, kiasi kwamba kutokana na usafi wake inaonekana nje yake kutokea ndani yake, na ndani yake kutokea nje yake, na ndani yake kuna manukato na uzuri usioweza kusifiwa na wenye kusifu, wala hata haukuwahi kupita katika moyo yeyote miongoni mwa walimwengu, haiwezi kuufikia hadi wauone na kufurahia kwa uzuri wake, na macho yao yatue kwa ajili yake. Kwa hivyo katika wa hali hiyo, lau kuwa Mwenyezi Mungu hakuwaumba wakazi wa bustani za mbinguni na akawafanya kuwa katika umbo kamilifu lisilokubali kuisha, basi wangekaribia kufa kutokana na furaha basi ametakasika Yule ambaye hakuna anayeweza kudhibiti sifa zake miongoni mwa viumbe vyake, bali Yeye ni kama alivyojisifu mwenyewe, na yuko juu zaidi ya namna anavyomsifu yeyote katika viumbe vyake, na ni Mwenye baraka nyinyi, Mzuri. Ambaye aliumba nyumba ya neema, na akaweka humo utukufu na uzuri kiasi cha kushangaza akili za viumbe na kuzishika nyoyo zao. Na ametukuka Yule ambaye ana hekima kamilifu, ambayo ni kwamba kama angewaonyesha waja bustani ya mbinguni na wakayaona yaliyo ndani yake ya neema, basi hangebakia nyuma akashindwa kuingia humo yeyote, wala hawangepata raha yoyote ya kuishi katika nyumba hii yenye dhiki, ambayo neema yake imechanganyika na machungu, na furaha zake na taabu zake. Bustani hii iliitwa Edeni; kwa sababu wakazi wake watakaa humo milele na kamwe hawatatoka humo, na wala hawatatafuta pengine pasipo hapo pa kwenda. Malipo hayo makubwa na mazuri ndiyo ushindi mkubwa ambao hakuna ushindi mwingine mfano wake. Haya ndiyo malipo ya kiakhera.