Qaaf
Bu, as-Saʿdī’nin tefsirinin, IslamHouse.com’un saadi.islamenc.com adresinde yayımladığı hâliyle bir çevirisidir; o sitenin sayfalarından okunmuştur. Site, kimin çevirdiğini ya da hangi basılı neşri izlediğini söylemez ve metnini almak için hiçbir şart belirtmez; bu yüzden bunu gösterme hakkı doğrulanmamıştır. Kimse bunu basılı bir kitapla karşılaştırmadı ve hiçbir âlim gözden geçirmedi. Her bölüm, yorumladığı âyetlerin yanında durur; bu âyetler Tanzil’in Kur’ân metnidir, orada olduğu gibi gösterilir; sitenin kendine ait bir yorum vermediği bir âyet kendisinden önceki bölümle birlikte durur ve dizin böyle her âyeti adıyla anar. Sabīl bunun hiçbirini yazmamış ve çevirmemiştir.
Metin kaynağı:saadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)2026-10-22 tarihinde alındı
بَلْ كَذَّبُوا۟ بِٱلْحَقِّ لَمَّا جَآءَهُمْ فَهُمْ فِىٓ أَمْرٍ مَّرِيجٍ 5
{5} Yaani, "Lakini" maneno yao waliyoyasema si chochote ila ukaidi na kukadhibisha tu haki, ambayo ndiyo aina ya juu kabisa ya ukweli. "ilipowajia; kwa hivyo wamo katika mambo ya mchanganyiko." na wala hawakai imara juu ya kitu chochote, wala hatulii juu ya suala lolote. Kwani wakati mwingine wanasema juu yako: 'Hakika wewe ni mchawi!' Na wakati mwingine wanasema: 'Wazimu!' Na wakati mwingine wanasema: 'Mshairi!' Kadhalika, waliifanya Qur-ani kuwa sehemu mbili, kila mmoja wao akasema juu yake yale ambayo rai yake ya upotovu ilitaka aseme. Na hali kadhalika kila anayeikadhibisha haki. Yeye kila wakati huwa katika jambo lililochanganyika, halijui wala hatulii kwa chochote. Basi utaona mambo yake yanapingana na ya uwongo, kama vile mwenye kufuata haki na kuisadiki, mambo yake huwa yamenyooka, njia yake huwa iko sawasawa, na matendo yake yakasadiki maneno yake.