Al-An'aam
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
وَلِتَصْغَىٰٓ إِلَيْهِ أَفْـِٔدَةُ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ وَلِيَرْضَوْهُ وَلِيَقْتَرِفُوا۟ مَا هُم مُّقْتَرِفُونَ 113
{113} Na ndiyo maana Yeye Mtukufu akasema, "Na ili ziyaelekee." Yaani, ili ziyaelekee katika maneno hayo yaliyopambwa "nyoyo za wale wasioiamini Akhera" sababu kutoiamini kwao Siku ya Mwisho na kutokuwa kwao na akili zenye kunufaisha vinawabeba kufanya hivyo; "nao wayaridhie" baada ya kuyaelekea. Kwa hivyo wanayaelekea kwanza, na wanapoyaelekea na wakaiona misemo hiyo ya iliyofanywa kuwa nzuri, Wanairidhia, na ikapambwa katika nyoyo zao, na ikawa ni itikadi thabiti na sifa isiyowaacha, kisha inatokana na hayo kwamba wafanye matendo na maneno wanayoyafanya. Yaani, wanafanya uongo kwa maneno na vitendo, ambayo ni katika yale yasiyoachana na itikadi hizo mbaya. Basi hii ndiyo hali ya wanaotenda maovu, mashetani wa watu na majini, wanaouitikia wito wao. Na ama watu wanaoiamini Akhera na wenye akili kamili na akili zilizo sawa, wao hawadanganywi na misemo hiyo, wala hawapotoshwi na ufichaji huo. Bali, hima yao inaelekezwa katika kujua mambo ya uhakika, kwa hivyo wanaangalia maana ambazo walinganizi wanayalingania. Basi kama ni haki, wanayakubali na kuyafuata, hata ikiwa yatavalishwa misemo mibaya na maneno yasiyotosha. Na ikiwa ni ya batili, wanayarudisha kwa yule aliyeyasema, yeyote yule, hata kama yatavalishwa misemo iliyofanywa kuwa mizuri iliyo laini zaidi kuliko hariri. Na Miongoni mwa hekima ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kuwafanyia Mitume maadui, na batili kuwa na watetezi wanaoilingania ni ili waja Wake wapate majaribio, na mtihani. Ili apambanuke mkweli na mwongo, na mwenye akili timamu na mjinga, na mwenye kuona na kipofu. Na katika hekima yake ni kuwa hatika haya kuna ubainisho wa haki, na kuuweka wazi. Kwa maana, unaangazika, na inakuwa wazi pale batili inapoisimama hupambana nayo na kuipinga. Basi hapo inabainika katika hoja za haki na ushahidi wake yenye kuashiria ukweli wake, na uhakika wake, na ubaya wa batili na ubatili wake ambayo ni katika mahitaji makubwa zaidi ambayo washindani ndani yake wale wanaoshindana.